Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Kiongozi wa EFF Julius Malema ameitaka serikali kuharamisha ukahaba. Akizungumza na wafuasi wa chama katika maandamano ya Siku ya Wanawake huko Mpumalanga, Malema alisema wafanyabiashara ya ngono wanastahili kupata ulinzi na vyombo vya sheria, ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kufungua kesi dhidi ya wabakaji au aina nyingine za unyanyasaji bila kudharauliwa na polisi.
"Serikali lazima ihalalishe ukahaba. Ukahaba ni taaluma kongwe zaidi duniani. Unaweza kuwa Mkristo ama dini nyingine; upende usipende, ukahaba ni kazi na kuna watu wanaofanya kazi humo. Jamii inajengwa na makahaba ndani yake na lazma tukubali kuwaunga mkono."
"Waheshimuni watu hawa na familia zao, wao pia lazima wawe na ulinzi na haki kama wafanyakazi wengine, mwili wake ni haki yake na anapaswa kulindwa dhidi ya unyanyasaji, anaweza kuwa na mume na watoto, kazi yake ndio inampatia kipato na maisha" alisema.
Kumekuwa na mjadala unaoendelea kuhusu kuhalalisha ukahaba ili kuimarisha afya na usalama kwa wafanyabiashara ya ngono na kulinda haki zao. Mnamo 2022, baraza la mawaziri liliidhinisha kuchapishwa Mswada wa Marekebisho wa Sheria ya Jinai (Makosa ya Kujamiiana na Mambo Yanayohusiana) kuhusu kuharamisha kazi ya ngono kwa maoni ya umma.
Malema alisema wanawake wote wanapaswa kulindwa dhidi ya kuwa wahanga wa unyanyasaji. Hivyo biashara hii iwe sehemu ya watu kujipatia kipato.
JE HOME BOY AMEZINGUA AU YUPO SAHIHI KATIKA HILI SUALA?