Joseph Mbilinyi (Sugu) aikabidhi kiwanja CHADEMA Mbeya Mjini

Joseph Mbilinyi (Sugu) aikabidhi kiwanja CHADEMA Mbeya Mjini

Sugu amefanya jambo la maana sana. Anapaswa kupongezwa.

NB: nje ya mada, je ni kweli Marcus Albanie amefukuzwa CDM?
Marcus ni Genius kipanga haswaa maisha yake hayahitaji Chadema
 
Sijui lolote ? bali natambua kwamba mtu hufukuzwa na vikao vya chama , sijaona wala kusikia kikao kilichokaliwa kwa ajili hiyo , halafu afukuzwe kwa lipi hasa ?

Ngoja nichunguze
Nitashukuru kwa taarifa hiyo boss.
 
Katika kusherehekea sikukuu ya Uzinduzi wa Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iliyofanyika Ikulu ya Magogoni , huko Mjini Mbeya, Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo, Mwekezaji na Mfanyabiashara wa Kimataifa , Bilionea Joseph Mbilinyi AMEIPA CHADEMA KIWANJA KIKUBWA kwa ajili ya kujenga Majengo ya Chama hicho.

Amekabidhi Kiwanja hicho kinachopakana na barabara kuu kwa viongozi wa Chadema Jimbo la Mbeya Mjini, ambapo amesema anataka abiria kutoka Congo au Zambia wakiwa kwenye basi la TAQWA wawe wanaliona Jengo la Chadema Mbeya Mjini.

Kwa niaba yangu binafsi nachukua nafasi hii kumshukuru Mwekezaji huyu kwa msaada wake huu.
Safi sana. Ni sawa na viwanja vya Mwananyamala walikuwa wanakabidhiwa TANU na Mzee Tambaza. Ni vya TANU, siyo vya umma. Na vya Sugu ni vya CHADEMA, siyo vyake tena kama Waarabu wa CUF walivyonyanganya majumba ya Mjimkongwe waliyowapa CUF lakini lilipoingia liprofessor Lipumba wakawanyanganya tena. Na Sugu akihamia CCM kesho wasiwe na hofu, bado yao.
 
Jambo zuri...

Wajenge kitu cha maana sasa...
 
Utawaweza Hao? Wameshazoea kurundika wanafunzi kwa kuwapalamiza malori, wale maofisa wengine kama hukuhudhuria inabidi ujieleze kwa nini usifutwe kibarua😀😀😀😀😀
People's wakowapi waliosema Chadema imekufa anzeni kuishuhudia Sasa nyomi kwenye mikutano ya hazara mkiwa Mngali hai hamjafa
 
Ofisi ya nini tena? Na tulikubaliana hazina umuhimu watu wanataka maendeleo tu.
 
Safi Sana Bilionea Sugu Moto Chini talanlalalalaaaaa ni MOTO CHINI.

Nafika mpaka bamako sio tu san fransico huku kote nafika katika kutafuta mshiko.

Mapromota koko sasa namiliki bunduki sitaki amani kwenye madili feki.
 
Katika kusherehekea sikukuu ya Uzinduzi wa Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iliyofanyika Ikulu ya Magogoni , huko Mjini Mbeya, Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo, Mwekezaji na Mfanyabiashara wa Kimataifa , Bilionea Joseph Mbilinyi AMEIPA CHADEMA KIWANJA KIKUBWA kwa ajili ya kujenga Majengo ya Chama hicho.

Amekabidhi Kiwanja hicho kinachopakana na barabara kuu kwa viongozi wa Chadema Jimbo la Mbeya Mjini, ambapo amesema anataka abiria kutoka Congo au Zambia wakiwa kwenye basi la TAQWA wawe wanaliona Jengo la Chadema Mbeya Mjini.

Kwa niaba yangu binafsi nachukua nafasi hii kumshukuru Mwekezaji huyu kwa msaada wake huu.
Lucas mwashambwa hebu soma uzi huu
 
Back
Top Bottom