Jukumu la Ulinzi wa Raia na mali zao

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
247
Yaliyotokea mkoani Mara yanatishia sana amani ya nchi yetu.
Hofu sasa imeanza kutanda, amani hamna tena,
ukiwa na mali japo kidogo tu, maadui wengi wanaibuka kila kona.
jeshi letu la kutulinda limelala doro, ukipiga simu namba ya dharura inapokelewa na answering machine.
Ukipiga simu ukiwa Namanyere Sumbawanga, inapokelewa Dar es Salaam.
Hivi jamani kweli nitapata msaada wa haraka kweli wakati mtu aliyepokea simu yangu ya dharura yuko huko mbali?
Naomba hizi namba za dharura zielekezwe kwenye kituo cha polisi wilaya ili tukiwa na shida tupate huduma kwa haraka.
Vinginevyo serikali ilivunje jeshi la polisi na itamke bayana kuwa ulinzi wa raia na mali zao ni jukumu la raia wenyewe.
 
Umesha amka?
Jana ulisema unatafuta mganga wa ukweli, nadhani atasaidia sana kwenye ulinzi wa mali zako.
Kusema ukweli Jeshi letu lina kabiliwa na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na mfumo wa kiutendaji.
Liko nyuma ki teknolojia na kiufanisi,
askari wetu wengi ni wale ambao hawakufanya vizuri mitihani yao ya sekondari, kwa hiyo hata ufahamu wao ni mdogo.
Kwa kweli matatizo yao tukiyaorodhesha hapa ni mengi mno, lakini pia mazingira wanayofanyia kazi ni magumu sana.
hamna vitendea kazi wala nini.
 
Kwa kweli jukumu la ulinzi Tz ni wewe mwenyewe. Ukishakuwa na uwezo ni muhimu kujihazari kama vile kuajiri mlinzi na kuweka silaha nyumbani za kujilinda. Usitegemee Jeshi la polisi njaa.
¬K
 
Back
Top Bottom