Jua vipodozi vyote visivyo salama, jua jinsi ya kuitunza ngozi yako vizuri na kuwa unavyopenda

said rashid

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
203
112
Watu wengi (wanawake na wanaume) wamekuwa wakitumia vipodozi visivyo salama na vile visivyoendana na ngozi zao na hata mahitaji yao. Wengi niliofanikiwa kuongea nao na kuwahudumia wameniambia walikuwa hawajui kabisa, lakini kuanzia sasa wataacha kabisa.

Madhara ya vipodozi visivyo salama ni pamoja na kuharibu ngozi, ini, figo, macho na ubongo; hatari ya kupata kansa; kuunguza ngozi; ngozi kuwa na rangi mbaya; ngozi kuzeeka haraka; macho kupofuka; ngozi kuwasha; vipele; chunusi; majipu; na kadhalika
Miongoni mwa mada zitakazojadiliwa katika semina ya AFYA ZAIDI Consultants siku ya tarehe 14/1/2016 ni VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA MADHARA YAKE. Pia watu wote watafundishwa vipodozi vinavyoendana na ngozi zao na vitakavyofaa kwa mahitaji yao.

Ili kuweza kujua na kupata matokeo mazuri ya vipodozi vyako basi ni vyema kujiandikisha sasa kupitia namba za simu 0659528724 au 0784082847 na kuhudhuria semina hii. Semina hii itafanyika MAGOMENI MAPIPA katika ukumbi wa RECREATION HALL uliopo jirani na STATE COLLEGE OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES na NEW BONDENI HOTEL
KITABU IMAGE.jpg
Vipodozi visivyo salama 5.jpg
Vipodozi visivyo salama 4.jpg
vipodozi visivyo salama 3.jpg
vipodozi visisvyo salama 2.jpg
Vipodozi vilivyopigwa marufuku 1.jpg


Kiingilio cha semina hii ni Sh. 3,000/= tu. Lengo ni kufanya watu wengi zaidi waweze kushiriki na kupata elimu na ushauri wa afya, urembo na vipodozi.
Pia vitabu vya SURA NZURI.... NGOZI NYORORO..... Vitapatikana kwa bei ya punguzo la 30% ; yaani kitatolewa kwa bei ya Sh. 2,000/= tu. Kitabu hiki ni muongozo wa jinsi ya kuitunza ngozi yako na jinsi ya kukabiliana na baadhi ya matatizo ya ngozi yako. Pia kinaelezea vipodozi visivyo salama na madhara yake kwa undani kabisa. PATA NAKALA YAKO SASA!

Jitahidi uje na wenzako. Au kama huwezi kufika basi mwambie mwenzako aje ili kujikinga dhidi ya matatizo makubwa ya vipodozi vibaya.
 
Back
Top Bottom