Joseph selasin mbunge (chadema) amvua nguo mwigulu nchemba kwa uongo

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
[h=6]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UZUSHI UNAOENEZWA NA MH.MWIGULU NCHEMBA JUU YANGU NA CHAMA CHANGU.
Ndugu zangu kwanza nachukua nafasi hii kuendelea kumshukuru Mungu kwa afya njema anayoendelea kunijalia mimi na Mke wangu hapa Hospitali ya KCMC. Pia niwashukuru wote walionifariji/wanaoendelea kunifariji katika kipindi chote cha matatizo yaliyotokea.

UTANGULIZI.
Itakumbukwa kuwa tarehe 28/05/2012 nilipata mbaya ya gari. Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Boma karibu na chuo cha VETA. Watu wa kwanza kufika kwenye Eneo la ajali na kutupa msaada walikuwa ni Askari Polisi waliokuwa Doria karibu na eneo lile na Raia waliofika wa pia walikuwemo MWENYEKITI WA CHADEMA (W) YA HAI pamoja na MWENYEKITI WA BAVICHA (W) YA HAI. Walisaidiana na Polisi kuchukua majeruhi (Mimi nikiwemo) pamoja na marehemu waliofariki pale hadi Hospitalini.
Baada ya kufika hospitalini pia walifika MHE.MEYA WA MANISPAA YA MOSHI (AMBAYE PIA NI DIWANI WA CHADEMA) akiongozana na baadhi ya VIONGOZI WA CHADEMA WA KATA YAKE NA BAADHI YA MAENEO YA MOSHI MJINI.. Baadaye alifika KATIBU WA CHADEMA MKOA WA KILIMANJARO AKIONGOZANA NA BAADHI YA MADIWANI WA CHADEMA WA MOSHI NA ARUSHA na Viongozi wengine ambapo nakumbuka walitokea Wilaya ya Mwanga kwenye Mikutano ya Hadhara. Tulikuwa wote hadi tunapatiwa huduma na majeruhi tukapelekwa Wodini. Siku iliyofuata nilipokea Simu kutoka kwa MHE. FREEMAN MBOWE (MWENYEKITI WA CHADEMA NA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI) akiwa Mtwara kwa shughuli za Chama akinipa Pole kwa yaliyotokea na kunifariji.
Baadaye hali yangu ilipoimarika kidogo tukapanga taratibu za mazishi ya Marehemu Mama yangu Mzazi (R.I.P) na miongoni mwa watu waliohudhuria kwanza ni WANACHAMA WA CHADEMA, MADIWANI WOTE WA CHADEMA ARUSHA, MADIWANI WA MOSHI MJINI NA MOSHI VIJIJINI. Kutoka makao makuu ya CHADEMA waliwakilishwa na Mhe.Rwakatare na Ndg.Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Utawala) Pia walihudhuria Baadhi ya WWABUNGE WA CHADEMA wakieleza sababu za viongozi na wabunge wengine kutokuhudhuria (Na zilikuwa Sababu za Msingi kabisa) kwa sababu hata baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria walileta salam za wakubwa wao ambao nao walitamani kuhudhuria lakini kutokana na sababu mbali mbali walishindwa!..
Pamoja na hayo,MHAMA JOSEPHINE MUSHUMBUSI (MKE WA MHE.KATIBU MKUU WA CHADEMA) alinitembelea hospitalini akiwa na wajumbe kadhaa... Aliniletea salam za pole kutoka kwa KATIBU WANGU MKUU WA CHAMA. Nilifarijika sana kuona kuwa kiongozi wangu pamoja na kuwepo kwake safarini kikazi lakini bado aliweza kutuma ujumbe kwangu..
Baadaye nilihamishiwa MOI (Muhimbili) kwa ajili ya matibabu Zaidi. Nakumbuka walifika wabunge wengi sana wa CHADEMA lakini kubwa zaidi alifika MHE.FREEMAN MBOWE (MWENYEKITI WA CHADEMA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI).

KANUSHO.
Nimekuwa nikisikia kwenye vyombo vya habari kuwa Mwigulu Nchemba (Mb-CCM) Anatangaza kuwa Chama changu kimenitupa na hakina msaada wala Ushirikiano na mimi kwenye Matatizo yaliyojitokeza..
Kwanza: Sijawahi kumwajiri Mwigulu Nchemba kuwa msemaji wangu!.
Pili: Mwigulu Nchemba si mkweli na hajui chochote kuhusu mimi wala CHADEMA.
Tatu: Mwigulu Nchemba anataka nionekane sina shukrani kwa viongozi na Chama changu kwa Umoja na Ushirikiano wanaoendelea kunipatia hata sasa.
Nne: Viongozi wangu wanafuatilia kwa karibu sana matibabu yangu na Mke wangu.

MWISHO:
Naomba Mwigulu aelewe kuwa sitaki malumbano yasiyo na Tija kwangu wala kwa Wananchi wangu Walionichagua. Pia nisingependa kumtaja Marehemu Mama Yangu (R.I.P) kabla hata ya Arobaini. Zaidi ya yote akumbuke kuwa Viongozi na Wabunge wa CHADEMA wana mambo mengi ya kufanya na hawatakuwa tayari tena kujibu uongo na uzushi DHAIFU kama aliouzusha!!.

Ahsanteni Sana,
Mungu aendelee kuwabariki.
Joseph Selasini
(Mb) Rombo-CHADEMA.[/h]
 
Huyu Nchemba anavyotajwa tajwa hivi ndio mnazidi kumpa 'bichwa' kwanini asipuuzwe tuu!!
 
Huyu mnyatulu Mwigulu chogo chemba ni mpumbafu kwa sababu gani, pale Kijiji cha Sukamahela kuna kambi ya wakoma, kijiji hicho ni kimo kwenye jimbo la uchaguzi la Mhe John Chiligati mbunge wako mkoa mmoja na chogo Chemba, sasa , sasa wakoma wale wamepewa magodoro na wafadhili, magodoro hayo yanataka kupita njia zingine yasiwafikie walengwa , sasa Mhe Chogo chemba asiwasemee wakoma hao ambao( kati ya wakoma hao mwingine ni shangazi yake chogo chemba) wanataka kuporwa haki yao akisaidiana na mbunge mwenizie Chiligati anamsemea Mhe. Selasini hivi inaingia kweli akilini? Kama Mh Selasini wabunge wenzie wa CDM wamemtosa ndo na wao wawatose wale wakoma masikini ambao wanawaulizia kweli hasa shangazi yake Nchemba ambae anaitwa ZELEYAGALA sasa hivi wamekaa barabarani wanaomba wanaopita kwenye mabasi yaendayo mwanza. KWELI HUYU MWIGULU CHOGO CHEMBA NI STUPID KABISA.

source. Mimi mwenyewe nimeikuta hiyo scandal live jana niko kijiji cha solya karibu na Sukamahela.
 
"Sijawahi kumwajiri Mwigulu Nchemba kuwa msemaji wangu"Hii sehemu imenifurahisha sana,ina maana jamaa ana kiherehere.
 
Nchemba aka _____________ (jaza jibu sahihi) ni mropokaji sana. Mwisho wake kisiasa utakuwa mbaya
 
chemba kwa kifupi ni kati ya wabunge wajinga ndani ya bunge hili la awamu ya nne ya jk ukisikiliza michango yake bungeni unaweza fikiria kuna wabinge wana vuta ndio wanaingia bungeni na mmoja wapo ni chemba akifuatiwa na ndugu yake wa jimbo la mtera
 
Huyu mnyatulu Mwigulu chogo chemba ni mpumbafu kwa sababu gani, pale Kijiji cha Sukamahela kuna kambi ya wakoma, kijiji hicho ni kimo kwenye jimbo la uchaguzi la Mhe John Chiligati mbunge wako mkoa mmoja na chogo Chemba, sasa , sasa wakoma wale wamepewa magodoro na wafadhili, magodoro hayo yanataka kupita njia zingine yasiwafikie walengwa , sasa Mhe Chogo chemba asiwasemee wakoma hao ambao( kati ya wakoma hao mwingine ni shangazi yake chogo chemba) wanataka kuporwa haki yao akisaidiana na mbunge mwenizie Chiligati anamsemea Mhe. Selasini hivi inaingia kweli akilini? Kama Mh Selasini wabunge wenzie wa CDM wamemtosa ndo na wao wawatose wale wakoma masikini ambao wanawaulizia kweli hasa shangazi yake Nchemba ambae anaitwa ZELEYAGALA sasa hivi wamekaa barabarani wanaomba wanaopita kwenye mabasi yaendayo mwanza. KWELI HUYU MWIGULU CHOGO CHEMBA NI STUPID KABISA.

source. Mimi mwenyewe nimeikuta hiyo scandal live jana niko kijiji cha solya karibu na Sukamahela.

Nchemba jibu hoja hizo, acha kukenua meno bungeni wkt hata shangazi yako yuko mitaani anatarandaranda kwa kuomba.
 
Hana maana huyo kada, hakuna hoja zozote za maana anazochangia bungeni kazi yake kupiga kelele na kukosoa tarakimu na maneno, inabidi aende shule za kata akafundishe kiswahili.
 
ugua pole kamanda,huyu mwigulu chana naye kwanza upone na inaonekana alitaka kusikia chochote kutoka kwako
 
hivi huyu mwehu chemba ya mav* si member humujf?yes ni member,au alijiunga apige kampeni za meru halafu akimbie..awe jasiri kama mwenzake kigwangalla anayeapia miungu yote kuwa hatorudi tena jf lakini masaa mawili baadae anaanzisha thread..chezea jf wewe!!!muulize msekwa....so addictive
 
Huyu Mwigulu chizi kweli kazi kujisifia bungeni kumbe shangazi yake anaungua jua tuu. Huyu atakuwa anawashwawashwa
 
Back
Top Bottom