Julius Mtatiro: Profesa Kitila ni msaliti?

Julius Mtatiro: Profesa Kitila ni msaliti?

PROFESA KITILA NI MSALITI?

Na. Mtatiro J

Kaka yangu na Mwalimu wangu Profesa Kitila Mkumbo amefanya uamuzi mkubwa sana katika maisha yake, lakini huo siyo uamuzi wa mwisho kwa maisha ya duniani.

...
Kama Mungu atamjalia umri mrefu bado anayo nafasi ya kufanya maamuzi makubwa zaidi, na si lazima iwe kwenye siasa.

Kitila amekuwa kiongozi mwandamizi wa CHADEMA (upinzani) akiwa mwalimu wa Chuo Kikuu (Mfanyakazi wa Serikali).

Kitila alihama CHADEMA na kuiasisi ACT (Upinzani kwenda Upinzani) akiwa Mfanyakazi wa Serikali.

Kitila alikubali uteuzi wa JPM kuingia ndani ya serikali ya CCM na kupigania na kutetea sera, itikadi, mbinu za uongozi na kila kinachofanywa na CCM, alikubali yote akiwa mwanachama na kiongozi mwandamizi wa ACT lakini zaidi ni (akiwa serikalini).

Jana Kitila amejivua uanachama wa ACT na kubaki na ukatibu mkuu wa wizara (ameendelea kubaki serikalini).

Ukifuatilia mlolongo wote wa maisha ya Prof. Kitila utagundua kila alipopita bado alikuwa serikalini. Walimu wenzake wengi wamepitia manyanyaso makubwa walipojaribu kuwa upinzani na serikalini kwa wakati mmoja, Kitila ni extra ordinary case, kwa miaka zaidi ya 20 ameweza ku-balance kazi ya kuikosoa serikali waziwazi akiwa mpinzani na mtu wa serikali kwa wakati mmoja.

Wapo watu wamekasirishwa na uamuzi wa Kitila kuachana kabisa na siasa za upinzani na kwa hiyo (automatically) kuipigania CCM. Watu hao ni watu wa ajabu, waliweza kumvumilia Kitila alivyokuwa mpinzani na mserikali kwa wakati mmoja, leo wanashindwaje kumvumilia anapoamua kuwa mserikali moja kwa moja?

Mimi binafsi namshukuru na kumpongeza Kitila kwa uamuzi huu wa sasa, kazi ya kuwa vuguvugu ni ngumu mno, kazi ya kutumikia mabwana wawili ni ngumu zaidi. Naamini kuwa Kitila anaweza kuwa na mchango mkubwa zaidi kwa watanzania katika kazi za Ukatibu Mkuu lakini naamini kazi ya kuipigania serikali inamfaa zaidi kuliko hii ya kupigania demokrasia ya kweli hapa Tanzania.

Na mwisho niwaeleze wanademokrasia wote kujifunza kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia yanayofanywa na wenzetu hata kama hatuyapendi. Wapo watu wanamuita Prof. Kitila "msaliti", hao hawajui lolote! Kitila si msaliti, ni mtu wa serikalini ndiyo maana alivyohama CHADEMA hakurudi kuivuruga. Kama mnataka kujifunza maana halisi ya usaliti, kajifunzeni kwa "Profesa wa Buguruni!".

Namtakia kila la heri Mwalimu Kitila, nimtake aendelee kujumuika nasi kwenye mijadala ya kijamii, sasa akiwa mserikali kwa asilimia 100!

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J
Sasa siungeongelea huyo prof. wa Buguruni moja kwa moja kuliko kuzunguka mkiishiwa hoja si mnyamaze tu
 
Ni kweli kabisa. nakumbuka kuna kipindi Profesa Baregu alikataliwa mkataba pale UDSM, wakati Kitila akizidi kuchanja mbuga, alipata ukuu wa idara, na pia akapanda kuwa Prof. kama unaielewa vizuri Tanzania na UDSM yake, kumbuka yaliyompata Dr. Masumbuko Lamwai, mambo yalimwendea hovyo mpaka akaamua kuingia CCM. sasa mambo safiii. Lamwai alitimuliwa UDSM kwa kosa la kuto-publish. sasa ukifuatilia pale UDSM, wasio-publish ni wengi sana. ila kama uko kimyaaaa, hakuna atakayekuuliza. ila jaribu kuifanya serikali "ikose raha" basi hapo watu watakumbuka kwamba hujapublish.

Kitila amerejea nyumbani, kwa hiyo hakuna cha pekee
 
upinzani wenyew hamueleweki, mara popo mara ndege.... which which???? mlipata umaarufu na ufuasi kutoka kwa wananchi hasa kwa kupinga na kuweka wazi mafisa tz wakiwemo Lowasa, sumaye.. leo mnawalamba viatu.... hakuna matumaini tena... mjipange upya
 
kama mwanadamu huru anahaki ya kuchukua maamuzi aliyochukua.
mfano siwezi kushangaa wala kuduwaa nikisikia Mbowe anahamia CCM.

"all human beings are unpredictable "
hata wewe Brother Mtatiro huwezi kutuhakikishia miaka kumi ijayo utakuwa mpinzani.
maana hapo katikati chochote kinaweza kutokea.
.
 
Fb,insta na twitter kafuta almost kila kitu
Huku kachemsha
Ahahahaha ha hah na huku ndio maana nawakubali sana mods kaburi linamwagiwa zege na nondo siku hiyo hiyo na linakauka muda huo huo kazi inabaki kwa wachimbuaji tu sio mzikaji.
 
kama mwanadamu huru anahaki ya kuchukua maamuzi aliyochukua.
mfano siwezi kushangaa wala kuduwaa nikisikia Mbowe anahamia CCM.

"all human beings are unpredictable "
hata wewe Brother Mtatiro huwezi kutuhakikishia miaka kumi ijayo utakuwa mpinzani.
maana hapo katikati chochote kinaweza kutokea.
Ni kweli kabisa.
 
Utabiri ume
 
Prediction ya kishule shule
 
Back
Top Bottom