Juisi ya chungwa na asali

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Mahitaji
Juice ya chungwa (Unaweza kukamua au ukatumia ya box)
Asali ya nyuki
Chombo cha kuchemshia ( sufuria, glass au bilauri)
Microwave au jiko la kawaida

Maelekezo
Unaweza kuandaa juisi hii kwa kuchanganya asali na juisi na kisha kuipasha moto.
Kama unatumia microwave changanya juisi na asali na kisha weka kwenye microwave kwa muda wa dakika 1 hadi 2 ili ipate kuchanganyika vizuri.
Kama huna microwave, changanya asali na juisi kisha weka kwenye sufuria na bandika jikoni kwa muda wa dakika 5 hadi 7. Acha ichemke vizuri ili asali na juisi zichanganyike vizuri. Unaweza kukoroga pia ili kusaidia mchanganyiko uwe sawia.
Asali ikiwa kwenye microwave inapata kulainika, hivyo huchanganyika vizuri na juisi na kuipa utamu wa kipekee. Kwa maana hiyo unaweza pia kutumia asali yenye mabonge maana italainika vizuri, kwani microwave pia hutumika kulainisha asali.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom