Mcharo son
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 6,164
- 5,117
Kujirudia inatokana na mhusika na mwenendo wake, baada ya kuombewa na mapepo kutimuliwa. Ukishaombewa na mapepokutimuliwa, unapata ulinzi wa Mungu. Hakuna pepo litakalorudi labda uvunje masharti ya huo ulinzi wa Mungu, kwa kifupi endapo utajiweka katika maisha ya kutenda zambi Mungu anajitenga na wewe, hapo nguvu zake za ulinzi zinajitenga na wewe unabaki mtupu. Hapo Mapepo yanarudi tena yanaarika na yenzao. Yote haya yapo katika bible sitoi kichwani (ingawa nukuu za mistari sikumbuki).Akili za mgalatia bhana !
Mie sijawahi kukutana na shetani.
Sasa nikuulize: yale mapepo yanayokemewa Kanisani kwanini yanajirudia kwa mtu kila mara ? na mengine yanagoma kutoka !
Kuhusu kugoma kutoka pia ni kutokana na msimamo wa muhusika. Kabla ya kuombewa muhusika upewa KWELI YA MUNGU NA ANAPEWA NAFASI YA KUMKILI YESU KUWA NI BWANA NA MWOKOZI NA KUWA TAYALI KUISHIA MAISHA KAMA YESU ALIVYOAGIZA (hapo ndipo penye chanzo cha kupata ulinzi wa kimungu dhidi ya shetani na mapepo yake). Sasa muhusika ana hiyari ya kukubali ili apate ulinzi wa Mungu au akatae. Endapo atakataa au hata akikubali juu juu BASI YESU HATOWEZA KUINGIA KATIKA MAISHA YAKE na KUMTETEA. HAPO atakuwa amekubali kuendelea kukaa upande wa shetani na MAPEPO yatagoma kutoka (kwa sababu hakuna nguvu ya Mungu kuyatimua) kwa kuwa muhusika kakubali kuegemea upande wao(Tena yanasema huyu ni mtu wetu katukubali). Yesu huwaponya na kuwatetea wale tu wanaomkili na kumkubari. Bila ulinzi na connection ya nguvu zake hutaweza kutoa pepo na wala mapepo hayatatoka. Tena ukitaja jina lake yanaweza kukuadhibu mana unayapa tumbo joto wakati wewe ni mtu wao.
Kama mtu haujamkili Yesu kuwa ndio bwana na mwokozi wa maisha yako, Yeye hatakulazimisha na huwezi kupata access ya kutumia nguvu za kimungu. Ndio mana sio wakristo wote wanaoenda kanisani wana uwezo wa kutoa pepo kwa kutumia jina la YESU. Ila ukweli unabaki palepale kuwa mapepo wanamjua yesu ni nani na wanaliogopa hilo jina kuliko kitu chochote hapa duniani, chunguza! Kama huna nguvu za Yesu, ukatumia ilo jina kutoa mapepo, yanaweza kukudhuru tu, kwa sababu ya kuyatisha wakati wewe ni mtu wao. Lakini ukiwa umemkili Yesu na kuokoka basi jina YESU kwako ni upanga wa moto kwa shetani, mapepo na uchawi wa aina yoyote. Nenda makanisa ya wokovu utapata huduma ya kumkili Yesu na kufanikiwa kujikinga na silaha hii.