Jua jinsi tunavyoibiwa madini yetu

ruby garnet

JF-Expert Member
Apr 10, 2017
2,869
3,851
Wana JF,

Kuna malalamiko mengi sana juu ya mikataba ya madini na hasa huhusishwa viongozi kuwa wanahusika kutuibia madini yetu wakishirikiana na makampuni ya mabwenyenye. Tuhuma hizi zimeanza toka mzee wa privatization (ubinafisishaji ufanyike) atowe go ahead ya sekta binafisi kuchukua mali za umma na kuanza kuziendesha. Mzee wetu Mkapa alituacha na sheria ya madini 1998 ambayo mikononi mwa Mzee Kikwete ilifanyia mabadiliko tukapata ya 2010 (MINING ACT 2010).

Mimi nitajikita kuchambua namna makampuni ya madini yanavyotozwa tozo mbalimbali. Kabula ya kuchambua hayo naomba nidokeze njisi ya kupata leseni ya madini kulingana na sheria yetu kunaaina mbili ya leseni za madini(mineral right). ambayo ni leseni ndongo na kubwa

1. Leseni ndogo(primary mining lisence) hii ni kwa ajiri ya watanzania tu(wazawa tu) na inaombwa kwenye ofisi za kanda za madini.

2. Leseni kubwa hizi zimegawanyika makundi mawili. Leseni za kutafiti na Leseni ya kuchimbia( prospecting licence and mining licence). Hizi leseni ni kwa ajili ya watu wote wenye uwezo wa kutafiti na kuchimba kitaamu.(Watanzania na wasio watanzania) na makampuni yote makubwa mnayosikia yanachimba na kutafiti yana Leseni kutoka kundi hili.

Ikumbukwe kuwa Leseni ya aina yeyote inapatikana baada ya mhitaji kutafuta eneo yalipo au anapohisia kuwa kunamadini na lisiwe lina Leseni ya madini ya mtu au kampuni na kisha kwenda kuomba Leseni katika ofisi za madini zilizochini ya wizara ya nishati na madini na katika kuomba hakuna mkataba unaoingiwa isipokuwa ni kufata sheria iliyopo.

Kutokana hayo sasa nijikite kufafanua njisi tozo zinzvyofanywa katika Leseni aina ya 2 (Leseni kumbwa kwani ndiyo zenye utata sana hapa TZ). Pia huwa kunagharama za maombi ya Leseni hizi pamoja na malipo ya kila mwaka kumiliki Leseni hizi huwa zinatozwa.

Ili uanze kuchimba kwenye leseni kubwa Mining Lisence and special mining Lisence kuna mkataba wa uendelezaji mgodi unaoitwa (Mining Development Agreement kwa kifupi MDA). Huu mkataba ndiyo ulikuwa unapigiwa kelele pia CAG kuwa ulivyowekwa hauwezi kubadilishwa yaani huwa stable katika hili ni inchi nyingi duniani huwa hivyo kama Austrial, Canada, Chile, Mexico na hii ipo hivyo kuepusha au kupunguza political risk katika secta hii ukizingatia kuwa ndiyo secta yenye risk kubwa kupata au kukosa ni kawaida etc.

Sasa hebu tuone tozo zinavyofanyiaka katika migodi mikubwa kama ACACIA, GGM etc.

1. Mrahaba(royalties) ni asilimia 4% ya madini kwa bei ya sokoni hii inamaana kwa mfano kama dhahabu(gold) kwa mwaka wamechimba 500kg na bei ya sokoni ni $40000 hapa pesa tunayopata ni $40000 x0.04=$1600 na katika nchi nyingi mirahaba ipo kati ya 3% hadi 6% na mrahaba huwa hauna mjadala wa kuwa umepata faida au hamuna na Tanzania ndiyo tunazoambilia ila sina uhakika kama mahesabu ya wingi wa madini huwa tunapewa sahihi kulingana na waliyochimba au na hapa tunadanganywa na sina uhakika kama tunafatilia kwa makini kusibitisha kiasi cha madii haya.

2. Corporate tax(ushuru wa kampuni). hii huwa tunachukua asilimia 30% ya faida
Hapa ndiyo madudu yamejaa sasa kutokana baba wataifa kutaifisha migodi yote(nationalizaion private sector) 1967. Mabwenyenye wote walikimbia na ukweli wengine walikata mitaji yao na hii siyo wageni tu na kunawazawa wengi waliasilika na hili swala. Hivyo wote waliondoka na kuacha migodi na ilimilikiwa na serikali lakini jambo la kusikitisha migodi yote tulishindwa kuiendeleza. Ndipo mzee wa kubinafisisha aliingia na kubinafisisha tena.

Sasa mzee Mkapa alipokuwa anabinafisisha walikataa kurudi kuwekeza kwa sababu za kuwa huwa watanzania hatueleweki. Kutoka na hili Mzee wetu mkapa aliwashawishi kwa sera ya kwamba wakija kuwekeza ni lazima warudishe mitaji yao ndiyo waanze kulipa ushuru wa kampuni(corporate tax 30%). Na hiki ndicho kinachosemwa na CAG kama FREE CAPITAL 100%. Hii inamaana kuwa mtu akiwekeza mfano Mradi wa graphite mkoani lindi unaomilikiwa na URANEX Unahitaji $600milion(Tsh1.2trion) kuwekeza anatakiwa arudishe mtaji wake kwa 100% ndiyo aanze kulipa corparate tax. sasa utata tunapoibiwa ni hapa;

1. Uhakiki wa mtaji kama ni kweri pesa hizo zinawekezwa?
2. Mtaji wa kuendeshea( running cost za day to day)?
3. Uhakiki wa madini yanayozalishwa na data wanazotoa serikalini ni sahihi?
kutokana na kutokuwa makini na vitu vitatu hapo juu hivyo hujikuta kila mwaka makampuni yasema hatujarudisha mitaji hivyo wanaendelea kuchimba madini pila kulipa corparate tax.

Naomba nikumbushe kuwa swala la kurudisha mtaji lipo inch zote duniani katika secta ya madini isipokuwa inch zingine zinasheria kuwa awe anarudisha mtaji wake kwa kiwango kidogo kidogo. Mfano kama mgodi atachimba miaka 15 wanaugawa mtaji wake kwa miaka 15. Hivyo kila mwaka atapunguza kwa kiwango hicho lakini maana yake mtaji wake wote razima arudishe.

hapa huwa nabaki najiuliza tunaibiwa kwa sababu ya mikataba mibovu au usimamizi mbovu?


 
Umasikini na mbaya sana.

Engineer amekulia familia ya kimasikini tena kijijini, Mungu kamsaidia amefaulu shule akapenya penya mwisho anajikuta yuko kitengo cha kukagua na kuhakikisha kampuni zinalipa mapato yote. Hapa ndio mtihani unaanzia.

Umasikini mbaya sana. Ukoo mzima unamtegemea ndg. Engineer, na yeye ndo kashika kitengo.

Umasikini mbaya sana, acheni tu wachimbe yakiisha waondoke
 
Back
Top Bottom