Juma Kaseja Atemwa Simba?

Juma Kaseja Atemwa Simba?

Mimi ni mshabiki wa Yanga lakini sikubaliani na upuuzi huu, kipa wetu wa Timu ya Taifa adhalilishwe hivi.

Simba mtimuweni huyo Msomali ana nia ya kuiuwa timu tu. Kibadeni najuwa ni njaa yako tu ndio imekupeleka hapo lakini subili tuwatandike Simba mfululizo uone utakavyoondolewa hapo kama ng'ombe.

wewe ni Matola kweli?
 
Bado namkubali kipa wetu,Tanzania one Juma Kaseja kama kipa ambaye ana uwezo na ningependa aendelee kuidakia Simba. Ameachwa na SSC msimu huu eti kiwango kimeshuka..najua si kweli,labda tumeshindwa kumlipa.#teamSSC
 
Kusema eti kiwango kimeshuka ni uongo na matusi kwa kocha mkuu wa staz kwa kumkubali kama kipa namba 1 wa tanzania, ukisema kushindwa kwa kumlipa pia ni uongo, mi nafikiri ni kumchoka au chuki ya kiongozi 1 wa SSC.
 
Bado namkubali kipa wetu,Tanzania one Juma Kaseja kama kipa ambaye ana uwezo na ningependa aendelee kuidakia Simba. Ameachwa na SSC msimu huu eti kiwango kimeshuka..najua si kweli,labda tumeshindwa kumlipa.#teamSSC
divided opinion bado ni nyingi sana, lakini wengi wanaotaka aondole ni watu wenye fikra finyu sana
 
Kusema eti kiwango kimeshuka ni uongo na matusi kwa kocha mkuu wa staz kwa kumkubali kama kipa namba 1 wa tanzania, ukisema kushindwa kwa kumlipa pia ni uongo, mi nafikiri ni kumchoka au chuki ya kiongozi 1 wa SSC.
kwa makipa ni kweli kuna kipindi kiwangom kinapungua tumesahau ni huyu huyu alimanusura aachwe mwaka jana hadi akasema anamwachia Mungu lakn baadae ndiye amedaka mechi karibu zote
 
[h=3]JUMA KASEJA ATOA MASHARTI ILI KUBAKI SIMBA SC[/h]



Nahodha wa timu ya Simba, Juma Kaseja ameweka sharti la kupatiwa kitita cha dola 40,000 (sh mil 64) ili asaini mkataba mpya.
Kaseja ambaye pia ni kipa namba moja wa timu hiyo aliyeitumia zaidi ya miaka 10, mkatabata wake unamalizika mwezi huu.
Habari kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema kwamba, nyota huyo ametaka kiasi hicho cha fedha ili aweze kuongeza mkataba mwingine wa kuitumikia klabu lakini haitawezekana kwani ni dau kubwa.
Kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alidokeza jana, ingawa bado wanamhitaji kipa huyo, kiasi anachotaka ni kikubwa.


"Kweli bado tunamuhitaji Kaseja, lakini kwa hali iliyopo hatuna kiasi hicho cha fedha. Ngoja tusubiri amalize majukumu yake ya kuitumikia timu ya Taifa halafu tutakaa naye na kuzungumza,"alisema.
Hata hivyo, taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa Kaseja zinaeleza, hata kama uongozi utaafikiana naye kuhusiana na mkataba wake, kuna mambo anataka yawekwe sawa.
Moja ya mastarti hayo ni kuhakikishiwa kwa nafasi yake ndani ya klabu hiyo, pamoja na uongozi kutoingilia benchi la ufundi.
"Unajua Kaseja ameona kuna mambo kadhaa ya kuzungumza na uongozi kwanza ili yaweze kumlinda katika mkataba wake,"alisema
Kaseja ambaye alikuwa tishio katika miaka ya nyuma kiasi cha kupachikwa jina la ‘Tanzania One' katika siku za hivi karibuni kiwango chake kimeonekana kushuka.
Baada ya kuona hali hiyo, uongozi wa Simba katika dirisha dogo la usajili ilimsajili kipa
 
[h=3]JUMA KASEJA ATUPIWA VILAGO RASMI SIMBA[/h]

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI[h=3][/h]

KLABU ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, leo imetangaza rasmi kumtema Nahodha wake ambaye pia ni Nahodha wa timu ya Taifa na Simba, Juma Kaseja, ambaye alikuwa akiwaumiza vichwa viongozi wa Klabu hiyo.


Awali Kaseja, alikuwa akikaririwa na Vyombo vya habari kuwa hajajua
hatima yake na Klabu ya Simba na kuhusishwa ukimya wake na kuhamia Timu ya Azam, ambao awali walionyesha nia ya kumhitaji.


Lakini alipohojiwa Kaseja, alisema kuwa bado alikuwa akihitaji
kupumzika ili kujua kuwa atasaini tena sima ama la, na kwa upande wa
Azam, walipohojiwa kuhusiana na hilo, nao waliruka Kimanga kuonyesha
nia ya kumhitaji Kipa huyo namba moja wa Simba.

Hili la kutunguliwa mabao kama haya si sababu za kutemwa, kipa
huyu nambamoja, lazima kuna sababu iliyojificha nyuma ya pazia,
'Kisiasa zaidi', na wala haiingii akilini kuwambiwa Kaseja ameshuka
kiwangi kama wanavyoeleza mashabiki na viongozi wa Simba.


Akizungumza na mtandao huu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel
Kamwaga alisema kuwa mpaka wanawasili kwenye Uwanja wa Kinesi
jioni ya leo kwa ajili ya mazoezi ya timu hiyo, Kipa huyo hakuwepo
mazoezini ambapo Ezekile, alisema kuwa inawezekana ameathirika kisaikolojia baada ya kufanyiwa vurugu na mashabiki wa Simbo mkoani Morogoro wiki iliyopita.

Nao Uongozi wa Klabu hiyo, leo umeweka wazi kuwa hawatakuwa na
Kipa huyo katika msimu ujao, na kutangaza rasmi kuwa wamevunja
ndoa yao rasmi leo, bila kueleza sababu za kumuacha kipa huyo, huku ikielezwa kuwa huenda ikawa ni dau alilohitaji kipa huyo, jambo ambalo limekanushwa na Uongozi huo.


Hatimaye uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa mwenyekiti wa
kamati ya usajili Zacharia Hans Pope umetangaza rasmi kuachana
na mlinda mlango mkongwe wa timu hiyo Juma Kaseja.

Hans Pope ameyasema hayo katika kipindi cha michezo cha Radio
One jijini Dar es Salaam.
Kaseja akifungwa bao katika moja ya mchezo wake.
Amesema hawatomuongezea mkataba Kaseja na wamempa baraka za
kutafuta timu nyingine.


Kwa muda mrefu Simba ilikuwa ikisuasua kumpa mkataba Kaseja
aliyeidakia Simba kwa takribani miaka 10, na hatimaye leo
wamethibitisha rasmi kumuacha Kaseja.



"Juma ndio basi tena kaka, Kasema yeye na Simba basi,
amesononeshwa mno na jinsi alivyodhalilishwa baada ya mechi ya Morogoro,"alisikika akisema mchezaji mmoja wa Simba baada ya
mazoezi Kinesi leo.


Kaseja alitukanwa na kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba
baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro wakimtuhumu kufungwa mabao ya kizembe.
Milovan, akiwa hoi katika moja ya mchezo akiwa Mocha wa simba.
Ikumbukwe ni hivi karibuni tu Klabu hiyo, ilimtupia vilango aliyekuwa
Kocha Mkuu wake, Milovan Circkovic, kwa madai ya kutotimiza malengo
ya Klabu hiyo kwa kufanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyomalizika hivi karibuni, na sasa leo ni zamu ya Juma Kaseja, huku ikiwa tayari imeshafanya hivyo kwa kuwatoa kwa mkopo wachezaji wake, Vipenzi vya mashabiki wa timu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' aliyepelekwa katika timu ya Coastal Union ya Tanga, na Juma Nyoso, huku ikitabiriwa anayeguata akawa ni Amir Maftah, ambaye ametetewa na Ofisa habari wa timu hiyo kuwa hayupoa mazoezini kwa sabau ana ruhusa maalum kutokana na kufunga ndoa hivi majuzi.

Juma Kaseja katika moja ya kazi nzuri aliyoifanya akiwa na Simba msimu wa 2012
 
[h=3]SIMBA YAWEWESEKA KWA JUMA KASEJA[/h]


kaseja+px.jpg
Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya klabu ya Simba Danny Manembe, kutangaza kutemwa Juma Kaseja, umeibuka mgogoro wa chini kwa chini baada ya baadhi ya viongozi kupinga hatua hiyo.


[h=3][/h]


Habari za ndani ya Simba zilizonaswa na mtandao huu zimedai kuwa uamuzi wa kamati hiyo hauungwi mkono na viongozi wote wa Simba na baadhi ya watu wenye ushawishi mkubwa kwenye klabu hiyo.
Wanaopinga uamuzi wa kamati, wanadai kuwa Kaseja bado ni kipa bora Tanzania kwa sasa na wanaona anastahili kuendelea kuvaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe.
Juzi wakati akitangaza uamuzi huo, Mwenyekiti Manembe alisema kuwa klabu yao ina makipa watatu wapya, hivyo hawana tena sababu ya kuendelea na Kaseja.
Makipa waliopo Simba kwa sasa ni Abel Thaira, Andrew Ntala aliyesajiliwa kutoka Kagera Sugar na Abuu Magube aliyepandishwa kutoka kikosi B.
"Tuna makipa watatu, hawa ni wengi sana kwetu. Hatuwezi tena kuongeza kipa mwingine, hivyo Kaseja tunaachana naye," alisema Manembe.
Akiongeza, Manembe alisema kocha mpya Simba Abdallah Kibadeni katika orodha ya wachezaji anaowataka kwa ajili ya msimu ujao, hakumjumuisha Kaseja hivyo na wao wameamua kuachana naye.
Mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hakutaka jina lake kuandikwa kwenye gazeti alisema: "Kamati yote ya utendaji haimtaki Kaseja ila Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Hanspope (Zakari) na baadhi ya Friends wa Simba wanamuhitaji."
Aliongeza:"Kwa namna hali ilivyo, Hanspope peke yake hawezi kutengua uamuzi wa kamati ya utendaji, sasa kilichobaki ni maneno ya chinichini."
Mtoa habari huyo alisema, yeye binafsi hana shida na Kaseja na anamkubali kuwa ni kipa bora kwa sasa Tanzania na ndiyo maana amepewa unahodha.
"Mimi nipo ndani ya Simba lakini ukiniuliza kwa nini wenzangu wanamchukia Juma siwezi kujua binafsi nilishahoji hakuna sababu yoyote ya maana sana sana ni chuki tu," alisema.
Mbali na suala hilo la Kaseja, pia viongozi wanadaiwa wakirushiana maneno kuhusu suala zima la usajili, ambalo limekuwa likiendeshwa kwa mali kauli kwa baadhi ya wachezaji hususan wanaopandishwa kutoka kikosi cha Simba B.
 
[h=1]JUMA KASEJA"SINA TIMU KWA SASA JAMANII"[/h]
KIPA wa Simba, Juma Kaseja, amesema kwa sasa hawezi kujiunga mapema katika mazoezi ya kikosi hicho kutokana na kwamba hana mkataba na klabu yoyote.
Kauli hiyo ya Kaseja inakuja kufuatia kipa huyo mkongwe kumaliza mkataba wake wa kuitumikia Simba, ambao ulifikia tamati mwishoni mwa msimu uliopita.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kaseja alisema kwa sasa hawezi kujiunga mapema na kikosi hicho alichokitumikia hadi msimu uliopita kwa kuwa hana mkataba na timu hiyo baada ya ule wa awali kumalizika.
Kaseja alisema kwa sasa atakuwa na mapumziko ya siku chache baada ya kumaliza majukumu ya Taifa Stars, ambapo atajua hatima ya timu atakayoichezea msimu ujao ndani ya siku saba kuanzia juzi.
"Ukiniuliza nitajiunga lini katika mazoezi ya Simba, sidhani kama nitakupa jibu zaidi ya sijui, kutokana na sasa sina mkataba wowote na Simba, mimi sasa ni mchezaji huru, mkataba wangu na Simba ulishakwisha," alisema Kaseja huku akiongeza kwa kusema:
"Hivi ninavyoongea na wewe (juzi jioni), ndiyo kwanza hata nyumbani kwangu sijafika, natoka katika kambi ya timu ya taifa, nataka kwanza nikapumzike kwa siku kadhaa na baada ya hapo nadhani ndani ya siku saba nitajua nini nifanye na wapi nitasaini."
 
Young african hatuna shida ya golikipa,Tulionao wanatosha sn na hatujawahi chukua makapi ya simba
Simbw sports club wameingia na sera ya wachezaj wadogo aka makinda but wanasahau kuwa HAKUNA KIJIJI KINACHOKOSA WAZEE NA KWANINI WAMUACHE KWA DHARAU HIVYO?
 
Jamaa anataka 40m na Simba wamechomoa kumpa!
Pale Yanga kama kipa mgana hayuko fiti ingependeza Yanga wampe nafasi ili wasaidiane na barthez klabu bingwa afrika.

Mkuu naheshimu sana mawazo yako. Kaseja hana mapenzi na Yanga, acha aende zake. Hii ni sawa na Mwanaume anayempenda sana 'dame' kiasi cha kumpa chochote kile huku 'dame' mwenyewe akiwa hana mpango na mwanaume huyo. Kaseja amevuna kile alichopanda. Go go go Kaseja.
 
Simba hawana hela ya kuwalipa kina Kaseja ndio maana msimu huu wamesajili watoto ambao itakuwa rahisi kuwalipa na kuwa-control
 
[h=3]EXCLUSIVE: JUMA KASEJA AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUTEMWA NA SIMBA - HAJAPEWA TAARIFA RASMI NA SIMBA....[/h]



Siku moja baada ya klabu ya Simba kupitia mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope kuthibitisha kwamba golikipa mkongwe wa timu hiyo Juma Kaseja hatoongezewa mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo aliyoichezea kwa takribani miaka 10, leo hii mtandao huu umepata nafasi ya kuongea na Juma Kaseja kutaka kujua anazungumziaje uamuzi huo wa Simba.

Kaseja ambaye ni golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania kwa sasa yupo kwao mjini Kigoma alipoenda kupumzika baada ya kumaliza majukumu yake timu ya Taifa hivi karibuni, amezungumza na mwandishi wa mtandao huu Johnson Matinde akiwa kwao Kigoma kuhusu mustakabali wake wa soka baada ya kutemwa na Simba pamoja na mambo mengine.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
C360_2013-06-27-18-20-43.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Juma Kaseja akijifua na vijana wadogo mkoani Kigoma wanaotaka kufuata nyayo zake. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Akizungumzia kuhusu suala la kutoongezewa mkataba mpya na Simba, Juma Kaseja alisema kwamba taarifa hizo yeye amezisikia kwenye vyombo vya habari kama watu wengine walivyosikia na hajapata taarifa rasmi: "Jana nikiwa natokea Tanga nilipokuwa nikapata taarifa za kuhusu masuala yangu na Simba. Klabu kupitia viongozi wake imeshaongea kuhusu suala hili na mie itafika siku nitaongelea kwa kina kuhusu jambo hili, ila kwa sasa ni kweli mimi sio mchezaji wa Simba na nisingependa kuzungumzia kuhusu wao."

Akizungumzia kuhusu mustakabali wake wa soka baada ya kuachana na Simba, Kaseja alisema: "Mimi ni mchezaji mpira, hii ndio kazi yangu hivyo nitaendelea kucheza mpira. Sasa kama unavyoniona nipo hapa kwetu nafanya mazoezi ili niwe bora kwenye kazi yangu. Mengine kuhusu ni timu gani nitachezea msimu ujao ningependa tuyaache kwa sasa, utakapofikia muda muafaka wa kuzungumzia then nitaongelea jambo hilo."

Kaseja akiwa mjini Kigoma amekuwa akijifua kwenye uwanja wa Shule ya msingi Kaluta, shule ambayo Juma Kaseja alisoma na uwanja wa shule hiyo ndio ambao alianzia career yake ya soka na ndio maana kila anapokwenda mapumzikoni nyumbani kwao Kigoma hupenda kufanya mazoezi uwanjani hapo na baadhi ya wachezaji chipukizi.
 
Young african hatuna shida ya golikipa,Tulionao wanatosha sn na hatujawahi chukua makapi ya simba
Simbw sports club wameingia na sera ya wachezaj wadogo aka makinda but wanasahau kuwa HAKUNA KIJIJI KINACHOKOSA WAZEE NA KWANINI WAMUACHE KWA DHARAU HIVYO?

=
chuji1.jpg

=
...tafadhari YANGA TUNAOMBA MPOKEENI KASEJA
Kikosi+cha+Yanga.JPG
 
Unajua viongozi wasanii wa Simba wanaona jamaa kishakuwa na umaarufu sana klabuni na kujiona yuko juu ya wote,hivyo wanataka kuiodoa dhana hiyo.
 
Back
Top Bottom