Joseph Kabila afanya mabadiliko katika jeshi la DRC

Joseph Kabila afanya mabadiliko katika jeshi la DRC

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,201
Reaction score
64,646
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo joseph Kabila amefanya mabadiliko katika jeshi la serikali ya nchi hiyo, FARDC ambapo baadhi ya maafisa waliokuwa kwenye usimamizi wa jeshi la Polisi nchini humo wamepewa nyadhifa muhimu ndani ya jeshi la nchi hiyo.

Miongoni mwa maafisa hao ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la polisi John Numbi Banza Tambo ambaye amekuwa akituhumiwa kuhusika na mauaji ya mwanaharakati Floribert Chebeya aliyeuawa akiwa mikononi mwa Polisi Juni 02 mwaka 2010, jijini Kinshasa.

Haya yanajiri wakati ambapo mvutano wa kisiasa nchini DRC unaendelea kutokota, huku wanasiasa wakitaka matumizi ya mashine za kielektroniki za kupigia kura wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu.

Baadhi ya wanasiasa hasa wale wa upinzani wanasema hawatoshiriki uchaguzi iwapo Joseph Kabila atawania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi huo.

Chanzo: RFI
 
Joseph Kabila angeachia madaraka tu kwa amani then atafute nchi atakayohamia aishi kwa amani. Watamuua kama baba yake asipoangalia.

Sijui kwanini wakishakuwa marais huwa wanajisahau hivi.
 
Joseph Kabila angeachia madaraka tu kwa amani then atafute nchi atakayohamia aishi kwa amani. Watamuua kama baba yake asipoangalia.

Sijui kwanini wakishakuwa marais huwa wanajisahau hivi.
Uwa wanaona wamepewa hati miliki ya nchi hizo na pia uwa wanajiona ni next to God
 
Back
Top Bottom