Jukwaa la Wahariri Tanzania chombo kisichokuwa na uwakilishi sawa kwa wanahabari

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Ni ajabu chombo hiki kujiita Jukwaa la Wahariri Tanzania, ilifaa kijiite Jukwaa la Wahariri wachache na wa Print Media Tanzania.

Kwa miaka kadhaa sasa tangu chombo hiki kianzishwe huku kikijinasibu kuwa kinawakilisha maoni na maslahi ya wahariri Tanzania kumekuwepo kasumba ya kupata uanachama kwenye chombo hicho huku uwakilishi ukiwa ni wa Wahariri wachache tena wa Dar es salaam pekee kana kwamba Wahariri wapo Dar es salaam Pekee.

Ukienda mikoa mingine ya Tanzania kunavyo vyombo vingi vya Habari huko huku redio zikitawala lakini ni nadra kuona uwakilishi wa wahariri wa Elektroniki Media kwenye chombo hicho hasa kutoka mikoani....Tatizo la chama hiki ni sawa na tatizo ambalo lipo kwenye vilabu vya uandishi wa habari huko mikoani ambavyo navyo pia vimekuwa na kasumba ya kuwabagua baadhi ya wanahabari kwa misingi ya kisiasa au sababu nyinginezo hasa za mshiko kwa madai kwamba mkiwa wengi mshiko unapungua kwa hiyo kukitokea mualiko wa press wanaitwa hao wachache walio na uanachama kwenye klabu huku waandishi wengine wakikosa uwakilishi.

Linalojiita Jukwaa la Wahariri Tanzania nashauri libomolewe au lichunguzwe na kuangalia uwakilishi wake kwa wahariri wa vyombo vyote vya habari Tanzania na namna kinavyoendesha shughuli zake.

Aidha ni wakati mujarabu sasa kwa Wizara husika kuunda ile Bodi ya kuwahakiki wana habari na hili Jukwaa la Wahariri litambulike kisheria na namna ya kujiunga wanachama iwe wazi ni nani anakidhi vigezo...maana hali ilivyo sasa kimekuwa chombo/NGO ambayo waandishi wakongwe wachache wanapiga hela tu humo huku waandishi/editors wengi wakikosa uwakilishi humo. Balile na wenzio kina Meena mjitathmini kama kweli hilo jukwaa linawawakilisha Wahariri wote Tanzania kwa kuzingatia mikoa nk...na uchaguzi mnafanyaje nk nk
 
Back
Top Bottom