Jukwaa la Katiba kutangaza Maombolezo ya siku 9!

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Jukwaa la Katiba kutangaza Maombolezo ya siku 9

Katika kuonyesha msimamo wao wa kutokubaliana na maridhiano tete kati ya CDM na JK, Jukwaa la katiba lipo katika mchakato utaofanikisha kutolewa kwa tamko rasmi muda wowote kuanzia sasa kuhusu maombolezo ya siku 9 kwa msiba mkubwa wa Katiba.

Tafsiri sahihi ya maombolezo haya ni kuonyesha kwa namna ambavyo mbio za katiba mpya zilivyofikia ukingoni kwa masilahi ya dola na si nini wanachotakiwa kufanyiwa watanzania.

Bado sintofahamu na wingu kuhusu makubaliano ya CDM na JK yanazua maswali mengi kwa makundi shiriki katika kudai uwazi juu ya mchakato wa Katiba Mpya.

Kama muafaka utapatikana maombolezo haya yatadumu kwa siku 9 kuanzia desemba mosi hadi siku ya kumbukumbu ya uhuru.

Technically: Makubaliano ya kuuboresha mswaada yaliyofikiwa na CDM na JK yatatoa nafasi kwa nyongeza hiyo kufanyia marekebisho sheria ya kuundwa katiba mpya na si mswaada kwa maana kwamba marekebisho ya sheria kwa mujibu wa taratibu za Bunge hufanyika baada ya Kipindi cha miezi 6 na si vinginevyo.

Utagundua ndani ya muda huu JK na CCM watakuwa wamefanya mengi ya kutosha katika kupata katiba mpya ikiwa ni pamoja na kuunda tume, kukusanya maoni kwa tume isiyo na meno na hatimaye baada ya miezi sita marekebisho ya sheria yanafanyiaka bungeni huku mchezo ni kama umekwisha hivi.

My Take: sijui hii move ya CDM tuiite bao la kujifunga au bao la offside, Tusubiri tusikie ya Jukwaa la Katiba leo.

ADIOS
 
Wananchi wa Tanzania hatuna sauti kabisa,hivi tume iliyoundwa kukusanya maoni ilifanya kazi wapi na kwa wananchi wa nchi gani?binafsi ni kama nasubiria tume ije huku kwetu,cha kushangaza nasikia mswada umepitishwa,mara rais kasign!hivi hii nchi ni ya nani,kwanini hawa watu wanafanya wanachofikiria wao?ingetakiwa yatangazwe maandamano na si maombolezo
 
Katika kupigania haki hutumii silaha moja kama ilivyo kwa vita yoyote duniani. Mimi nafikiri hii ni njia mojawapo ya kufikisha ujumbe hata hivyo si vema kubeza yale yaliyofanywa na CHADEMA hasa ukizingatia hali tete ilivyokuwa.
Nawapongeza jukwaa la katiba kwa kufikiria mkakati huu.
 
Kulia na kucheka zote ni kelele. hivi MAOMBOLEZO NI NAMNA YA MAANDAMANO

Something similar hasa ikihusisha watu kukaa mahali huku wakiomboleza. Wanawake wa kenya waliwahi kuifanya pale uhuru park na ilileta impact. Polisi walipowafuata walivua nguo na kubaki uchi. Sijui hii ya kwetu itakuwaje?
 
Jukwaa la Katiba kutangaza Maombolezo ya siku 9

Katika kuonyesha msimamo wao wa kutokubaliana na maridhiano tete kati ya CDM na JK, Jukwaa la katiba lipo katika mchakato utaofanikisha kutolewa kwa tamko rasmi muda wowote kuanzia sasa kuhusu maombolezo ya siku 9 kwa msiba mkubwa wa Katiba.

Tafsiri sahihi ya maombolezo haya ni kuonyesha kwa namna ambavyo mbio za katiba mpya zilivyofikia ukingoni kwa masilahi ya dola na si nini wanachotakiwa kufanyiwa watanzania.

Bado sintofahamu na wingu kuhusu makubaliano ya CDM na JK yanazua maswali mengi kwa makundi shiriki katika kudai uwazi juu ya mchakato wa Katiba Mpya.

Kama muafaka utapatikana maombolezo haya yatadumu kwa siku 9 kuanzia desemba mosi hadi siku ya kumbukumbu ya uhuru.

Technically: Makubaliano ya kuuboresha mswaada yaliyofikiwa na CDM na JK yatatoa nafasi kwa nyongeza hiyo kufanyia marekebisho sheria ya kuundwa katiba mpya na si mswaada kwa maana kwamba marekebisho ya sheria kwa mujibu wa taratibu za Bunge hufanyika baada ya Kipindi cha miezi 6 na si vinginevyo.

Utagundua ndani ya muda huu JK na CCM watakuwa wamefanya mengi ya kutosha katika kupata katiba mpya ikiwa ni pamoja na kuunda tume, kukusanya maoni kwa tume isiyo na meno na hatimaye baada ya miezi sita marekebisho ya sheria yanafanyiaka bungeni huku mchezo ni kama umekwisha hivi.

My Take: sijui hii move ya CDM tuiite bao la kujifunga au bao la offside, Tusubiri tusikie ya Jukwaa la Katiba leo.

ADIOS

Maombolezo bila kibali nayo ni uvunjaji wa sheria zinazopaswa kusimamiwa na geshi la polisi la nji hii! Ikiwa mliacha kuandamana kwa kuogopa virungu na mabomu ya machozi; basi hata mkiomboleza tutakuja kuwanyuka na hivyo vitu huko huko msibani! By the way, issue haikuwa kuandamana, issue ni tishio kutoka kwa Alshabab, na kv tishio hilo halijaondoka, basi tutakuja piga mabomu huko kwenye makutano ya maombolezo yenu......amini amini nawaambia, ni kheri tuwatwangwe virungu wale wasio na mbio pamoja na mabomu ya machozi kuliko mje kutwanga na risasi pamoja na maguruneti toka kwa Alshabab....!! By the way, Alshabab wataua halaiki, sisi tutaua kama wawili watatu tu ili tusichafue sana rekodi yetu....Zimwi likujualo, halikuli likakwisha!
OVER!
 
Dah! hivi yupo mtu anaweza kuja na solution hapa! yani sisi kama wenye nchi tumepuuzwa waziwazi sasa tufanye nini? mambo ya cdm na Jukwaa la katiba tuwaache waendelee na bidii zao sisi kama raia tufanye nini sasa?
 
Maombolezo bila kibali nayo ni uvunjaji wa sheria zinazopaswa kusimamiwa na geshi la polisi la nji hii! Ikiwa mliacha kuandamana kwa kuogopa virungu na mabomu ya machozi; basi hata mkiomboleza tutakuja kuwanyuka na hivyo vitu huko huko msibani! By the way, issue haikuwa kuandamana, issue ni tishio kutoka kwa Alshabab, na kv tishio hilo halijiondoka, basi tutakuja piga mabomu huko kwenye makutano ya maombolezo yenu......amini amini nawaambia, ni kheri tuwatwangwe virungu wale wasio na mbio pamoja na mabomu ya machozi kuliko mje kutwanga na risasi pamoja na maguruneti toka kwa Alshabab....!! By the way, Alshabab wataua halaiki, sisi tutaua kama wawili watatu tu ili tusichafue sana rekodi yetu....Zimwi likujualo,
halikuli likakwisha!

Dah! ha! ha! ha!
Hii kweli nchi ya mazuzu na hivi ndo tuavyopelekwa! LOL!
 
Dah! hivi yupo mtu anaweza kuja na solution hapa! yani sisi kama wenye nchi tumepuuzwa waziwazi sasa tufanye nini? mambo ya cdm na Jukwaa la katiba tuwaache waendelee na bidii zao sisi kama raia tufanye nini sasa?
sisi kama raia hatuna namna zaidi ya kuingia barabarani kwasababu najua tukiomba tukutane na JK (Jua Kali) hatakubali
 
Jukwaa la Katiba msituletee huko!
Hizo pesa za wafadhili zitawatokeeni puani.Mkiomboleza halafu ndio iweje?
Mlikuja motoooooo sasa mmejikwaa juu ya jukwaa??
 
miafrika ndivyo ilivyo mtapost mpaka keyboard zitoboke hakuna maandamano wala mabadiliko hapa tz..
chamsingi ni kumuomba mungu awafumbue na kuwazidishia watu mioyo ya kuchukulia kila kitu poa kama ilivyo sasa.
RIP Tanzania..
 
GR ulipotea sana mkuu wangu.......hao jukwaa la katiba sitaki hata kuwasikia!!!!

Back Home Mkuu...Tupo pamoja Tena.

Kinachoninyima usingizi ni hizi rasilimali wanazotumia kuamsha vuguvugu la Katiba na Midahalo ya TV waliyoendesha nchi nzima. Inasadikiwa wanalipia karibu milioni 20 kwa airtime ya kipindi kimoja.

Ntafuta details zaidi. Hapa si bure
 
nyambafu kabisa hili jukwaa la katiba. siwaamini tena toka siku ile waimbe nyimbo na jeshi la polisi
 
Maombolezo kwa mtindo gani, watu watavaa nguo nyuesi au nyupe, kama wakikaa eneo moja kama inavyokuwa kwenye misba bila kufanya kazi huo ni mgomo.
 
Yatupasa kulichukulia suala hili kitaifa zaidi! tuweke mambo ya parts pembeni! Zingatieni JK amelazimika kusign mswaada kwa sababu eti asiposign chama chake hakitamwelewa! Hili ni tatizo kubwa sana! Kumbe nchi hii ni ya ccm?? wale wasio na chama kumbe si raia wa nchi hii sasa twende wapi tufanye nini Ebu tufikiri hapa kwa uchache wetu na tutoke humu na kitu cha kufanya pls tuache utani katika suala hili nakuombeni sana sana.
 
Dah! hivi yupo mtu anaweza kuja na solution hapa! yani sisi kama wenye nchi tumepuuzwa waziwazi sasa tufanye nini? mambo ya cdm na Jukwaa la katiba tuwaache waendelee na bidii zao sisi kama raia tufanye nini sasa?

Nimesikia siku moja katika TV kuna Mtu yupo Mza anawadhifa wa mwenyekiti wa wapiga kura kanda ya Ziwa, sijui alipatikanaje ila kama ni kwa njia za kidemokrasia kuna haja ya kuwa na mwenyekiti wa watanzania kila wilaya sasa ili aweze kutoa sauti za wananchi hasa kwa dhati na wala si huu usanii wa baadhi ya makundi kuficha agenda zao nyuma ya mgongo wa kuwa kwa maoni ya wananchi wengi (wangapi haswa?) mbona kama tunaburuzwa hivi?

Time for change

ADIOS
 
Back
Top Bottom