Mwandishi Mohamed Said
Mchapaji: Africa Proper Education Network, Dar es Salaam
Hiki kitabu kimechapwa mwaka jana 2020 na kinawafaa sana watoto wa shule za msingi kwa kujifunza Kiingereza na historia ya Zanzibar.
Kupitia kitabu hiki mwanafunzi atajifunza mengi katika maisha ya kila siku ya Wazanzibari na utamaduni wao.
LEO SIKU YA VITABU DUNIANI 2
''The Torch on Kilimanjaro''
Mwandishi Mohamed Said
Mchapaji: Oxford University Press, Nairobi
Kitabu hiki kilikuwa katika mradi wa Oxford University Press, Nairobi kwa ajili ya kusomesha Kiingereza na Historia kwa shule za msingi.
Ni kitabu kinachoeleza harakati za kudai uhuru zikiongozwa na Julius Nyerere msimuliaji akiwa mtoto mdogo aliyeshuhudia harakati hizo.
Kitabu hiki ni riwaya inayoeleza matukio ya kweli ya historia ya Tanganyika katika miaka ya 1950 wakati wananchi wamejizatiti kupambana na ukoloni wa Muingereza.
Kitabu kimechapwa mara mbili na hiyo picha hapo ni toleo la pili.
Toleo la kwanza lilichapwa mwaka wa 2007.
Mwandishi: Mohamed Said
Mchapaji: Abantu Publications, Nairobi Kenya.
Mchapaji wa kitabu hiki alikusudia kitabu hiki kitolewe wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya Uchaguzi wa Kura Tatu wa mwaka wa 1958.
Utangulizi wa kitabu ilikuwa uandikwe na mmoja kati ya viongozi wa juu wa CCM ambao ndiyo warithi wa historia ya TANU.
Kitabu kinaeleza historia muhimu sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya chama cha TANU.
Ingawa kitabu kilitoka kwa muda muafaka lakini lengo lililokusudiwa halikufanikiwa.
Kitabu hakikuandikiwa utangulizi kama ilivyokusudiwa wala hakikutumika katika kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Tabora.
Kitabu hiki kimefeli na ni ''out of print,'' yaani hakipatikani.
Duka moja maarufu la vitabu walikikataa kukiuza walikichukua kisha wakakirudisha kwa mchapaji.