Joshua Nassari usiwalaghai wapigakura Arumeru Mashariki

Kamura

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
506
52
Sasa hivi Nassari anaomba kura kwa kubeba vichanga mbona hakufanya hivyo kabla ya kugombea?
 
Unashangaa Nassari kubeba vichanga mbona hukushangaa waliopiga magoti na kukaa chini ?.
 
ni kuwa kwa sasa ndo vyombo vya habari vinamuangalia kwa ukalibu ila hii ni tabia yake mkuu, vp ulikuwa unamfuatilia kiasi hicho hebu sema jingine bwana achana na upuuuzi huu!

Angalia necha ya kuripoti matukio yake hasa gazeti la Nipashe mara kupewa upako feki leo Ukurasa wa 3 kabeba kichanga alikuwa wapi wakati wote. Tunamfahamu hana tabia hiyo.
 
Sasa hivi Nassari anaomba kura kwa kubeba vichanga mbona hakufanya hivyo kabla ya kugombea?

Habari za Kitaifa

Mke wa Sioi apiga magoti kuomba kura

....................................

MKE wa mgombea ubunge Arumeru Mashariki (CCM) Sioi Sumari, Pamela, juzi alianza kutumia mbinu ya kuwapigia magoti akina mama na vijana wa mji mdogo wa Usa River akiomba wamchague mumewe, katika uchaguzi huo utakaofanyika Aprili mosi.

Akitumia nafasi aliyopewa na mumewe kujitambulisha, Pamela aliyeonekana kukomaa kisiasa, alitumia dakika hizo chache kuwaomba wanawake na vijana kujitokeza kwa wingi ili kumchagua Sioi.

"Naitwa Pamela ni mama wa watoto watatu. Nimekuja hapa kuwaomba wananchi wa Usa River kumchagua mume wangu katika uchaguzi wa tarehe moja mwezi wa nne," alisema Pamela na kushangiliwa na umati wa watu.

Pamela, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alisema atatumia nafasi yake kama mama kumshauri ipasavyo mumewe endapo atachaguliwa, ili kuharakisha maendeleo ya Arumeru Mashariki.

Kwa upande wake, Sioi alimshukuru Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na kamati za siasa za wilaya ya Arumeru na mkoa wa Arusha, kwa kumteua kugombea ubunge.

Pamoja na kushukuru viongozi hao wa CCM na chama hicho, Sioi pia alimshukuru Pamela akisema amekuwa akimpa moyo na matumaini tangu alipojitosa katika kinyang'anyiro hicho.

Alisema kama atachaguliwa, kazi yake ya kwanza itakuwa ni kukamilisha ahadi za marehemu baba yake, Jeremiah Sumari, alipokuwa akiomba ridhaa ili kuchaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mkuu mwaka juzi.

"Nitatekeleza ahadi zote za Mbunge Sumari. Nazifahamu fika ahadi hizo na changamoto zinazoambatana nazo, nipo kutumia uwezo wangu na maarifa yangu kuzitatua," alisema.

Wakati joto la kisiasa likizidi kupanda, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, alianza kampeni kutoka juzi Arumeru Mashariki na anatarajiwa kuzindua rasmi kampeni za mgombea wa chama hicho, Abraham Chipaka, leo huku akijivunia historia yake ya kutatua mgogoro wa kidini wa Arumeru.

Mrema amekuwa akitumia muda mwingi kuomba wananchi wa Arumeru Mashariki kukumbuka alichowafanyia akiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani na baadaye Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana wa Serikali ya CCM ya Awamu ya Pili chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

"Nadhani ndugu zangu wa Arumeru mnafahamu kazi kubwa niliyofanya katika wilaya yenu nilipokuwa Waziri na Mbunge wa CCM, sasa naomba mkumbuke fadhila kwa kuchagua Mbunge wa TLP," alisema Mrema alipohutubia kwa muda mfupi baadhi ya vijana katika stendi ya mabasi ya Leganga, Usa River juzi jioni.

Pamoja na kuomba wachague mbunge wa TLP, lakini hatua hiyo ya Mrema kusema kuwa alipata mafanikio makubwa akiwa Waziri na Mbunge wa CCM, imekuwa ikitafsiriwa na vijana wa CCM jimboni hapa, kuwa inasaidia kukinadi chama chao.

"Hili liko wazi kabisa, Mrema anasaidia kukipaisha chama chetu. Alikuwa Mbunge wa CCM (Moshi Vijijini), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani lakini pia Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana katika Serikali ya CCM, hivyo ni sera za CCM zilizotatua mgogoro ule," alisema Abubakar Msuya aliyejitaja kuwa shabiki wa CCM.
 
ni kuwa kwa sasa ndo vyombo vya habari vinamuangalia kwa ukalibu ila hii ni tabia yake mkuu, vp ulikuwa unamfuatilia kiasi hicho hebu sema jingine bwana achana na upuuuzi huu!
Huyu alikuwa mchochezi wa vurugu na migomo UDSM wala hana la maana la kuwafanyia Arumeru.
 
Hakuna ulaghai hapa, ile habari ya assasination iliyofanywa na Mkapa dhidi ya hayati baba yetu ndo habari iliyotawala kwenye kila sikio la mpiga kura kwa sasa.
Wazee wa boma wanatafakari.
Kuitete CCM inahitaji uwe na akili ya maiti.
 
mshaanza kumuonea wivu mpiganaji wetu nassary, basi kama vp mwambieni gamba mwenzenu sioi akawabebe watoto wa kenya alipozaliwa.
 
Unashangaa Nassari kubeba vichanga mbona hukushangaa waliopiga magoti na kukaa chini ?.
09_10_xa137s.jpg
 
Huyu alikuwa mchochezi wa vurugu na migomo UDSM wala hana la maana la kuwafanyia Arumeru.

Kumbe uwa wanafikaga mpaka chuo kikuu na kuwa convice wasomi wenzao kugoma kupgania haki zao na wakamsikiliza,basi kumbe ana akili!me nilidhani ni kama wewe,mliopata elimu ya msingi tu na kuishia kujipendekeza kwa watu wa chama,kupiga kelele bila hoja,na kugoma kujiendeleza kielimu
 
Back
Top Bottom