Julius Mtatiro awapongeza ACT Wazalendo

Julius Mtatiro awapongeza ACT Wazalendo

albuluushiy

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
1,404
Reaction score
687
HONGERENI ACT - WAZALENDO......
Mwanademokrasia yeyote hapaswi kukasirika pale ambapo chama kipya kinaanza kazi zake huku kikionesha mambo kadha wa kadha mazuri na ya kuigwa na vyama vilivyopo.

Japokuwa chama hiki kipya pia kina mambo lukuki ya kuiga na kujifunza kutoka kwa vyama vikongwe. Kwa uzoefu wangu wa siasa, huwezi kukilinganisha chama hiki kipya na vyama utitiri ambavyo hata ofisi zao hazijulikani ziko wapi na lini wanafanya mkutano mkuu au vikao vya maamuzi.

Ifikie wakati tuwe na sheria ambayo inavilazimu vyama fulani kujifuta moja kwa moja vikishindwa kupata ushindi kiasi fulani kwenye uchaguzi. Nchi inahitaji kuwa na vyama vichache vyenye malengo ya kuleta ushindani wa kweli, Mimi ni muumini wa ushindani na nawakaribisha ACT kwenye ushindani wa kidemokrasia.

Njooni mjenge hoja na tushindanishe sera. Naamini kuwa chama chenu ni platform ya kisiasa kama zilivyo zingine.

J. Mtatiro,
DSM.
 
Ni tofauti kati ya ACT TANZANIA na ACT WAZALENDO, Je vyama viwili tofauti?
 
Uzalendo upi unaozungumziwa? Ningeona kweli wanania ya dhati kwa kuanza kuitukuza lugha ya kiswahili kwenye jina.Jina lao tu halisadifu kile wanachokihubiri.
 
Chadema wanatumia mgongo wa Cuf kujinufaisha, Sasa hivi wanalazimisha Slaa agombee urais halafu msomi prof, lipumba akagombee ubunge Tabora, Chadema wanafiki sana
 
Ni tofauti kati ya ACT TANZANIA na ACT WAZALENDO, Je vyama viwili tofauti?

Hili swali hata wafuasi wa ACT hawawezi kujibu. Kinachoelekea zito kaanzisha tena chama ndani ya chama.
 
Mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe, ya UKAWA hayakuhusu na kwa taarifa yako CUF imeafiki maamuzi yote ndani ya UKAWA na hakuna anayeona mwenzie anataka kutumia mgongo wake ili anufaike kwa namna yoyote ile.

Chadema wanatumia mgongo wa Cuf kujinufaisha, Sasa hivi wanalazimisha Slaa agombee urais halafu msomi prof, lipumba akagombee ubunge Tabora, Chadema wanafiki sana
 
Chadema wanatumia mgongo wa Cuf kujinufaisha, Sasa hivi wanalazimisha Slaa agombee urais halafu msomi prof, lipumba akagombee ubunge Tabora, Chadema wanafiki sana

hawa jamaa wanafiki sana,na wamewaghilibu cuf wapate credibility natabiri umoja huu kufa kabla ya june pale chadema watakapolazimisha askofj slaa ndie awe mgombea wakati hana sifa.
stay tunned.
 
hawa jamaa wanafiki sana,na wamewaghilibu cuf wapate credibility natabiri umoja huu kufa kabla ya june pale chadema watakapolazimisha askofj slaa ndie awe mgombea wakati hana sifa.
stay tunned.

Angalia usije ukafa wewe kabla ukawa haijafa.....
 
Tusijisumbue bure, hawa watu na sera zao za kijamaa eti azimio la Arusha huku viongozi wao wakitembelea Hammer, pia wakidate kimapenzi na mabinti wa bongo movie, kuna ujamaa hapo kweli?
 
Chadema wanatumia mgongo wa Cuf kujinufaisha, Sasa hivi wanalazimisha Slaa agombee urais halafu msomi prof, lipumba akagombee ubunge Tabora, Chadema wanafiki sana

Ccm pia tumuachie msomi wetu Andrew Chenge agombee Urais, hakuna kama yeye Ccm.
 
Hivi CUF wao hawana msamiati unaoitwa msaliti kwenye kamusi yao?

Wawe makini huu umoja wao usiwaambukize misamiati mipya wakapoteana mazima.
 
Jamani angalieni maCCM yalivyowafanyia CUF jana wakati wanarudi kuifuta CCM makunduchi ambapo Maccm 590 walitejesha kadi na kujiunga na CUF ImageUploadedByJamiiForums1427718421.256495.jpg
 
Mtatiro nae huwa hazimtoshi vizuri.

Chama cha kisaliti kimeanzishwa na kufa siku hiyo hiyo unakipongeza kwa lipi?

Chama kina mfaume ZZK.
 
Uzalendo upi unaozungumziwa? Ningeona kweli wanania ya dhati kwa kuanza kuitukuza lugha ya kiswahili kwenye jina.Jina lao tu halisadifu kile wanachokihubiri.

> Umenigusa sana mkuu, uzalendo ni kitu kingine wanafikiri wako sawa kumbe wana mapungufu lukuki. Lakini pia kama chama cha democrasia ya ujamaa vipi nafasi ya kiongozi mkuu ilishindaniwa na watu wangapi? sijaelewa hapa au hiyo nafasi haina democrasia?
 
Back
Top Bottom