Jua yachomoza mashariki—upendeleo kwa China duniani waendelea kuongezeka

Jua yachomoza mashariki—upendeleo kwa China duniani waendelea kuongezeka

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
169
Reaction score
287
1689ccfe50f91f69bafcab76c19baab9.jpeg
Maneno kama “Mshiriki mwenye ushawishi mkubwa zaidi katika masuala ya kimataifa”, “Mshirika wa kuaminika”, “China inazidi kuvutia”. Yanasikika zaidi katika zama hizi. Hivi karibuni, hojaji zilizofanywa na mashirika mbalimbali ya kimataifa ya uchunguzi wa maoni zimeonyesha kuwa taswira ya China inaendelea kuimarika, huku mvuto wa China kwa watu duniani ukiongezeka kwa kasi.

Kura za maoni zilizofanywa hivi karibuni na Shirika la Pew zinaonesha kuwa mvuto wa China duniani unaendelea kuongezeka, huku idadi ya waliohojiwa wakiwa na mtazamo chanya kuhusu China ikiongezeka kwa asilimia 5 ikilinganishwa na mwaka jana.

Hojaji iliyofanywa na Shirika la Morning Consult kwa takriban watu wazima 4,900 katika nchi 41 ilionesha kuwa, kiwango cha mvuto wa China kimataifa kilikuwa 8.8, huku kile cha Marekani kilikuwa 1.5 chini ya sifuri.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2025 ya “Viashiria vya Nguvu Laini duniani” iliyotolewa na Shirikisho la Biashara ya Chapa la Uingereza, China imekuwa na ukuaji mkubwa katika viashirio kadhaa vya nguvu laini. Ripoti hiyo inaona kuwa hali hiyo inatokana na China kuendelea kusukuma mbele pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kuhimiza maendeleo endelevu duniani, na ushawishi wa chapa za kibiashara za China kuongezeka.

Katika zama hii yenye habari nyingi kupita kiasi, maoni ya umma yanayodhibitiwa na nchi za Magharibi kwa muda mrefu yameunda “Ukuta wa Habari” dhidi ya nchi zinazoendelea ikiwemo China. Lakini ukweli daima huushinda uwongo. Kutokana na teknolojia mpya za usambazaji wa habari, watu wengi zaidi duniani wameweza kuona hali halisi za China.

Mvuto wa China umeongezeka zaidi katika nchi za Dunia ya Kusini. Kutoka Afrika hadi Latin-America, kutoka Mashariki ya Kati hadi Asia ya kusini mashariki, China inatazamwa kama “mshirika wa kutegemeka”. Utambuzi huo unatokana na kwamba China inashikilia kithabiti kanuni za kuheshimiana, haki na usawa, na kuhimiza mafanikio ya pamoja. Kama Profesa Mulaku Lemmy Nyongesa, ambaye ni msomi wa masuala ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, alivyosema, ushirikiano wa China na nchi za nje unazingatia kikamilifu hali halisi na mikakati ya maendeleo ya nchi nyingine, na China na nchi nyingine za Kusini pia zina mguso sawa wa kihisia kutokana na historia.

“Jua inachomoza mashariki”— ripoti ya mwaka 2025 ya “Viashiria vya Nguvu Laini duniani” iliyotolewa na Shirikisho la Biashara ya Chapa la Uingereza imefupisha vizuri matarajio chanya ya watu duniani kwa China. Katika siku za mbele, China itaendelea kuwa mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya kimataifa, na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa, na mkuzaji wa mawasiliano ya staarabu za binadamu
 
Umeandka pumba tu sa hayo yanatusaidia nn sisi watanganyka CHINA ni wanyonyaji na majangili tu wa africa kama walivyo nchi za magharibi mamaeee walahi.
 
Back
Top Bottom