Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,508
- 830,009
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!
Wiki 2 zilizopita nilipigiwa simu kutoka Kata ya Shangani, Halmashauli ya Manispaa Mtwara. Aliyenipigia simu alijitambulisha kwa jina la Faudhia Napome, ni mdada hivi. Alinipa taarifa kuwa kaka yake aliyemtambulisha jina la Juma Napome alichukuliwa askali jeshi ambaye ni jirani yao aliyepanga katika nyumba ya Warida Mbelenje. Huyo askari anaitwa Mathias Fabian John anatumia namba ya simu 0767494412.
Baada ya kumchukua, yule kijana hakupatikana tena. Faudhia alikwenda kutoa taarifa Polisi na polisi wakasema kuwa hawana taarifa ya mtu huyo. Hiyo ilikuwa siku ya tarehe 14/12/2025, siku ambayo Juma alichukuliwa na yule askari. Faudhia alipewa taarifa kwa siri na dereva wa bodaboda aliyewabeba hao (askari na Juma), aliwapeleka katika kambi ya Umoja ya Mtwara iliyo karibu na Bandari na Jimbo Kuu Katoliki Mtwara (Palish ya Uaskofuni).
Siku ya Jumatano 17 Desemba 2025, Faudhia alipigiwa simu na Mkuu wa Upepelezi akimtaka aende kituoni. Alipofika kituoni, aliambiwa na Mpepelezi wa Wilaya aende hospitali kutambua maiti. Faudhia alipofika hospitali alimkuta kaka yake akiwa amefarika na mwili ukiwa umeoza unatoa harufu kali.
Mimi nilipopewa taarifa nikafanya juhudi zangu za kiharakati, yule askari Mathias akakamatwa na sasa yupo polisi, hajapelekwa mahakama. Lakini jana, Faudhia alinipigia simu kuwa kuna mtu alimpigia simu akitaka apatiwe fedha. Pia, baba wa Mathias alifika kutoka Singida na yeye aliwashawishi kutoa fedha ili suala hili liishe.
Vyombo vya habari vya Mtwara havijalitangaza hili jambo, na hii hatua ya kutoa fedha inaweza kuharibu kesi. Baba Askofu, unaweza kusaidia familia hii kwa mambo mawili:
1. Polisi Mkoa wa Mtwara waharakishe kufanya upepelezi mtuhumiwa apelekwe mahakamani.
2. Dereva Bodaboda anasema aliwabeba askari wawili pamoja na marehemu katika bodaboda yake, aliyekamatwa ni askari mmoja tu.
3. Waandishi wa habari Mtwara hawajatangaza habari hii. Ni kwa nini hawataki kuitangaza?
Nakutakia kazi njema.
B. K., 28 Desemba 2025.