Ningependa kujua Waandishi walipata fulsa ya kuumuuliza Mswali Bush...Naomba kujua waliuliza maswali gani...
Mwana_harakati, hicho kichwa cha habari cha thread yako kinaonyesha wewe unadharau. Baya zaidi, ni dharau inayoambatana na kujiona unajua, wakati hujui. Huo ni ujinga mbaya sana kwa kuwa kuufuta, hata kwa elimu ya watu wazima, ni vigumu. Kwanza nyoosha sentensi yako ili utuonyeshe kuwa nawe si kichekesho.
Ungekuwa kweli unataka tujadili hilo, ungetuambia ni vichekesho gani unavyoviona kwa journalist wa kibongo.
Kwa wale wenye shauku ya kujua maswali yaliyoulizwa, ni kwamba fursa ilikuwa watu wanne tu ndiyo wangepewa fursa ya kuuliza maswali; wawili toka vyombo vya wennyeji, wawili wageni.
Watu wetu, mmoja aliuliza ni kwa nini GWB ameamua kuja Afrika, na hasa Tanzania wakati huu, na si kabla, na kwamba kuna umuhimu gani sasa hivi? Mwingine aliuliza kwa namna gani GWB atamsaidia JK akiwa mwenyekiti wa AU kufanikisha utafutaji amani huko Dafur,Somalia, na Kenya?