Julius Mtatiro: Profesa Kitila ni msaliti?

Julius Mtatiro: Profesa Kitila ni msaliti?

msaliti mkubwa, ila hajakusaliti wewe, wala hajaisaliti CUF.

KITILA
-Kaisaliti kauli yake kuwa rais asichague wasomi kwenye post za kiserikali

-kawasaliti wana ACT, wanaopambana kushika dola, ila mshauri wao kaingia upande wa maadui

-kwa sasa tutegemee kuwasaliti wana nchi hasa wanafunzi wake, ambao aliwafundisha kuwa waje waajiliwe au wawezeshwe na serikali kujiajiri lakin atakuwa upande wa kuwa mapato yote ya serikali ni sawa kujengea uwanja "CHATLE" na kununua midege ila mipanga boi..

-kawasaliti wananchi wa Iramba magh. ambapo aliahidi atarudi kumuondoa mwigulu na mkoloni mweusi, lakini sasa keshakuwa mfuasi mtiifu wa Sizonje, hana habari nao.

automatically mkumbo ni mfuasi wa sera zifuatazo.
- sera za visasi
- sera za chuki kwa usiowapenda utawazushia madawa ya kulevya.
-sera za upendeleo wa kikanda,kidini.
sera za ubabe, na kuikanyaga katiba
sera za kuto ongeza mishahara wtumishi ili hela zikajenge uwanja chatle
Mh, taratibu mkuu.
 
Mwalimu alisema ukishakula nyama ya mtu huachi, msaliti naye husalitiwa. kamdanganya Zitto ili akisaliti chama chake hence CDM iyumbe. Sasa kamwachia zigo lote la chama rafiki yake, kama si usaliti ni nini. Pole Zitto ungekuwa bado CDM nakwambia ndoto ya kukiongoza chama ulichokipenda kwa moyo wako ulikuwa umefika. Ni kosa kuamini kila rafiki
 
Mungu ambariki huyu prof,shida ya maji Dar inaanza kuwa historia,anakusaidia hata wewe Mtatiro utakaporudi Segerea 2020 ,suala la maji halitakuwa kipaumbele tena
Suala la maji alitokaa likawa sio kipaumbele kwa wanasiasa ktk campaign zao na ndiomana CCM hawalimalizi, sio kama wanashindwa kulimaliza, ila ni mtaji wao wa kisiasa.
 
Mtatiro, Julius ama kwa hakika leo umezungumza UKWELI ambao mtu aliyepungukiwa pekee ndie atakaye UPINGA.Kitila amefanya uamuzi SAHIHI KABISA, kwani ni vigumu kutumikia MABWANA WAWILI.
Kazi ya kumtoa Zito alishaikamilisha, na keshazawadiwa hata kama ungekuwa wewe utafanya nini, labda kama ungekuwa na jukumu lingine
 
huyo mtatiro lipumba alipobana ruzuku alikesha kwenye media akilia lia tu. hana jipya ni wale wale tu.
 
Hapana.Si msaliti.Katumia haki yake kujichagulia anachopenda.

Wasaliti ni Prof Lipumba na Dr.Slaa.Hawa mabwana baada ya kujitoa katika vyama vyao wamefanya juu chini kujaribu kuviuwa vyama vyao.
 
DEMOCRACY INAMRUHUSU KUFANYA ALICHOFANYA NI KWA MASLAI MAPANA YA NCHI , CHAMA TAWALA NI WATANZANIA PIA UPINZANI NI WATANZANIA TUNACHOANGALIA SIO MALUMBANO TUNAANGALIA MAENDELEO
 
PROFESA KITILA NI MSALITI?

Na. Mtatiro J

Kaka yangu na Mwalimu wangu Profesa Kitila Mkumbo amefanya uamuzi mkubwa sana katika maisha yake, lakini huo siyo uamuzi wa mwisho kwa maisha ya duniani.

...
Kama Mungu atamjalia umri mrefu bado anayo nafasi ya kufanya maamuzi makubwa zaidi, na si lazima iwe kwenye siasa.

Kitila amekuwa kiongozi mwandamizi wa CHADEMA (upinzani) akiwa mwalimu wa Chuo Kikuu (Mfanyakazi wa Serikali).

Kitila alihama CHADEMA na kuiasisi ACT (Upinzani kwenda Upinzani) akiwa Mfanyakazi wa Serikali.

Kitila alikubali uteuzi wa JPM kuingia ndani ya serikali ya CCM na kupigania na kutetea sera, itikadi, mbinu za uongozi na kila kinachofanywa na CCM, alikubali yote akiwa mwanachama na kiongozi mwandamizi wa ACT lakini zaidi ni (akiwa serikalini).

Jana Kitila amejivua uanachama wa ACT na kubaki na ukatibu mkuu wa wizara (ameendelea kubaki serikalini).

Ukifuatilia mlolongo wote wa maisha ya Prof. Kitila utagundua kila alipopita bado alikuwa serikalini. Walimu wenzake wengi wamepitia manyanyaso makubwa walipojaribu kuwa upinzani na serikalini kwa wakati mmoja, Kitila ni extra ordinary case, kwa miaka zaidi ya 20 ameweza ku-balance kazi ya kuikosoa serikali waziwazi akiwa mpinzani na mtu wa serikali kwa wakati mmoja.

Wapo watu wamekasirishwa na uamuzi wa Kitila kuachana kabisa na siasa za upinzani na kwa hiyo (automatically) kuipigania CCM. Watu hao ni watu wa ajabu, waliweza kumvumilia Kitila alivyokuwa mpinzani na mserikali kwa wakati mmoja, leo wanashindwaje kumvumilia anapoamua kuwa mserikali moja kwa moja?

Mimi binafsi namshukuru na kumpongeza Kitila kwa uamuzi huu wa sasa, kazi ya kuwa vuguvugu ni ngumu mno, kazi ya kutumikia mabwana wawili ni ngumu zaidi. Naamini kuwa Kitila anaweza kuwa na mchango mkubwa zaidi kwa watanzania katika kazi za Ukatibu Mkuu lakini naamini kazi ya kuipigania serikali inamfaa zaidi kuliko hii ya kupigania demokrasia ya kweli hapa Tanzania.

Na mwisho niwaeleze wanademokrasia wote kujifunza kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia yanayofanywa na wenzetu hata kama hatuyapendi. Wapo watu wanamuita Prof. Kitila "msaliti", hao hawajui lolote! Kitila si msaliti, ni mtu wa serikalini ndiyo maana alivyohama CHADEMA hakurudi kuivuruga. Kama mnataka kujifunza maana halisi ya usaliti, kajifunzeni kwa "Profesa wa Buguruni!".

Namtakia kila la heri Mwalimu Kitila, nimtake aendelee kujumuika nasi kwenye mijadala ya kijamii, sasa akiwa mserikali kwa asilimia 100!

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J

Kweli nautamani uproffesa,
Ili nikiona mambo ya baadhi yao,
Sina hamu nao.
 
Kitila alikuwa UD Faculty of Education.....alikua akifundisha psychology course ambazo soko hazina na ofcourse michongo hapati...kwahiyo tusimlaumu na njaa zake
Acha uongo wewe. Kitila ni kati ya maprof. wachache waliokuwa na consultancy na research nyingi pale UDSM. Kwa mazingira ya kitaaluma hiyo ina maana ya pesa na cheo. Fanya homework yako vizuri.
 
Ukienda na mpenzi wako Bar halafu akawa anapapatikia kila mwenye bia nyingi mezani , basi muogope kama ukoma .
 
Mimi kwangu naona alichofanya Kitila ni haki yake kikatiba. Kuliko sasa hivi aendelee kuwa mwanachama wa chana kinachoikosoa serekali anayoitumikia hadharani. Ninaamini kama naye sio mchumia tumbo anaweza kumshauri rais mawazo na jinsi ya kuishi na wapinzani. Ahakikishe anashauri matumizi ya smg sio kinga ya hoja kinzani.
 
Kitila alikuwa UD Faculty of Education.....alikua akifundisha psychology course ambazo soko hazina na ofcourse michongo hapati...kwahiyo tusimlaumu na njaa zake
Ni Tanzania pekee ambayo msomi wa saikolojia ya binadamu anasema haina soko.
Wafungue vituo vya ushauri wa saikolojia.
Dereva wa Tundu hadi Leo yupo Nairobi akirekebishwa saikolojia.
Maugomvi ya kifamilia ni saikolojia syndrome, matalaka, kujinyonga,.
Soko lipo. Family Court!
 
kama mwanadamu huru anahaki ya kuchukua maamuzi aliyochukua.
mfano siwezi kushangaa wala kuduwaa nikisikia Mbowe anahamia CCM.

"all human beings are unpredictable "
hata wewe Brother Mtatiro huwezi kutuhakikishia miaka kumi ijayo utakuwa mpinzani.
maana hapo katikati chochote kinaweza kutokea.
malizia hv, hata wew pia inaezekana kutoka ccm ukahamia upinzani
 
Kitilya siyo msaliti ni mshabiki wa chama tawala kumbuka PM7 ya Msaliti Shonza sasa huyu Waziri huyu katibu
 
Ni maamuzi ya mtu mmoja mmoja (person decision)

Kibaya ni kufanya maamuzi yako binafsi ambayo yatawavuruga wengine.

Unless, everyone has a right to choice.

Back
Top Bottom