Asante WoS, apart from our resident Philadelphia lawyer (the great Kuhani) who has been AWOL for a while, you are the first one that came to my mind that you'd at least give this topic a crack.
Nadhani falsafa kuu ya mahakama zote ni kutenda haki kwa kufuata sheria zilizoko kwenye katiba na kwenye vitabi vingine vya sheria. Na kwa ufahamu wangu mimi mahakama nyingi bila kujali ni za wapi hufuata precedents.
Kwa hiyo, nilichokuwa nataka kusema ni hiki: Ingawa katika kusoma soma kwangu mambo ya sheria sijaona definition inayokubalika kuhusu nini maana ya 'judicial philosophy', nilichokuwa nataka kuuliza ni jinsi gani majaji wetu wanatafsiri sheria kulingana na views/ beliefs zao pamoja na imani au maono yao ya kiitikadi (ideological convictions).
Nikupe mfano kuhusu Supreme court ya Marekani ambayo ina jopo la majaji 9. Watano kati ya hao ni judicial conservatives na wanne waliobaki aidha ni ma liberal au wana mrengo wa kati kidogo. Na mara nyingi kwenye maamuzi yenye utata ndio utaona wanasimama wapi kwenye ideological spectrum maana maamuzi huwaga ni 5-4 in favor of the ones with the conservative leanings.
Nina hakika kabisa kwa mfano suala la abortion likipelekwa tena mezani, Justices Antonin Scalia na Clarence Thomas watapiga kura kui-overturn Roe v. Wade kwa sababu wao ni conservatives who believe in the sanctity of human life.
Sijui kama kama nimeeleweka lakini hicho ndicho nilichokuwa nauliza....kwamba ideologically majaji wetu wanasukumwa na convictions gani katika kutoa maamuzi.