Atakuwa anauza unga! Hawezi kuwa na pesa yote kwa muziki tu.
Huyu uwezo wake wa kufikiri umefikia tamati. ubongo wake umeaminishwa kwamba kila mwenye mafanikio ni drug dealer.
Msome maneno yake mwenyewe Chameleone ni haya:
Anakumbuka akiwa na Bebe Cool na Redsun alipata fursa ya kutumbuiza katika shindano la kumsaka Mrembo wa Kenya.
Anakiri hapo ndipo milango ya neema ilipoanza kufunguka. Anasema Dorotea, baada ya kuzoeana alimshawishi ahamie nyumbani kwake badala ya kuendelea kulala studio, ushawishi ambao ulimchukua zaidi ya wiki moja kumkubalia.
"Nilipohamia tulikuwa marafiki, lakini mengine yaliibuka tukiwa katika nyumba moja. Mara nyingi kila akitoka, alinikuta nimetulia naandika nyimbo, huku akihoji ni lini nitarekodi. Nilikosa jibu kwa kuwa siku wa na fedha.
"Siku moja akiwa safarini huko Afrika Magharibi aliniachia bahasha yenye dola za Kimarekani 1,000 (karibu Sh milioni 1.8 za Tanzania kwa sasa), akaniambia niingie studio.
"Huo ukawa mwanzo wa kibao Mama Mia na sikuamini kama fedha ile ingebadilisha maisha yangu na kunifikisha hapa nilipo. Mengine yanabaki kuwa historia," anasema.
Pamoja na utajiri aliovuna kupitia muziki, nyota huyo anasema historia ya kushuhudiwa `Live' na watu zaidi ya bilioni 9 akitumbuiza wakati wa Kombe la Dunia kwake ni kitu cha kipekee.
"Mtoto wa Afrika tena Afrika Mashariki kupewa heshima ile haikuwa kitu kidogo. Najiona mwenye bahati na ni mastaa wachache wanaweza kuingia katika kundi la bahati hata wangeishi kwa miaka 1000."
Anasema kutokana na baraka alizopata maishani, ameamua kuanzisha taasisi ya Chameleone ili aweze kuwasaidia wasiojiweza.
"Nikiwa mdogo sikuwa na maisha mazuri, sikutoka katika familia bora, kwa hiyo ninajiona mwenye wajibu wa kuwasaidia wengine wakianzia katika misingi mizuri ya kielimu. "Nimeshanunua eneo kwa ajili ya kujenga kituo.
Nataka jamii siku moja inikumbuke kwamba niliwika na kuitangaza nchi yangu, lakini pia sikuwa mchoyo, bali niliyatumia vyema matunda ya muziki.
Kwa kufanya hivi, naamini ipo siku nitawashawishi wengi kufanya mambo makubwa kwa ajili ya jamii wanayotoka."
Huyo ndiye Joseph Mayanja ambaye pamoja na misukosuko ya maisha tangu akiwa shule hadi sasa akiwa staa, bado nyota yake inang'ara.
Je, atazidi kupata mafanikio? Bila shaka ni jambo la kusubiri na kuona, hasa ikizingatiwa kuwa, mwenyewe amejijengea falsafa ya kutolewa sifa, bali kazi kwa kwenda mbele.
Pamoja na yote, Chameleone anapaswa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengi wa Kitanzania ambao huvuma kwa muda mfupi, lakini wakishazikamata fedha hupotelea kwenye ulimwengu wa anasa na baadaye kujikuta wakiwa `choka mbaya', tena wakiwa hawana akiba benki wala hawajawekeza.