JPM: Na Stori ya Mzee Kimweri

JPM: Na Stori ya Mzee Kimweri

EWGM's

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
1,521
Reaction score
2,112
Kipindi kile wakati niko shuleni. Nyakati za likizo watoto wote wa ukoo wetu tulikuwa tunakwenda kijijini kwa babu. Kule kijijini kulikuwa na kimgahawa karibu na stendi kuu ya mabasi. Chakula maarufu pale mgahawani kilikuwa ugali/wali na samaki wa kukaanga kutoka bwawa maarufu kule kijijini.

Kulikuwa na mzee mmoja anaitwa Kimweri, mzee huyu alikuwa kila ikifika jioni akitoka shambani lazima apite pale mgahawani kusalimia au kunywa chai. Tukaja gundua kitu kutoka kwake na tukakifanya ni mchezo. Yule mzee Kimweri alikuwa anapenda sana kusifiwa “sifa”.

Kuna siku tukazua mabishano ya kizushi baina yetu kuhusu yeye ili tuona atachukua hatua gani. Ndugu yangu akawa anasema Mzee Kimweri anakula sana pilipili, mimi nikawa najibu hamna chochote hawezi kitu sana sana atakula pilipili 2 au 3 tu.

Mzee Kimweri akadakia “nunueni ugali na samaki niwaonyeshe ulaji wangu wa pilipili”. Baada ya siku ile kula pilipili kichaa 6 basi tukafanya ni mchezo. Kila siku jioni tuna mnunulia ugali na samaki na mapilipili kibao ili avunje rekodi alizoweka siku zilizopita.

Wakati anakula pilipili yule mzee ulikuwa ukimtazama usoni unaona kabisa ana maumivu makali. Lakini kwa kuwa alikuwa anapenda sifa alikuwa anabugia tu, huku jasho linamtoka mpaka machozi na makamasi juu. Tukawa tunamchochea tu “Mzee Kimweri kiboko anakula pilipili, mtazame leo atakula 8 au 10” basi kwa sifa kila siku anazidisha idadi ili avunje rekodi yake mwenyewe.

Leo nimeikumbuka stori ya mzee Kimweri na nikitazama matendo ya JPM nimebaki nacheka tu.
 
''Tuna haki ya kuhoji na kuwakosoa wale wote waliopiga pushups tukawapa kura na sheria inaruhusu'' - Tundu A. Lissu
 
Nyie rukeni rukeni tu kama maharage ya mbeya sijui mtawaambia nin wananchi 2020 mana muda wote mnakaa nyuma ya kibodi kuandika wakat mwenzenu kaenda mpaka BUSELESELE huko shauri yenu.
.
.
.
kyenekyaka nkighanile une

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HHAHHAHAHAHAHAH,Dah Mkuu huyo mzee alikua jinga aisee,so ndio Mzee JPM Anafanana naye au siyo,we mtu wewe si kwa staili hiyo bana
 
Back
Top Bottom