Jukwaa la wahariri fanyeni hivi kuweka uwiano

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,121
Mkuu wa mkoa, alituhumiwa kuvamia studio za clouds akiwa na wanausalama nimetumia lugha tuhumiwa kwa sababu sina mamlaka ya kuhukumu pamoja na kwamba kuna cctv footage zilizosambaa,

Jukwaa la wahariri kupitia mwenyekiti wake walikubaliana kutokuandika habari zozote zinazomuhusu RC ikiwa kama adhabu.

Wiki iliyopita tuliona jinsi wanachama wa CUF academia walivyovamia mkutano wa CUF original wakiwa wamejihami na silaha za jadi na za moto (kwa mujibu wa mashuhuda)ambapo waandishi wengi walijeruhiwa na wengine kuonyeshewa silahanza moto, kilichonifurahisha zaidi ni mwenyekiti wa CUF academia kukiri kuwa wale waliokuwa ni walinzi wake.

Ili kuweka uwiano na kuaminisha umma kuwa adhabu aliyopewa RC haikuwa ya uonevu ambapo hapa hakupigwa wala kujeruhiwa yeyote binafsi nitashangaa sana na kuingiwa na mashaka na utendaji kazi wa TEF Kama hamtatoa adhabu kwa tukio hili ambalo nina amini limekuwa na madhara kuliko lile la shilawadu na ushahidi wake upo dhahiri ikiwa ni pamoja na ukiri wa mwenyekiti wa CUF academia nawasilisha.
 
Kumbe liprofeseli alikiri kuwa jamaa ni walinzi wake??.
Polisi wapo kimya
Mwigulu yupo kimya
Mwakye ndio kalala kabisa
 
Back
Top Bottom