TAARIFA KWA WANAROMBO:Itakumbukwa kuwa pamoja na mambo mengine; Changamoto za Rombo ni Ukosefu wa Maji na Uvamizi wa Tembo kwenye mashamba naMakazi ya Wananchi.1. Tatizo la maji kwa Jimbo la Rombo limekuwepo miaka mingi kutokana na kukosekana kwa Mipango thabiti ya kudumu ya kumaliza tatizo hili. Tangu nimechaguliwa kuwa Mbunge nimefuatilia na hatimayekufanikiwa kupata jumla ya visima 30 kwa mchanganuo ufuatao.(i) Visima 10 - Mradi unaofadhiliwa na World Bank(ii) Visima 14 - Mradi wa PWB(iii) Visima 6 - Msaada kutoka kwa Mzee Mustapha Sabodo.Miradi ya WB na PWB tayari mikataba imesainiwa na kazi ya Usanifu imeanza wataalam wapo Site kuanza miradi hiyo mapema iwezekanavyo. Mradi wa visima 6 vya msaada kutoka kwa Mzee Mustapha Sabodo tunatarajia kuanza utekelezaji wake (Ikiwa ni pamoja na kutambua sehemu vitakakochimbwa) baada ya vikao vya bunge la Bajeti.Natambua uhaba wa maji kwa Wananchi wa Rombo ni Tatizo kubwa na Mradi wa maji wa Kili Water bado haujaweza kuwasaidia wananchi wangu kama ilivyolengwa. Watu wasio na nia njema wamekuwa wakihujumu mradi huo na kuwakosesha Wananchi wengine maji kwa wakati na baadaye kuwauzia maji hayo kwa bei kubwa. Nashukurusana wananchi wanaoendelea kunipa ushirikiano kwa kunitumia majina ya wanaohujumu miradi ya maji na nitawashughulikia mara tu baada ya bunge hili.2. Tatizo la tembo ambao wamekuwa wakivamia mashamba ya watuna kuharibu mali/kujeruhi watanchi nimefanya utafiti wa kina na kugundua yafuatayo;Tembo wamekuwa wakikimbia ukame kwenye nchi za Sudani na Somalia na kuja maeneo ya kenya lakini kutokana na baadhi ya wamiliki wa mashamba makubwa huko kenya kuzungusha uzio wa Umeme tembo hao wamekuwa wakija mpakani na hatimaye kuingia Tanzaniahasa Rombo na kufanya uharibifu mkubwa wa watu na Mali zao. Sheria za umoja wa Mataifa zinakataza kuuawa kwa wanyama kama. Hata hivyo njia pekee iliyobaki nimeamua kufanya mazungumzo na Serikali kuu ili ikutane na Serikali ya Kenya tuone namna tunaweza kudhibiti Tembo hao. Utaratibu wa sasa wa kufidiwa kwa wananchi ambao watapata uharibifu kutokana na Tembo hao bado unaendelea kama nilivyosema kwenye mikutano yangu ya hadhara kwenye maeneo kadhaa huko Jimboni..Nimeona nitoe ufafanuzi huu wa awali kutokana na maswali haya kuzidi kwenye INBOX na sehemu mbalimbali Jimboni. Kama mtu ana Ushauri wowote wa kutatua kero hizo kwa njia nyingine pia nakaribisha ushauri hapa chini na nitauchukua kama unatekelezeka.Ahsanteni sana!Mungu Ibariki Rombo,Mungu ibariki Tanzania,Mungu Ibariki CHADEMA na Watu wake.Joseph SelasiniMb.Rombo - CHADEMA