Jukwaa la Wahariri mmetumwa?

Don Mangi

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,198
852
Wana JF,
Hawa jukwaa la wahariri wana maana gani wanapotoa waraka na kusema wanatambua ufinyu wa rasilimali za nchi wakati ongezeko la posho kwa wabunge zimesainiwa? Mbona hawakutoa waraka kupinga na posho kwa kusema wanatambua pia rasilimali ni finyu. Naomba mnapotoa nyaraka msikurupuke hovyo. Mnaudhi watu wanaotambua uhalisia wa siasa ya hii nchi.
Nawasilisha.
 
..Nadhani inawezekana hawakutumwa; isipokuwa wakati wa kutoa tamko lenyewe si muafaka! Wakati Jukwaa la Wahariri wanatoa tamko lenye hoja ya kuonyesha kwamba nchi ina rasilimali chache kulikuwa na haja ya kuangalia mambo haya:
  1. Kwa nini baadhi wa watumishi wa umma wanalipwa posho nono na kubwa kuliko kada nyingine?
  2. Kwa nini madaktari wagome ilhali wanalipwa vema na posho zao ni kubwa kuliko kada nyingine?
  3. Wabunge sawa; madaktari hapana na walimu pia hapana!
Kuna kila sababu ya kuangalia ukomo wa matumizi ya rasilimali kwa kuangalia uwiano wa mgao wake kwa kada zote zinazohitaji malipo ya halali na yanayokidhi mahitaji yao kiuchumi, kijamii na kisiasa! Tuangalie rasilimali kwa mtazamo wa mgawanyo wa uhuru, haki na usawa. Isiwezekane kwa kada moja kupewa nafasi ya kutumia zaidi ilhali kada nyingine wakiambia wajifunge mkanda (mkwiji) kukubali maumivu ya maisha.
 
Nchi ina wambea hii.. kwl no research no right to speak..mara kasaini mara hajasaini..na matamko juu.

bado barkwatah tu
 
hapo jamaa wamefuka sana tu, sikubali

Wamefuka vibaya mno, sijawaelewa hata kidogo, mi nna wasiwasi kuna kitu nyuma ya huo waraka wao, hawawezi kujifanya ndio wana uchungu kumbe wanafki wakubwa, wameniudhi sana, hiyo dhambi wakaitubu.
 
..Nadhani inawezekana hawakutumwa; isipokuwa wakati wa kutoa tamko lenyewe si muafaka! Wakati Jukwaa la Wahariri wanatoa tamko lenye hoja ya kuonyesha kwamba nchi ina rasilimali chache kulikuwa na haja ya kuangalia mambo haya:
  1. Kwa nini baadhi wa watumishi wa umma wanalipwa posho nono na kubwa kuliko kada nyingine?
  2. Kwa nini madaktari wagome ilhali wanalipwa vema na posho zao ni kubwa kuliko kada nyingine?
  3. Wabunge sawa; madaktari hapana na walimu pia hapana!
Kuna kila sababu ya kuangalia ukomo wa matumizi ya rasilimali kwa kuangalia uwiano wa mgao wake kwa kada zote zinazohitaji malipo ya halali na yanayokidhi mahitaji yao kiuchumi, kijamii na kisiasa! Tuangalie rasilimali kwa mtazamo wa mgawanyo wa uhuru, haki na usawa. Isiwezekane kwa kada moja kupewa nafasi ya kutumia zaidi ilhali kada nyingine wakiambia wajifunge mkanda (mkwiji) kukubali maumivu ya maisha.

Labda kweli wakati wa hicho ki tamko chao ulikua haujafika, lakini bado nashawishika kuhisi kama wametumwa hivi!
 
Hakuna aliyemweli kweny hii nchi kila mtu anabweka tu kama mbwa akishatupiwa nyama kama mbwa ananyamaza wizi mtupu kwanza hawa watu wanashekula nyama ya mtu hivyo hawezi kuacha kuongwa...
 
Back
Top Bottom