Joseph Pombe Magufuli anayo nafasi bado kupata sifa na shwange anazotaka kwa kufuata ushauri huu

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,932
5,560
Wana JF,

Rais bado anayo nafasi kubwa sana kupata shangwe na sifa anazotaka kwa kufanyia kazi mambo muhimu sana;

1-Joseph Pombe Magufuli anatakiwa kuhahikisha mchakato wa kuanza kuandika katiba mpya unaanza mpya .maoni ya wananchi yaliyotolewa kwenye rasimu ya Warioba yanafanyiwa kazi.

2-Joseph Pombe Magufuli anatakiwa kushauriana na bunge juu uamuzi wa kuzuia matangazo ya bunge kurushwa live kupitia TBC .

3-Joseph Pombe Magufuli anatakiwa kukaa na kuongea vyombo vya usalama kuruhusu vyama vya siasa kufanya mambo yao kwa kufuata sheria. Hakuna nchi imeweza kupiga hatua maendeleo kwa kukagandamiza demokrasia.

4.Joseph Pombe Magufuli anatakiwa kukubali kukoselewa kwa kuruhusu uhuru wa watu kutoa maoni.Tofauti ilivyo sasa ukitoa maoni yako kuhusu kuiokosoa serikali unaitwa kuhojiwa.

5.Joseph Pombe Magufuli anatakiwa kushughulikia mafisadi kuanzia ngazi ya juu mpaka ngazi ya chini kwa kufuata sheria.

6-Joseph Pombe Magufuli anatakiwa kufikiria tena uamuzi wake wa kuzuia wafanyabiashara kuagiza sukari kutoka nje.

Washauri wa rais mshaurini kuhusu hayo mambo ni muhimu sana kufanyia kazi haraka sana.
 
Mkuu tatizo huyu mtu anajiona yeye ndiye yeye hashauriki kabisa. Pia hilo la katiba mpya ya rasimu ya Warioba sahau kabisa Mkuu. Huyu mtu anajua ili "kushinda" 2020 anaihitaji hii katiba fake na Tume fake ya uchaguzi ili waibe tena uchaguzi kama walivyofanya 2015.

Anajua fika katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ni kuizika kabisa CCM nchini na yeye kushindwa vibaya sana kwenye uchaguzi wa 2020.

Wana JF

Raisi bado anayo nafasi kubwa sana kupata shwange na sifa anazotaka kwa kufanyia kazi mambo muhimu sana ÷
1-JPM anatakiwa kuhahikisha mchakato wa kuanza kuandika katiba mpya unaanza mpya .maoni ya wananchi yaliyotolewa kwenye rasimu ya Warioba yanafanyiwa kazi
2-JPM anatakiwa kushauriana na bunge juu uamuzi wa kuzuia matangazo ya bunge kurushwa live kupitia TBC 1
3-JPM anatakiwa kukaa na kuongea vyombo vya usalama kuruhusu vyama vya siasa kufanya mambo yao kwa kufuata sheria. Hakuna nchi imeweza kupiga hatua maendeleo kwa kukagandamiza demokrasia.
4.JPM anatakiwa kukubali kukoselewa kwa kuruhusu uhuru wa watu kutoa maoni .Tofauti ilivyo sasa ukitoa maoni yako kuhusu kuiokosoa serikali unaitwa kuhojiwa.
5.JPM anatakiwa kushughulikia mafisadi kuanzia ngazi ya juu mpaka ngazi ya chini kwa kufuata sheria .
6-JPM anatakiwa kufikiria tena uamuzi wake wa kuzuia wafanyabiashara kuagiza sukari kutoka nje .
Washauri wa raisi mshaurini kuhusu hayo mambo ni muhimu sana kufanyia kazi haraka sana.
 
Mkuu tatizo huyu mtu anajiona yeye ndiye yeye hashauriki kabisa. Pia hilo la katiba mpya ya rasimu ya Warioba sahau kabisa Mkuu. Huyu mtu anajua ili "kushinda" 2020 anaihitaji hii katiba fake na Tume fake ya uchaguzi ili waibe tena uchaguzi kama walivyofanya 2015.

Anajua fika katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ni kuizika kabisa CCM nchini na yeye kushindwa vibaya sana kwenye uchaguzi wa 2020.
Bila Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi basi bado tuna safari ndefu sana kuondoa utawala huo 2020 kama hashauriki yule mshauri alimteua wa kazi gani ?
 
Mkuu mtu anayemuogopa yule aliyemteua kamwe hawezi kutoa ushauri muafaka kwa kuogopa "kutumbuliwa" hivyo atatoa ushauri wa kinafiki ili tu kumfurahisha muhusika. Bila katiba mpya ya rasimu ya Warioba bado tuna safari ndefu sana Mkuu.

Bila Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi basi bado tuna safari ndefu sana kuondoa utawala huo 2020 kama hashauriki yule mshauri alimteua wa kazi gani ?
 
Hahahaaa!! Yaani asiyoyapenda kufanyika wewe ndo unamshauri ayafanye. Seriously?
 
Kabisa Mkuu pale Bungeni kaingiza jipu Tulia ili tu kuwadhibiti Wabunge wa UKAWA na sasa kaamua pia kuwadhibiti Wabunge wa UKAWA nje ya Bunge ili wasikemee maovu mbali mbali ndani ya Serikali hii ya kukurupuka ikiwemo ufisadi wa Lugumi, UDA, PRIDE, Escrow, Ukwapuzi wa nyumba za Serikali, Ununuzi wa boti lililooza kwa bilioni 8.

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali inapigwa vumbi Ikulu na Bungeni. Bungeni haitajadiliwa kwa sababu huyu aliyejitoa kafara kupambana na ufisadi hataki ripoti hiyo ya CAG ijadiliwe kwa sababu tu kuna ufisadi unaomuhusu yeye na maswahiba wake waliompigia debe kuingia Ikulu.

Wabunge wetu wanatakiwa kulipigia sana hilo swala katiba na Tume huru ya uchaguzi kwa sababu hata ukiangalia madaraka ya raisi yamekuwa makubwa sana ndo maana leo tumefika hapa tulipo kutokana ubovu wa katiba iliyopo ambayo raisi anamteua mpaka tume ya uchaguzi ambayo haiwezi kwenda kinyume na matakwa ya boss wake
 
Ni sawa mkuu lakini wabunge gani hao wa kuipigania katiba ya warioba? Hawa wa "NDIYO" na kukata viuno? Katiba ni swala la Taifa ni bahati mbaya sana katika nchi hii katiba imekua ni swala la CCM so pale inapowaharibia ufalme wao basi inakua batili na ndio maana umeona jaji walioba akidhalilishwa na wakubwa kabisa walioko na waliokuwepo madarakani na vibaraka wao wakaenda mbali zaidi hata kumpiga
 
Tulia yupo pale bungeni kwa kazi maalumu ambayo ameagizwa. Pamoja uamuzi wa wabunge wetu kutohudhuria vikao vya bunge vinavyoongozwa na Tulia bado wapinzani walikuwa haja kutumia zaidi hiyo kutoka nje kwa sababu mambo mengi ya umuhimu wanawaachia wabunge wa CCM hawana hoja za kuiokosoa serikali ya kuisifia kwa kila kitu ndo maana nchi tumefika hapa tulipo kutokana utawala wa CCM pamoja wabunge kwa kushindwa kuisimamia serikali. Hata kwenye tuhuma za ufisadi kama Escrow waliotuhumiwa wengine na wabunge na mawaziri wa serikali iliyopo madarakani leo. Kwenye hili sakata la Lugumi natamani wabunge wetu wangekuwepo ingetusaidia kufahamu nini kinachoendelea hapo kuna siri kubwa inataka kufinikwa kama ilivyokuwa kwa tuhuma nyingine
Kabisa Mkuu pale Bungeni kaingiza jipu Tulia ili tu kuwadhibiti Wabunge wa UKAWA na sasa kaamua pia kuwadhibiti Wabunge wa UKAWA nje ya Bunge ili wasikemee maovu mbali mbali ndani ya Serikali hii ya kukurupuka ikiwemo ufisadi wa Lugumi, UDA, PRIDE, Escrow, Ukwapuzi wa nyumba za Serikali, Ununuzi wa boti lililooza kwa bilioni 8.

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali inapigwa vumbi Ikulu na Bungeni. Bungeni haitajadiliwa kwa sababu huyu aliyejitoa kafara kupambana na ufisadi hataki ripoti hiyo ya CAG ijadiliwe kwa sababu tu kuna ufisadi unaomuhusu yeye na maswahiba wake waliompigia debe kuingia Ikulu.
 
Natamani wabunge wote wa CCM waige mfano wa mbunge mwenzao Hussein Bashe ambaye akisimama bungeni anaongea kwa kuweka maslahi taifa mbele tofauti hao wenzake ambayo wanaweka maslahi chama kwanza. Mchakato wa katiba ya Warioba unaweza kufanikiwa kupita endapo wabunge wakitambua wajibu wao

Back
Top Bottom