Juma Duni apita Igunga na kusalimiana na wana Igunga

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
Leo mnamo saa nne asubuhi Mh. juma duni Hadji amepita Igunga na kuwasalimia wananchi na kuwapongeza kwa kumpokea kwa wingi huku akiwaambia wafanye jambo sahihi ifikapo 25 Oct ili wananchi waweze kupata neema ya kupata huduma bora za Afya, Elimu miundombinu N.k aliongea mengi lakini naomba niishie hapo kwani lengo langu ni kutaka kuwafahamisha wale ambao kila wakiamka wanaulizia huyu Mh. yuko wapi kwa hiyo nawaambia kuwa Juma Duni Haji anapiga kazi na anakimbiza Mwizi (CCM) kimya kimya

** Hizo picha zinaonyesha tarehe ya nyuma hilo ni kosa la kamera nilikuwa sijarekebisha tarehe kwa hiyo Marumumba hiyo haitakuwa issue**

P1030574.JPG P1030576.JPG
 
Last edited by a moderator:

GOD THE BOSS

Senior Member
Aug 4, 2015
145
170
Piga mafisiem haooooooo hamtoki mwaka huu, maana hapa babu duni, pale mama regina lowasa, kule lowasa na kingunge yani ccm chaliiiiii.
 
The Elephant

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
4,183
2,000
Hatuwezi chagua mwizi igunga tushazinduka baba
Kuna mwizi zaid ya ccm? Magufuli kuna alichochangia kwenye ilani zaidi ya kusibiri kila kitu kutoka kwa wenye chama? Je, wakat anatafuata wadhamini ndani ya chama zaid ya kusema anasubiri ilani ya ccm kuna kitu amezungumza? Kwa ujumla hana vission ya kuongoza taifa zaidi ya mtu aliyezoea kupangiwa majukumu!

Ndio maana yeye nikushangaa tu!
Kwanini ccm wamemchagua anashngaa! Kwanini nchi ni maskin anashangaa

Tunataka Rais anayeijua Tz siyo wa kushangaa
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
Mkuu hii ndo inanifanya nihoji sasa! Kwa nini usingerekebisha tarehe na unajua tunamtafuta Babu Duni wiki 3 sasa mnashindwa kuweka picha au video?
Kama umeisikiliza VIDEO sidhani kama unaweza kuandika ulichokiandika kwani tarehe inaonyesha ni 1 january 2011 je wakati huo Babu Duni alikuwa CHADEMA?
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,123
2,000
Mkuu hii ndo inanifanya nihoji sasa! Kwa nini usingerekebisha tarehe na unajua tunamtafuta Babu Duni wiki 3 sasa mnashindwa kuweka picha au video?
Mkuu hakuna kitu hapo.wameishiwa hoja wanafanya kazi ya kuleta picha za zamani na mafuriko ya guinea
 
Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
2,000
Kama umeisikiliza VIDEO sidhani kama unaweza kuandika ulichokiandika kwani tarehe inaonyesha ni 1 january 2011 je wakati huo Babu Duni alikuwa CHADEMA?
Ni kweli lakini inaweza ikawa imechukuliwa Agosti 25 2015 pia. Hakuna ushahidi kuwa footage ni ya leo na nafasi ipo kuweka tarehe ya leo. Ndo nasema it's questionable!
 
Pelekaroho

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
1,594
1,500
Ni kweli lakini inaweza ikawa imechukuliwa Agosti 25 2015 pia. Hakuna ushahidi kuwa footage ni ya leo na nafasi ipo kuweka tarehe ya leo. Ndo nasema it's questionable!
Kwani tatizo ni nini, unaamua tu kuamini au kutoamini. Kisha unaendelea na nyuzi nyingine.
 
Livejr

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
1,528
2,000
Kuna mwizi zaid ya ccm? Magufuli kuna alichochangia kwenye ilani zaidi ya kusibiri kila kitu kutoka kwa wenye chama? Je, wakat anatafuata wadhamini ndani ya chama zaid ya kusema anasubiri ilani ya ccm kuna kitu amezungumza? Kwa ujumla hana vission ya kuongoza taifa zaidi ya mtu aliyezoea kupangiwa majukumu!

Ndio maana yeye nikushangaa tu!
Kwanini ccm wamemchagua anashngaa! Kwanini nchi ni maskin anashangaa

Tunataka Rais anayeijua Tz siyo wa kushangaa
Daaah pole sana mkuu nyie chagadema sijui mna matatizo gani, Mkiambiwa Lowassa ni taasisi na akiwa Rais atafanya vile atakavyo mnasema Lowassa lazima afanye kutokana na Ilani ya Chadema /ukawa. Ila kwa Magufuli kusema anasubir Ilan na atafuata Ilani we unasema hana vision mbona mnashindwa kueleweka
 
kson m

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
5,643

Tatizo tope kujaa kichwani badala ya ubongo.chuki zako za kikabila ni chukizo kwa siasa za karne hii.bado unawaza uchagga-wachagga sio watanzania?jadili kuhusu chadema,ccm etc mambo na siasa za kupandikiza chuki za kikabila hazitasaidia chama chako kushinda.enzi hizi watanzania sio mazezeta tena.mlianza chokochoko na kudai cuf ni chama cha kidini,kigaidi nk na hii hutoke majira ya uchaguzi.sasa ni chadema na ukawa mnapandikiza ukabila na ukanda.acheni uzezeta,ushindi haupatikani tena kwa ulaghai.
 
Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,278
2,000
Leo mnamo saa nne asubuhi Mh. juma duni Hadji amepita Igunga na kuwasalimia wananchi na kuwapongeza kwa kumpokea kwa wingi huku akiwaambia wafanye jambo sahihi ifikapo 25 Oct ili wananchi waweze kupata neema ya kupata huduma bora za Afya, Elimu miundombinu N.k aliongea mengi lakini naomba niishie hapo kwani lengo langu ni kutaka kuwafahamisha wale ambao kila wakiamka wanaulizia huyu Mh. yuko wapi kwa hiyo nawaambia kuwa Juma Duni Haji anapiga kazi na anakimbiza Mwizi (CCM) kimya kimya

** Hizo picha zinaonyesha tarehe ya nyuma hilo ni kosa la kamera nilikuwa sijarekebisha tarehe kwa hiyo Marumumba hiyo haitakuwa issue**

View attachment 297216 View attachment 297217
Wee kweli kiboga ni wa Igunga, yaani unaleta picha za kichovu namna hiyo? You can do better than that my broda!!
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom