Julius Malema wa Tanzania yuko wapi?

mzee mwanakijiji nawewe huko shambani hufiki?!kila siku na jembe lako begani unapiga porojo wenzakeo wanahenyeka na "kilimo cha kufa na kupona".Ok tuyaache hayo maana kilimo kwanza hata mtoto wa mkulima kimemshinda kabaki na porojo tu.Ni hivi watu hawaguswi na bwana Malema kutokana na umri wake bali misimamo yake na kutoogopa kumwambia ukweli mtu yeyote hata yule anaekunywa nae kahawa,akizingua anamgonga tu...wanaojua uhusiano wa zuma na malema wanaelewa nasema nini hapa.

Watanzania hatumihitaji Malema,tunahitaji kiongozi mwadilifu, mwenye dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko na mtetezi wa kweli wa uzalendo, asiyemuonea haya mshikaji yeyote, mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu ya kimapinduzo kwa manufaa ya watu anaowaongoza na siyo anayfanana na mwingine. Nyerere alikuwa kijana alipoipatia Tz uhuru, alikuwa mzalendo kweli lakini alishindwa sababu ya chaguzi mbaya za mifumo ya uongozi aliochagua. Aidha hakuwa amejiandaa akafukuza wazungu huku akijua hana uwezo wa kuendesha miradi aliyoanzisha. Hitaji la watanzania siyo watu wenye mvuto wa sura au hotuba zilizonyooka, hitaji letu siyo umaarufu wa mtu, hitaji letu ni mtu anayweza kuthubutu na akaweza kuleta mabadiliko tunayohitaji kupitia rasilimali zetu. Hatumhitaji Malema! Tunamhitaji mzalendo, mchapakazi, anayechukia mapato ya aibu kivitendo, aliyetayari kutoa sadaka uongozi wake pale atakapoonekama ameshindwa

Julius si mwema au mwenye msimamo kama inavyoaminiwa. Ni opportunist na wanasiasa wanamtumia kwasababu ameshakuwa na influency. Alichochoe kuondoka kwa Mbeki na sintofahamu nyingi ndani ya ANC.

Kinachoudhi ni yeye kuchochea ubaguzi 'racial slur' zile zile walizokuwa walizozipinga. Anataka kuharibu misingi aliyoijenga Mandela ya kuishi kama taifa lenye utangamano. Kwa Kauli za Malema, akina Walter Sissulu, Tambo, Chris Han et al wanajigeuza huko makaburini kwa uchungu na hasira.

Ingawa mada inajirudia tena ni vema nikumbushe kuwa tatizo la taifa letu si umri, ni mmomonyoko wa maadili na ukosefu wa uzalendo.
Kama ni akina Malema mbona tumeshawahi kuwa nao wengi? mmoja ni Pius Msekwa aliyeaingia madarakani akiwa 26?
Angalia safu ya wazee kama akina Salim, Msuya, Warioba, EL, Mramba n.k uone walipewa madaraka katika umri gani.

Tena Nyerere ndiye aliyekuwa rais wa kutumia akina 'Malema'. Miaka 20 baada ya uhuru ukiwa na degree hata miaka 20 Kiongozi.
Hakuwa na chaguo kama sasa. Swali ni je akina 'Malema wetu walifanya kitu gani tofauti hadi tulilie wazaliwe wengine?

Kama kigezo ni 35 below basi tukubaliane kuwa after 35 wasipewe uongozi tena, vinginevyo tutaishia kuwa na akina Msekwa na Kingunge tu kwani watakuwa wamejenga mtandao na wanataka kurithisha watoto wao na kuwalinda hadi watakapokuwa na uwezo wa kujilinda na hapo kuzuia uzao wa Malema wengine.

Sasa hivi ndani ya bunge na serikali hao 35 below wapo wengi, je wamefanya nini cha kutushawishi kuwa ni akina Malema wanaohitaji nafasi?
Si hao akina Ngeleja wasiojua kuandaa bajeti, si hao kina Maige wasiojua ndege za kijeshi zina uhusiano gani na wanyama, si hao akina Manyanya wanaoponda akina malema wenzao bungeni. Si hao akina Nape wanaozunguka kuhubiri mafanikio ya uhuru n.k n.k. (Samahani nalazimika kutaja majina niwe kama Malema asiyeuma maneno)

Kama kuna kitu tunahitaji kuagiza tena kwa FEDEX au DHL kutoka mahali popote duniani ni kurudisha uzalendo, kujenga nidhamu na kusimamia maadili. Huu ndio umasikini wetu, hatuna umasikini mwingine.

Uondoa hilo pendekezo la kipuuzi. Hakuna kitu hapo.

Julius Malima wa TZ ni Nape
Usifanye "mchezo", ushabiki au utani kwenye masuala ambayo ni mustakabali sio wa maisha yako tu bali ya vizazi vyako vijavyo.

Tukiacha ushabiki kupita kiasi wa vyama mi nadhani ni kweli angalau Nape tunaweza kumtaja kama anaweza kuwa Malema wa bongo akipewa support,hii ni kwa sababu Nape angalau aliweza kumvaa Lowassa na genge lake kwenye issue ya uvcmm,halikua jambo rahisi hasa kwa kipindi kile ambapo Lowassa na hilo genge lao walikua na nguvu kubwa ndani ya chama na serikali,si mnakumbuka ilibaki chupu chupu makamba amvue uanachama kama sio Bernard Membe kumshika masikio Jk ambae kina Lowassa kupitia Makamba walikua tayari wameshamuingiza king kwamba dogo "anakiumiza" chama kisa kupinga uuzwaji wa jengo la uvccm.Na hata kwenye vikao vya NEC ni nape ndio alikua na ujasiri wa kumvaa Rostam na mpaka kutukanana nae,nani mwingine labda na Marehemu Chacha wangwe ambae nae alikua na ujasiri wa kumdindishia Mbowe live akitaka kuleta udikteta wake!toka afe Chacha nani anamuweza Mbowe?Zitto alijaribu kumvaa kwenye uchaguzi nini kilitokea..nadhani kila mtu anajua kwamba alikosa ujasiri eti akajitoa kumpisha mzee mzima apite bila kupingwa tena kwenye chama cha demokrasia!!!!!!!!!

Ur cult overzealotry is misplaced..kama unataka kuleta mambo yenu ya dini za kuchonga zilizoanzishwa na watu wasiojua kusoma na kuandika, walokuwa wakiishi mapangoni na kutawadha kwa kutumia mawe, whom I wouldn't let them near my son, let alone my daughter due to their pedofilic inclinations, utafanya la maana ukienda kule kwene jukwaa lenu la myths wenyewe mnaita 'dini na imani'. nadhani kuna watu watakuskiza..hapa umepotea njia bw. Mkamua Kinyesi Maiti (MKM).

Nawewe acha ufala wako, hebu kuwa open minded kidogo,if u christian or muslim is up to u....dini ya mtu inatusaidia nini sisi hapa,kwani umeambiwa tunataka kuungama hapa?...sisi tunamtafuta kijana wa kibongo wa aina ya Julius Malema,kama unae tutajie tumchambue,mbona unachanya taarifa kaka!rudi kwenye mstari kama vipi piga kimya!

Unajua ANC ya sasa hivi ni kama CCM tu. tofauti na ANC ile ya ukombozi yakina S. Biko, N, Mandela.
Huyu Julius Mulema ni Fisadi mtoto anatumia kigezo cha ubaguzi wa rangi kufanikisha Ufisadi wake.
Huyo Mulema, hata bado ajaingia serikali saizi anaendesha gari la kifahari la dola laki mbili, na sio moja tu ni aina tofauti tofauti, ametowa wapi pesa hizo

Nawewe acha ufala wako, hebu kuwa open minded kidogo,if u christian or muslim is up to u....dini ya mtu inatusaidia nini sisi hapa,kwani umeambiwa tunataka kuungama hapa?...sisi tunamtafuta kijana wa kibongo wa aina ya Julius Malema,kama unae tutajie tumchambue,mbona unachanya taarifa kaka!rudi kwenye mstari kama vipi piga kimya!
We khanithi nini? hivi ni nani ameanza kuleta upuuzi wenu wa dini ktk hii thread..shenz type.

Hakuna shaka kuwa julius malema ana ushawishi mkubwa sana ndani na nje ya ANC,na amekuwa haogopi kusema kile anachokiamini, mara nyingi amekuwa akitofautiana na viongozi wa juu wa ANC tena hadharani, mfano amekuwa akisema wazi BEE(Black Economic empowernment) haiwasaidii black south african kama ilivyokusudiwa ila ipo kwa manufaa ya viongozi na familia zao, kwenye hili amemshutumu raisi zuma na familia yake.
Amekuwa akizungumza hadharani kuhusu nationalization of mine which is against sera za ANC.
Kwa upande mwingine ana udhaifu na mapungufu makubwa na amekuwa haishi kutoa kauli tata, aliwahi kuulizwa na muandishi wa habari ktk mkutano Luthuli house juu ya maisha yake ya ufahari, aliishia kumtimua muandishi wa habari mbele ya kamera za kimataifa alimwambia 'hey you bloody agent get out' huku akiita polisi wamtoe nje ya mkutano, ameshitakiwa na anti forum kwa ajili ya hate speech na ule mwimbo aupendae 'DUBUL IBUNU' (Kill the boers), alishawahi pewa suspended sentence na kuamuriwa kuhudhuria 'anger management'. president zuma alishwahi kumwambia malema, 'malema you have to respect elders in the ANC' na nafikiri sasa hivi yuko ktk kipindi kigumu in his political career kuliko wakati wowote ule

Unajua ANC ya sasa hivi ni kama CCM tu. tofauti na ANC hile ya ukombozi yakina S. Biko, N, Mandela.

Huyu Julius Mulema ni Fisadi mtoto anatumia kigezo cha ubaguzi wa rangi kufanikisha Ufisadi wake.

Huyo Mulema, hata bado ajaingia serikali saizi anaendesha gari la kifahari la dola laki mbili, na sio moja tu ni aina tofauti tofauti, ametowa wapi pesa hizo

Utajiri aliokuwa nao umezua maswali mengi kuliko majibu, ana tuhuma mbalimbali ikiwa pamoja na zile za kujipatia tenda isivyo halali kule Limpopo, nyumba ya kifahari anayomiliki sandton, na hiyo anayoijenga ya 16 millions rands, sasa hivi anachunguzwa na south africa revenue authority for tax evasion, na national prosecuting authority wameona kuwa ana kesi ya kujibu juu ya fraud,na hata hii trust fund yake aliyoianzisha ambayo amewaandika mtoto wake na bibi yake inachunguzwa, kwani huenda ikiwa inajihusisha na money laundering, swali linaloulizwa who is behind malema luxurious life.

Mkuu sijui lengo lako ni nini. Kama unataka kijana mwenye umri wa miaka 31 kama Julius Malema anayeweza kuamsha moyo wa watu kuipenda nchi yao naweza kukubaliana nayo.

Lakini baada ya kuangalia CV ya Julius Malema na kuona ni mbaya kupita kiasi, na baada ya kuona jamaa ni racist kuliko hata Botha, baada ya kuona anafananafanana na hali ya kupanda kwa Hitler, baada ya kuona kuwa hate politics anazoleta zimesababisha Afrika Kusini kupoteza wawekezaji wengi, baada ya kuona jamaa ni fisadi (yaani anapata pesa kwa kuwatishia watu na kuiba hela za chama-ili na yeye akae kimya kwa kuwa anajua wakubwa wameiba nini), baada ya kusikia anajenga nyumba ya Rand milioni 16 yenye bunker, sijui lengo ni nini, baada ya kusikia kuwa jamaa bila kujua maana ya sovereign country ni nini (alisema atatuma jeshi kuwasaidia wapinzani Botswana kuondoa serikali anayodai kuwa inawaunga mkono mabeberu, yaani hajui hata kuwa nchi yake Afrika Kusini ni beberu pia), baada ya kuona kuwa anatumia kipaji cha kuongea lakini hana vision yoyote.......naona mungu kuwa Tanzania asitokee mtu kama yeye. Naomba Mungu hata siku moja asijetokea mtu mwenye akili za ajabu kama Julius Malema.

Alikuwepo Mzee Idd Simba, alikuwa anajaribu kuleta ubaguzi kwa kisingizio cha sera ya uzawa, lakini bahatai alipuuzwa. So ni better iishie hapo, isiendelee.Malema ni hatari. Huu ni mtazamo wangu.

Bora hata mnafiki anaeweza kuwambia wazungu kwamba ni majizi which is true haya Mazungu ni maparasite mabaya sana hayana kitu in absence of Africa...if we manage to get people like Malema hakika tutasonga mbele..kati ya Viongozi wa Vijana wa vyama Afrika alipinga sana ukoloni unaoendelea kule Libya mimi namkubali sana,,,

Tatizo ni kuwa hawa wazee wa miaka 60 walipoingia madarakani enzi zao ndio walikuwa vijana wenyewe wenye maneno motomoto. Ndio walikuwa kina Mulema wenyewe. Tukitaka kurudia makosa tuanze kuangalie umri kama kigezo cha msingi. Miaka hamsini baadaye kizazi kingine kitatushangaa na wao wataanza kulilia vijana tena. UONGOZI NI UWEZO SIYO UMRI.

obama3.jpg

obama4.jpg

[The Sectera Edge, a combination phone-PDA that's been certified by the National Security Agency as being acceptable for Top Secret voice communications and Secret e-mail and Web sites.]

Mkuu MM Umri kwa kizazi cha sasa kinachokimbia kwa kasi kubwa kitekinolojia ni kitu cha msingi sana.Viongozi wengi wa Afrika pamoja na kuwa na umri mkubwa basi wangezungukwa na vijana wenye umri mdogo lakini akili sharp kiakili na maamuzi,wamebaki kuzungukwa na wazee wenye kuamini wao kwa kuwa walishiliki kuanzisha Nchi basi wao ndio Nchi na pasipo wao hakuna Nchi,hatimae wameishia kukimbia Nchi zao na wengine utawala umewashinda.

Ukitizama Taifa kama Marekani Marais waliopata kufanya vizuri katika Taifa hilo ni wale waliokuwa na umri mdogo wa miaka 40-55.Rais John F Kennedy,Bill Williama Clinton na Barak Obama ni Moja ya Matokeo ya aina ya viongozi vijana kwa umri waliofanya mengi na wanaendelea kufanya maamuzi yenye umakini mkubwa sana na wenye faida kwa Taifa lao.

Rais Obama wakati anaingia kwenye Uchaguzi alikuwa anatumia simu ya aina ya BlackBerry ambapo leohii kitanzania zinamatumizi makubwa sana kwa kada ya vijana wa kuanzia miaka [15-45] na kama kuna wanaotumia wakiwa na umri zaidi ya hapo basi ni wale ambao ni wapenzi au wadau wa tekinolojia kitaaluma na si kimatumizi kama matumizi ya kawaida ambayo kiongozi mwenye mwamko alipaswa kuwa nayo.

Kwa sasa hivi Rais huyo atakuwa anatumia simu yenye mfumo huo hapo juu [The Sectera Edge, a combination phone-PDA ] ,lakini akiwa bado yuko ndani ya tekinolojia ya mawasiliano ya kasi.Lakini mtangulizi wake George W Bush yeye aliacha kutumia simu ya mkononi na email pindi tu alipoingia madarakani na alipotoka madarakani ndio ameanza upya kutumia mtandao.

Hivyo umri kwa kizazi cha sasa ni swala la msingi ukizingatia kuwa kama Watanzania tulio wengi wanachagua kiongozi kwa kuchaguliwa wao nani awaongoze, mjadala wa sifa za kiongozi pia uzingatie kichwani kwake akili yake ni akili yenye uwezo wa kukabidhiwa mamlaka na kuyasimamia na si matope ambayo kwa umma uliomwingi wa Watanzania wamezoezwa kuwa kiongozi ni yule wanaeonyeshwa kupitia chama tawala.

Julius-Malema-007.jpg

As much as baadhi ya watu humu wapenda status quo lakini ukweli uko pale pale.

We are tired of these political elites ambao ni mzao wa Nyerere. watu wana miaka zaidi ya 60 lakini utawaona kwenye front bench politics na hawaishi ku play politics mpaka na uchumi

Kwa nchi ambayo 70% ya population ni vijana wenye chini ya miaka 30 its a disgrace kuona over 90% ya viongozi wake (ambao so far wametufikisha kwenye hii balaa ndio wamejikita kila kona) wana umri uliozidi 60 na kuendelea

Imagine the likes of wasira au Anna Abdallah au etc ni kama ma dinosaurs na utashangaa kuona watu bila aibu wala haya wanakuja humu JF kumfanyia kampeni Lowassa aje kuwa rais baada ya ku mess up alipokuwa madarakani

Binafsi nadhani wananchi have had enough of these old men and their oldboy network, tukaachana na mambo ya kuwapa nafasi wanawake kwa sababu tuu ya jinsia na politcal correctness na pia tukaacha hizi party politics ambazo hazitufikishi mahala

Nashauri kama wapo the likes of Julius Malema ambaye jana gazeti la Forbes limemtabiria kuwa anaweza kuja kuwa the next SA President simply because wananchi have had enough of those from elite backgrounds that are out of touch na wananchi wa kawaida

To be honest I care less na chama atakachotoka the next Julius Malema wetu awe CCM au CHADEMA au CUF, I care less as long as huyo mtu ni below 35 years na ambao wana uwezo.

Kiukweli sijamuona malema hapa Tanzania kijana huyo ni mtata na anajiamini sana (Anaamini kile anachosema) hauogopi ukweli hata kama unawaumiza wakubwa wake.

Hapo kwenye red katiba yetu inasema ili uchaguliwe kuwa rais inabidi uwe na miaka 41,

Ntajisikia vibaya kama leo hii tunafikiria kutengeneza watu wajinga, wabinafsi na wenye mitazamo isiyoendana kabisa na mazingira ya sasa kama Julius Malema hapa Tanzania. Huyu bwana watu tunamjua vizuri kweli?? Mbona yeye ni famous kama yule wa Tanzania wakati wa uchaguzi wa 2005??? Mmesikia skendo zake za rushwa na ufisadi??
Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza!!!

Hakuna shaka kuwa julius malema ana ushawishi mkubwa sana ndani na nje ya ANC,na amekuwa haogopi kusema kile anachokiamini, mara nyingi amekuwa akitofautiana na viongozi wa juu wa ANC tena hadharani, mfano amekuwa akisema wazi BEE(Black Economic empowernment) haiwasaidii black south african kama ilivyokusudiwa ila ipo kwa manufaa ya viongozi na familia zao, kwenye hili amemshutumu raisi zuma na familia yake.
Amekuwa akizungumza hadharani kuhusu nationalization of mine which is against sera za ANC.
Kwa upande mwingine ana udhaifu na mapungufu makubwa na amekuwa haishi kutoa kauli tata, aliwahi kuulizwa na muandishi wa habari ktk mkutano Luthuli house juu ya maisha yake ya ufahari, aliishia kumtimua muandishi wa habari mbele ya kamera za kimataifa alimwambia 'hey you bloody agent get out' huku akiita polisi wamtoe nje ya mkutano, ameshitakiwa na anti forum kwa ajili ya hate speech na ule mwimbo aupendae 'DUBUL IBUNU' (Kill the boers), alishawahi pewa suspended sentence na kuamuriwa kuhudhuria 'anger management'. president zuma alishwahi kumwambia malema, 'malema you have to respect elders in the ANC' na nafikiri sasa hivi yuko ktk kipindi kigumu in his political career kuliko wakati wowote ule

ANC's Julius Malema lashes out at 'misbehaving' BBC journalist

Furious youth leader ejects reporter from Johannesburg press conference calling him a 'bloody agent' with 'that white tendency'
Julius malema insults bbc journalist - YouTube A firebrand South African youth leader today threw a BBC journalist out of a press conference, accusing him of "white tendency" and calling him a "bastard", "bloody agent" and "small boy".
Julius Malema, president of the youth wing of the African National Congress, exploded in rage when Jonah Fisher, a white Briton, interrupted him at the ANC's headquarters in Johannesburg.
The row began when Malema, who has just returned from Zimbabwe, praised Robert Mugabe's Zanu-PF party and poured scorn on the "Mickey Mouse" opposition. He mocked exiles linked to the Movement for Democratic Change, led by Zimbabwe's prime minister, Morgan Tsvangirai, for using offices in Sandton, a wealthy suburb of Johannesburg.
"They can insult us here from air conditioned offices of Sandton," Malema told journalists at Luthuli House. "We are unshaken. They must stop shouting at us. They must go and fight for their battle in Zimbabwe and win … why are they speaking in Sandton and not Mashonaland or Matabeleland?"
As Malema went on, Fisher interjected: "You live in Sandton."
Evidently stung, Malema replied: "Let me tell you, this is a building of a revolutionary party and you know nothing about the revolution."
Fisher pressed: "So they're not welcome in Sandton but you are?"
Malema snapped: "Here you behave or else you jump."
This prompted laughter from Fisher and others.
"Don't laugh," Malema growled.
Fisher commented that the situation had become a "joke".
Malema then erupted, asking for a security guard to eject Fisher and telling him: "If you're not going to behave, you're [sic] going to call security to take you out. This is not a newsroom, this is a revolutionary house and you don't come here with that tendency.
"Don't come here with that white tendency. Not here. You can do it somewhere else. Not here. If you've got a tendency of undermining blacks, even where you work, you are in the wrong place. Here you are in the wrong place."
Fisher responded: "That's rubbish. That's absolute rubbish."
Malema continued: "You can go out. Rubbish is what you have covered in that trouser. That is rubbish. You are a small boy, you can't do anything."
Collecting his dictaphone and walking out, Fisher said: "I didn't come here to be insulted."
Malema bellowed after him: "Go out. Go out. Bastard! Go out. You bloody agent!"
Later, asked to explain why he had ejected the BBC journalist, Malema said: "This is Luthuli House. This is the headquarters of a revolutionary party which has liberated the people of South Africa. It's not a playground. Here you come, you restrain yourself, you behave in a manner that is befitting of being the headquarters of the African National Congress. It's not a beer hall here.
"You don't howl here. Especially when we speak, you behave like you are in an American press conference? It's not America. It's Africa. You must behave in an African way. You are in Rome, you do what the Romans do … if you feel offended by the removal of this gentleman, you are most welcome to walk."
The opposition Democratic Alliance said the incident proved that Malema was "South Africa's Mugabe".
Mpowele Swathe, shadow minister of rural development, said: "Malema's hysterical, conspiracy theory-laden attack on the BBC is painfully reminiscent of the frequent claims by Mugabe that he is the victim of 'malicious propaganda by external forces'.
"His actions, in throwing the journalist out of the press conference, are no different to Mugabe's censorship of the press in Zimbabwe, and his banning of outlets like the BBC from reporting there."
Malema announced that he would heed the ANC's call for restraint and stop singing the apartheid era song that has the words "Shoot the Boer", an incitement seen by some people as causing the recent murder of the white supremacist Eugene Terre'Blanche.

Malema == Mtikila, mtaji wao wa siasa umejengwa kwa misingi ya kuwagawa watu kwa kupandikiza na/au kulea chuki. Ni watu hatari sana. Nawashangaa wengi wenu mnaowatetea na kuwaona ni wakombozi huku mkijifanya hamjui madhambi yao ya "ufisadi" na "udhalimu" mwingine.

Kwa kweli stroy hii inatupa changamoto kubwa watanzania. Mhe. Zitto mwanzoni alianza kujipambanua ktk muelekeo huu, sina uhakika kama kwa sasa ikoje. Ila Malema is a lesson to all of us!

Kwani ni sifa kuwa kama Malema?

Back
Top Bottom