Jose Mourinho: Mkufunzi wa Manchester United anaonekana kupitwa na wakati - Chris Sutton

Propaganda ya vyombo vya habari vya England, wanamchukia sana Mourinho.
Japokua Kweli Mourinho mda mwingine anakera hila vyombo vya habari vya England vinaongoza kwa kumsimanga Mourinho.

Bila kufanya hivyo hawawezi kuuza hard copy au kupata "traffic" kwenye magazeti yao ya online.
 
Maana yako nini? Kwahiyo nawe unaona ni kosa hapo paliposahihishwa ili ieleweke kirahisi kwa wote?
Sijakuelewa bado umesimamia wapi?


Wapi nimesema ni kosa? You did right ndio maan nikasema inategemea na alivyokosolewa. Hebu fikiri ungemwita kilaza ange respond namna gani.
 
safi sana kwa kuleta challenge....hata kama mo akipondwa bado ni kocha mzuri huwezi mfananisha na kocha ambaye timu yake ni ya ishirini
 
View attachment 721012

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anaonekana kupitwa na wakati na tabia zake zimebadilika , kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton.

Mourinho amekosolewa na baadhji ya mashabiki wa United pamoja na wachanganuzi wa kandanda kwa mtindo wake wa kucheza kandanda unaoonekana kutokuwa na mbinu mpya.

United iko katika nafasi ya pili katika ligi ya Uingereza na wako katika nusu fainali katika kombe la FA lakini walibanduliwa katika kombe la vilabu bingwa wiki iliopita.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright aliambia BBC Radio 5 live asingependelea kucheza chini ya Mourinho hivi sasa.

United wako pointi 16 nyuma ya Manchester City katika ligi huku kukiwa imesalia mechi nane na itachuana na Tottenham mwezi ujao ili kufika fainali ya kombe la FA.

Lakini huku City ikiwa imefanikiwa kufunga mabao 85 katika ligi ya Uingereza msimu huu , United imefunga mabao 58 pekee, ikiwa ndio machache zaidi miongoni mwa timu nne bora katika ligi hiyo kulingana na jedwali.

Red Devils walibanduliwa katika kombe la Ulaya na Sevilla, walioshinda 2-1 katika uwanja wa Old Trafford huku City na Liverpool zikisonga mbele katika robo fainali.

Sutton akizumnguza siku ya Jumatatu alisema: Mourinho amebadilika yeye binafsi kutoka alivyokuwa 2004. Anaangazia maswala madogo ya kijinga. Je ni janga kwa Man United kwa sasa? Hapana.

Lakini hilo ndio lililokuwa lengo la Mourinho kuja Man United na kumaliza nyuma ya City na kutokuwa na ari ya kuwania mataji makubwa? amepitwa na wakati.

Anaangalia City na mtindo wa soka wao na Liverpool .Huyu ni mtu ambaye alisajiliwa na Man United kwa kuwa alikuwa anaonekana kuwa na kipaji , Sasa anaonekana amepitwa na wakati kutokana na mtindo wa mchezo wake na vile timu nyengine zinavyocheza.

Mourinho mwenye umri wa miaka 55 alishinda ligi ya Uingereza mara tatu , mara mbili akiwa mkufunzi wa Chelsea.

Alimrithi Louis van Gaal kama mkufunzi wa United mnamo mwezi Mei 2016 na ameshinda kombe la EFL pamoja na lile la Yuropa katika msimu wake wa kwanza .

Wright anamlaumu mkufunzi huyo kwa kuleta kiza katika klabu hiyo .

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza alisema: Sijui amefanywa nini. Klabu hiyo ilimleta Mourino ili kuleta ubora ,ametumia fedha nyingi lakini anazozana na kila mtu.

Manchester City inacheza mtindo wa kandanda ambao ni mzuri na unaonekana .

Chanzo: BBC Swahili
Mourinho ni mjinga tu
 
Mimi sipendi sana mpira ila nashindwa kuelewa
How time ya pili kwenye msimamo wa ligi iwe na kocha mbaya?

That's mean timu za kumi kushuka chini zina walimu wazuri au
Angalia Pesa aliyotumia kusajili, point alizoachwa na anayeongoza, makombe na timu zilizomtoa mwisho tofauti ya point na mshindi wa tatu kwenye ligi.
 
Angalia Pesa aliyotumia kusajili, point alizoachwa na anayeongoza, makombe na timu zilizomtoa mwisho tofauti ya point na mshindi wa tatu kwenye ligi.

Okay, sasa kati ya man City na man united nani ameweka pesa nyingi zaidi kwenye usajili
 
Unatumia Paundi milioni 300 na ushee kusajili halafu unapaki bus!? Ni upuuzi.

Wadau wa Man U wana haki ya kulalamika.

Kama akitaka kutumia mfumo huo, asisajili wachezaji wa gharama. Hawa wa kawaida wanaweza ku fit tu.

Kwa mfumo huu wa MOU, NAMUONA SANCHEZ akiwa kama DI MARIA kipindi cha "wing back" za VAN GAAL..!

Pundi milioni 50 zilipotea tu sababu ya mfumo wa mtu mmoja. Pathetic!
 
Back
Top Bottom