Joseph Sinde Warioba: Jiwe walilokikataa waashi

Joseph Sinde Warioba: Jiwe walilokikataa waashi

"Kulikuwa na ulazima gani wa kuunda tume kama tayari mlikuwa na majibu? Mliounda tume kwa minajili ya kutafuta jukwaa la kutukana wazee? Hivi ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya makamu Rais walitoa maoni ya dhati au ya kisanii? Je maoni yalitolewa kama chambo cha kutafutia sababu ya kumtukana Warioba? Kwa umri alionao huyu mzee atake kuvunja Tanzania ili apate nini hasa? Sisi wengine ni watazanzania halisi, tumelelewa kitanzania na kufunzwa adabu na heshima kwa wakubwa. Hatukufundishwa kudhihaki waliotuzidi umri, achilia mbali waliotuzidi elimu, uadilifu na uzoefu. Ninyi watoto mnaotukana wazee mmefilisika adabu, na nyie wazee mnaotukana wazee wenzenu mnahitaji kupimwa akili...........!"

Usikose kusoma makala hii ndani ya Gazeti la Raia Tanzania,Alhamisi May 1, 2014. Katika Jukwaa la Mwale Wa Demokrasia, ukurasa wa 19…

Inayoletwa kwako na Mwandishi radiki, Robert Lengeju
Imebidi nisome tena uzi huu baada ya kupata taarifa za kufariki kwa mtoa uzi. Alikuwa mwandishi mahiri sana. Apumzike kwa amani LENGEJU BOB, Ameni!
 
Imebidi nisome tena uzi huu baada ya kupata taarifa za kufariki kwa mtoa uzi. Alikuwa mwandishi mahiri sana. Apumzike kwa amani LENGEJU BOB, Ameni!
Kama mtoa mada amekufa basi hakuna haja ya kuchangia mada hii!
Rest In Peace [RIP), mtoa mada!
 
Kama mtoa mada amekufa basi hakuna haja ya kuchangia mada hii!
Rest In Peace [RIP), mtoa mada!
Sio kweli! Mtoa mada akifa haina maana kuwa mada nayo imekufa. Hapa tunajadili mada au hoja sio mtu. Shabani Robert na waandishi wengi walikufa miaka mingi iliyopita lakini vitabu vyao bado vinasomwa na kuchambuliwa mashuleni. Unataka kutwambia kwavile Shabani Robert kafa kwahiyo hata kitabu chake cha KUSADIKA tusikisome wala kukichambua? Mbona bado tunasikiliza na kuchambua hotuba za Nyerere? Tunaendelea kusikiliza na kuchambua nyimbo za waimbaji mbali mbali waliokwishafariki kama Marijan Rajabu na Mbaraka Mwinshe kwani tunachoaangalia ni maudhui ya nyimbo hizo kwa jamii ambayo yanarithishwa kizazi hadi kizazi. Pamoja na kuwa mimi sikuchangia mada ya marehemu isipokuwa nilikuwa naomboleza kifo chake ukweli unabaki wazi kuwa Uzi huu unabaki kwa jamii pamoja na kuwa mtoa mada katangulia mbele za haki tena kauandika kwa umahiri mkubwa na alikuwa kama ni mtu anayetoa wosia. Mkuu, wanazuoni wengi ambao huwa tunawatumia katika kuthibisha hoja zetu walishafariki lakini walichokiandika au kukiimba kimebaki kwa sisi tuliohai kwa ajili ya maisha yetu. Kwa mawazo yako ni kama unatwambia kwa vile mtoa mada kashafariki, basi tusisome maandiko yake. Hata wewe ukifa kama kuna mada au kitabu ulichoandika tutaendelea kusoma na kujadili maudhui yake na wewe tutakujadili kama mwandishi tukikupa sifa inayostahili kulingana na kazi yako. Akina Pilato, Sokrate, Isaack Newton, Nyerere, Martin Luther King, mitume na manabii mbali mbali ndio tunao watumia kujenga hoja zetu kutokana na umahiri wao katika kuelezea au kuvumbua mambo ingawa wao wameshakufa. Mawazo yako ni kama vile kutwambia kuwa kwakuwa mwenye basi amekufa kwahiyo tusipande basi lake au kwakuwa mwenye nyumba amekufa, nyumba yake ifungwe wasikae watu! Ajabu! Mada hii ilitolewa mwezi wa tano tarehe moja. Kuonesha kuwa iko hai na kuna wendawazimu wasiosikia, juzi juzi wamemfanyia fujo hadi kumpiga Jaji Joseph Warioba wakati akiwa anatoa mada katika mdahalo pale Ubungo kwenye hoteli ya Blue Pearl
 
Back
Top Bottom