Joseph Warioba azungumza ktk Kumbukizi ya Maisha ya Jaji Francis L. Nyalali

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
NYALALI ALIBADILI MAHAKAMA KUTOKA KUWA IDARA YA SERIKALI HADI MHIMILI

Familia, marafiki na viongozi wastaafu wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Francis Nyalali wamekutana Aprili 04 jijini Dar es Salaam, kwenye kumbukizi ya maisha ya Jaji huyo kwa ajili ya kujadili mchango wake katika Taifa ambapo wamebaini jinsi kiongozi huyo alivyoibadilisha Mahakama kutoka kuwa Idara ya Serikali na kuwa mhimili unaojitegemea.

Source: Millard Ayo

Joseph Warioba aliyepata kuwa Waziri Mkuu amesema ni Jaji Francis L. Nyalali alikuwa mtu asiye na makuu lakini ni mzalendo kweli kweli. Warioba aliyasema hayo akizungumza hayo mbele ya Mke wa Marehemu Mama Loyce Nyalali na Jaji Steven Bwana na wageni wengi waalikwa.

Warioba alisema kipindi chao ili kutenganisha mihimili ya Mahakama na Serikali Kuu, walikuwa na utaratibu wa kumfuata Jaji Mkuu Francis Nyalali ofisni kwake kwa mazungumzo ingawa baadhi ya vigogo serikali kuu walikuwa wanahoji kwanini Jaji Mkuu asiitwe ofisini kwa Waziri Mkuu maana Waziri ni mkubwa Zaidi ya Jaji Mkuu.

Lakini Joseph Sinde Warioba alikataa hoja hiyo ya kumuita Jaji Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu na badala yake walipendekeza wakutane sehemu neutral kunywa chai na kuzungumza masuala mazito na Jaji Mkuu. Na Mara nyingi Waziri Mkuu alimfuta Jaji Mkuu katika makazi yake rasmi ya kuishi na kunywa naye chai huku wakibadilishana mawazo kuhusu changamoto za mihimili hiyo miwili katika kutekeleza wajibu wao kwa kuheshimiana.

Joseph Sinde Warioba alibainisha kuwa Jaji Francis L. Nyalali alikuwa mwadilifu na alisimamia uadilifu ndani ya mahakama na kuongoza mradi mkubwa wa Mahakama kuanza kutumia TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano)/ ICT. Mahakama ilikuwa ni idara ya mwanzo kabisa kuingiza mfumo wa TEHAMA kabla ya idara /wizara zote za serikali ya Tanzania.

Mama Loyce Nyalali alizungumzia umuhimu wa wazee na viongozi kuandika wosia na kumbukumbu za Maisha yao kwa ajili ya manufaa ya familia na watanzania kwa ujumla kufahamu mchango wao katika nchi ya Tanzania.

Jaji Joseph Warioba asimulia Siku ya Uteuzi wa Francis L. Nyalali kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania

Source: MCL Digital

1062936

Makala /Uzi By SubiriJibu wa JamiiForums
Siyo Kenya tu Hata Tanzania Jaji Mkuu Francis Lucas Nyalali alitaka kujiuzulu
Hakuna Jaji atakayepelekeshwa mtu anavyotaka. Mwaka 1984 Jaji Francis Nyalali alimfuata Rais Nyerere pale Msasani na kumwambia kwamba kama nchi inaendelea kuendeshwa kwa misingi ya kutofuata sheria basi yeye kama Francis Nyalali atajiuzulu.

Mwalimu akaitisha kikao cha NEC ya CCM na Jaji Nyalali akaitwa kueleza dhana yake. Alishambuliwa na wajumbe wa NEC tena wengine ni wanasheria wenzake. Lakini wakati wanamshambulia vile hawakujua kwamba Nyalali hakuw ana shida na mashambulizi yao na wajuumbe wa NEC hawakujua kwamva Nyalali alishaanza kuongea na Rais pale Msasani na kadiri walivyokuwa wanapendekeza au kujipendekeza ili Rais amuweke ashinikize aondolewe, ndiyo kwanza Nyalali alikuwa nafurahia moyoni.

Wapo waliouliza, "Je, unamaanisha hata Rais anatakiwa kufuata sheria". Jaji Nyalali aliwashangaa watu kuuliza hivyo na bahati nzuai Rais alikaa kimya kumbe alikuwa akiijua tabia ya wanachama wake japo wngine ni wasomi tena wasomi wa sheria.

Kama mnakumbuka kipindi hicho kulikirthiri vitendo vingin vya kutokufuata sheria. Mtu alikuwa akipelekwa kwenue jeshi liitwalo "Sungusungu" anacharawa viboko hata 30 bila kufikishwa mahakamani.

Hivyo Nyalali aliona siyo muda wa kuendelea na ujaji mkuu wakati hali ni hiyo ambako ni kama vile sasa hana kazi.

Nimesahau kitu kimoja. Wakati Nyalali anaitwa kwenye NEC aliona awachukue majaji wenzake wakamsaidie kufafanua jambo lile na ndipo ule moto ukawaka ndani ya NEC. MMOja wa waliochukuliwa ni Jaji Agustino Ramadhani.

Tatizo la wajumbe wa NEC kama nilivyosema hawakuwa wamesoma muelekeo wa Rais Julius Nyerere na kukawa na hisia kwamba Jaji Nyalali na wenzake wangekubwa na sekeseka la kutaka kuilazimisha serikali ifutae ya mahakama badala ya kufuata "chama kushika hatamu".

Kilichotokea ni kwamba baada ya majadailiano Rais Nyerere akahitimisha kwa kauli iliyowashangaza wengi kwamba "kila mtu hapa nchini ataishi kwa kufuata sheria".

Hii ni kwa mujibu wa mahojiano ya Jaji Nyalali ambayo yamerekodiwa na media. Hata kabla ya kurekodiwa, kikao cha NEC kilipoisha gazeti la kesho yake yaani DAILY NEWS la May 31, 1984 lilitoka na kicha cha habari kisemacho "NEC stresses rule of Law".

Hivyo, mhimili wa mahakama ni mhimili usiojaribiwa na hautikisiki unapoamua kusimama kidete kama alivyosimama Jaji Francis Nyalali au majaji wa Kenya jana walioamua kiujasiri kwamba uchaguzi urudiwe.

Haki iko mahakamani. Mahakama ni mhimi uliojichimbia kuliko mihimili yote.

Chanzo: Mwananchi
 
Wanasheria wasomi wengi wazungumza katika kumkumbuka Jaji Nyalali juu ya Utawala wa Sheria

wanakumbusha hata utawala wa kikaburu uliokuwepo Afrika ya Kusini ndiyo nchi iliyokuwa inafuata Utawala wa Kisheria kwelikweli ndiyo maana Mwalimu Nyerere alisema kuna zaidi ya Utawala wa Sheria yaani Utawala wa haki. Jaji Mkuu Francis Lucas Nyalali hakupenda briefcase Lawyers alipenda rule of Law yaani Utawala wa Sheria wa haki kabisa. Kitabu cha Haki za Binadamu Tanzania mwaka 1997 cha Prof. Chris Maina Peter chapewa changamoto nyingi na Jaji Mkuu Nyalali . Paper ya Jaji Mkuu Francis Nyalali The Social Context of Judicial Decision Making in Tanzania

Source: Millard Ayo
 
Kilichotokea ni kwamba baada ya majadailiano Rais Nyerere akahitimisha kwa kauli iliyowashangaza wengi kwamba "kila mtu hapa nchini ataishi kwa kufuata sheria".
Rahisi tu kama hivyo. Ni kipi kisichoeleweka hapo?
Hivyo, mhimili wa mahakama ni mhimili usiojaribiwa na hautikisiki unapoamua kusimama kidete kama alivyosimama Jaji Francis Nyalali
Bado hii leo hali ipo hivyo huko, au imeanza kubomoka? Nawafikiria akina Mtungi, si watakuwepo wengi huko sasa; na akina Mashauri------na wengine.

Watu wenye 'calibre' ya Nyalali; kama ilivyokuwa 'calibre' ya Mwalimu Nyerere inazidi kuwa nadra sana kuwapata nyakati hizi.
Lakini wakati huu ndio ingetakiwa tuwe na watu wa aina hiyo wengi huko mahakamani.

Sisemi hawapo, ni swala la muda tu watajitokeza wahesabiwe, kama ilivyo hata huko Bungeni, na serikalini kwenyewe.

"kila mtu hapa nchini ataishi kwa kufuata sheria.'

Na kufuata sheria havipishani na kufuata taratibu katika utendaji. Kama ni matakwa ya 'mazingira', kuna taratibu zake zinazotakiwa kufuatwa, sio amri tu za mtu kwa kuwa anacho cheo kikubwa!
 
NYALALI ALIBADILI MAHAKAMA KUTOKA KUWA IDARA YA SERIKALI HADI MHIMILI

Familia, marafiki na viongozi wastaafu wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Francis Nyalali wamekutana Aprili 04 jijini Dar es Salaam, kwenye kumbukizi ya maisha ya Jaji huyo kwa ajili ya kujadili mchango wake katika Taifa ambapo wamebaini jinsi kiongozi huyo alivyoibadilisha Mahakama kutoka kuwa Idara ya Serikali na kuwa mhimili unaojitegemea.

Source: Millard Ayo

Joseph Warioba aliyepata kuwa Waziri Mkuu amesema ni Jaji Francis L. Nyalali alikuwa mtu asiye na makuu lakini ni mzalendo kweli kweli. Warioba aliyasema hayo akizungumza hayo mbele ya Mke wa Marehemu Mama Loyce Nyalali na Jaji Steven Bwana na wageni wengi waalikwa.

Warioba alisema kipindi chao ili kutenganisha mihimili ya Mahakama na Serikali Kuu, walikuwa na utaratibu wa kumfuata Jaji Mkuu Francis Nyalali ofisni kwake kwa mazungumzo ingawa baadhi ya vigogo serikali kuu walikuwa wanahoji kwanini Jaji Mkuu asiitwe ofisini kwa Waziri Mkuu maana Waziri ni mkubwa Zaidi ya Jaji Mkuu.

Lakini Joseph Sinde Warioba alikataa hoja hiyo ya kumuita Jaji Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu na badala yake walipendekeza wakutane sehemu neutral kunywa chai na kuzungumza masuala mazito na Jaji Mkuu. Na Mara nyingi Waziri Mkuu alimfuta Jaji Mkuu katika makazi yake rasmi ya kuishi na kunywa naye chai huku wakibadilishana mawazo kuhusu changamoto za mihimili hiyo miwili katika kutekeleza wajibu wao kwa kuheshimiana.

Joseph Sinde Warioba alibainisha kuwa Jaji Francis L. Nyalali alikuwa mwadilifu na alisimamia uadilifu ndani ya mahakama na kuongoza mradi mkubwa wa Mahakama kuanza kutumia TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano)/ ICT. Mahakama ilikuwa ni idara ya mwanzo kabisa kuingiza mfumo wa TEHAMA kabla ya idara /wizara zote za serikali ya Tanzania.

Mama Loyce Nyalali alizungumzia umuhimu wa wazee na viongozi kuandika wosia na kumbukumbu za Maisha yao kwa ajili ya manufaa ya familia na watanzania kwa ujumla kufahamu mchango wao katika nchi ya Tanzania.

Jaji Joseph Warioba asimulia Siku ya Uteuzi wa Francis L. Nyalali kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania

Source: MCL Digital

View attachment 1062936

Makala /Uzi By SubiriJibu wa JamiiForums
Siyo Kenya tu Hata Tanzania Jaji Mkuu Francis Lucas Nyalali alitaka kujiuzulu
Hakuna Jaji atakayepelekeshwa mtu anavyotaka. Mwaka 1984 Jaji Francis Nyalali alimfuata Rais Nyerere pale Msasani na kumwambia kwamba kama nchi inaendelea kuendeshwa kwa misingi ya kutofuata sheria basi yeye kama Francis Nyalali atajiuzulu.

Mwalimu akaitisha kikao cha NEC ya CCM na Jaji Nyalali akaitwa kueleza dhana yake. Alishambuliwa na wajumbe wa NEC tena wengine ni wanasheria wenzake. Lakini wakati wanamshambulia vile hawakujua kwamba Nyalali hakuw ana shida na mashambulizi yao na wajuumbe wa NEC hawakujua kwamva Nyalali alishaanza kuongea na Rais pale Msasani na kadiri walivyokuwa wanapendekeza au kujipendekeza ili Rais amuweke ashinikize aondolewe, ndiyo kwanza Nyalali alikuwa nafurahia moyoni.

Wapo waliouliza, "Je, unamaanisha hata Rais anatakiwa kufuata sheria". Jaji Nyalali aliwashangaa watu kuuliza hivyo na bahati nzuai Rais alikaa kimya kumbe alikuwa akiijua tabia ya wanachama wake japo wngine ni wasomi tena wasomi wa sheria.

Kama mnakumbuka kipindi hicho kulikirthiri vitendo vingin vya kutokufuata sheria. Mtu alikuwa akipelekwa kwenue jeshi liitwalo "Sungusungu" anacharawa viboko hata 30 bila kufikishwa mahakamani.

Hivyo Nyalali aliona siyo muda wa kuendelea na ujaji mkuu wakati hali ni hiyo ambako ni kama vile sasa hana kazi.

Nimesahau kitu kimoja. Wakati Nyalali anaitwa kwenye NEC aliona awachukue majaji wenzake wakamsaidie kufafanua jambo lile na ndipo ule moto ukawaka ndani ya NEC. MMOja wa waliochukuliwa ni Jaji Agustino Ramadhani.

Tatizo la wajumbe wa NEC kama nilivyosema hawakuwa wamesoma muelekeo wa Rais Julius Nyerere na kukawa na hisia kwamba Jaji Nyalali na wenzake wangekubwa na sekeseka la kutaka kuilazimisha serikali ifutae ya mahakama badala ya kufuata "chama kushika hatamu".

Kilichotokea ni kwamba baada ya majadailiano Rais Nyerere akahitimisha kwa kauli iliyowashangaza wengi kwamba "kila mtu hapa nchini ataishi kwa kufuata sheria".

Hii ni kwa mujibu wa mahojiano ya Jaji Nyalali ambayo yamerekodiwa na media. Hata kabla ya kurekodiwa, kikao cha NEC kilipoisha gazeti la kesho yake yaani DAILY NEWS la May 31, 1984 lilitoka na kicha cha habari kisemacho "NEC stresses rule of Law".

Hivyo, mhimili wa mahakama ni mhimili usiojaribiwa na hautikisiki unapoamua kusimama kidete kama alivyosimama Jaji Francis Nyalali au majaji wa Kenya jana walioamua kiujasiri kwamba uchaguzi urudiwe.

Haki iko mahakamani. Mahakama ni mhimi uliojichimbia kuliko mihimili yote.

Chanzo: Mwananchi

Leo, hasa wakati wa Awamu ya Tank, Mahakama imerudi kuwa Idara ya Serikali vivyo hivyo Bunge pia limegeuka kuwa ni Idara tu ya Serikali ambayo nayo imeachana na utawala wa sheria. Sasa ni vurugu tupu!
 
Back
Top Bottom