Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,227
- 26,047
Nimesikia una mpango wa kujenga mabwawa kwa ajili ya kuhifadhi maji ya mvua ili kukabiliana na upungufu wa maji
Ushauri wangu kwako, Achana na hiyo mipango ya kizamani na ya kimaskini ambayo haiendani na wakati uliopo. Kwa mabadiliko haya ya hali ya hewa, napenda kukuhakikishia kuwa huo mradi sio endelevu na utalitia hasara taifa
Nimepita mikoa ambayo kuna mabwawa yalichimbwa kwa ajili ya wafugaji kama Singida, Tabora, Arusha na Dodoma, kusema kweli kwa ukali wa jua mabwawa mengi hata hayo maji hayana yamekauka
Ushauri wangu kwako
1. Kwa mikoa ya Tanga, Pwani, Dsm , Lindi na Mtwara waambie watendaji wako waandike proposal za miradi ya Desalination. Yaani kuchujwa kwa maji chumvi ya bahari kwa ajili ya kunywa. Viwanda hivi Vicente kwenye hii mikoa ili watumie maji ya bahari ya hindi
2. Kwa Mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma Songwe na Tabora hawa watumie maji ya Ziwa Tanganyika. Miradi ijengwe kutoa maji ziwa hili kusambaza kwenye mikoa hiyo
3. Kwa Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Dodoma na Singida hawa mradi wa maji ziwa Victoria ndo usambazwe kwenye mikoa hii yote.
4. Kwa mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma na Iringa, ingawa hii mikoa ina mvua za kuridhisha hasa Mbeya, Ruvuma na Njombe ila ushauri ni kwamba ziwa Nyasa liwe backup na kuwe na miradi ya kuipa maji ya kunywa mikoa hii kutoka ziwa nyasa
5. Kilimanjaro na Arusha. Mikoa hii iunganishwe na mradi wa maji yatokanayo na bahari yatakayokuwa yanatumika katika Mkoa wa Tanga
6. Morogoro
Maji ya mito ya Morogoro na Pwani ndo yatumike kwa ajili ya mkoa wa Morogoro
Hili litaokoa gharama ambazo mnataka kuziweka kwenye miradi ambayo haitakuwa na uhakika wa kuwepo kwa muda mrefu.