Jorum nkumbi: mathematics ni lugha ya Mungu

Jorum nkumbi: mathematics ni lugha ya Mungu

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
22,854
Reaction score
32,657
Hisabati imenipa Fikra Tunduizi

“Mathematics is the universal dialect; where words fail, equations speak.”

Nikiwa kijana mdogo nilipenda sana Algebra, nilipenda Maumbo na sura zake, tangu zamani nikiwa shule ya Msingi na Sekondari niliona somo la hisabati likiwa na cheche za kuwasha fikra tunduizi, Wanafunzi wenzangu walinipa jina “Jonku Manamba” kwa vile wakati mwingi nilitumia kukokotoa milinganyo migumu ya hisabati na furaha yangu ilikuwa kupata jibu hatimaye. Mujarabu nilipofika Chuo Kikuu nilizama na kuvama kusoma kwa kina “Pure Mathematics na History of Mathematics” ndiposa nilirovywa rovurovu na kutebwereshwa tebwere na wanahisabati wakuu wa wakati wote, kulikuwa na wakati nilikaa chini nikatafakari:
Je, ni nini hasa huunganisha miujiza yote ya ulimwengu?
Je, ni lugha gani Mwenyezi Mungu alitumia kuumbia ulimwengu ?

“Mathematics is the language in which God has written the universe.”

Kutoka kwenye sayari na nyota angani hadi kwenye mfumo wa damu inayopita kwenye mishipa yetu, nilibaini kwa mantiki kuwa Hisabati inaunganisha ulimwengu.

Nikiwa kijana mdogo, sikuchagua Hisabati kwa sababu ilikuwa rahisi. La hasha. Nilivutiwa nayo kwa sababu ilikuwa ngumu, na ndani ya ugumu huo ndiposa akili yangu ilipata chakula. Nilitaka changamoto zinazotetemesha mawazo, nilihitaji kitu kitakachochochea ubongo kuhoji, kuchambua, na kufikiri kwa undani. Ndipo nikamkumbatia Malkia wa Sayansi Hisabati.

Hisabati haikuniimarisha tu darasani ilinilea kuwa mtafakari wa maisha. Nilipenda Mawazo ya Wanahisabati wakubwa wa wakati wote kama;
Galileo Galilei ambaye aliwahi kusema:

“Mathematics is the language in which God has written the universe.”

Nukuu hii si ya kufurahisha tu, bali ni ya kweli ya ajabu. Ukiitazama anga la juu, sayari zinazozunguka katika obiti zao, mwanga wa jua unaopasua giza, hadi miendo ya mawimbi ya bahari kila kitu kimeandikwa kwa lugha ya kihisabati.

Kupaa angani, kujenga roketi, kuelekeza setilaiti kwenye obiti, hadi kuchora ramani za dunia kwa teknolojia ya GPS, vyote hivyo haviwezekani bila Hisabati. Hakuna mawasiliano ya kisasa, hakuna uchumi wa kidijiti, wala ustaarabu wa kiteknolojia unaojengwa pasipo namba, kanuni, na mantiki yaani hisabati.

Nikapenda sana mawazo ya mwanahisabati mwingine
Albert Einstein aliyepata kusema Hisabati ni ushairi wa Fikra Safi yaani;

“Pure mathematics is, in its way, the poetry of logical ideas.”

Akaenda mbali zaidi kusema anataka kujua fikra za Mwenyezi Mungu kihisabati;

“I want to know God’s thoughts in mathematical way, I want to form an equation, not longer than one inch, that would explain the beauty, mystery, and power of the universe”.

Kisha akavumbua mlinganyo wa miujiza.

E = mc²

Na kwa kweli, kila mlinganyo ni beti ya shairi. Kila uthibitisho wa nadharia ni kiitikio cha muziki wa fikra. Wanafunzi wengi huogopa hisabati kwa sababu hawajaelekezwa kuisikia kama muziki wa akili, Wanafunzi wengi wanaona somo la Hisabati ni adhabu ya kiakili badala ya furaha ya kugundua mpangilio wa ulimwengu.

Ukitazama Mapiramidi ya Afrika utagundua miujiza ya Hisabati, Ukitazama kazi za Ramanujan, unagundua hisabati ni utukufu wa kiroho. Ukifuatilia kazi za Euclid, unajikuta katika dunia ya maumbo yenye ustaarabu wa kimaadili. Katika dunia ya Gauss na Euler, unajifunza kuwa ujenzi wa hoja ni kama kusuka shairi lenye kila kiitikio kikiwa na maana. Hili ndilo lililonivuta kama sumaku katika Hisabati si tu kuhesabu, bali kufikiri, kutafakari, na kuandika mashairi ya akili kwa njia ya mantiki.

Ulimwengu Bila Hisabati ni Giza totoro

Fikiria dunia isiyo na wahandisi, madaktari wa takwimu, wachumi, wanaanga, au mafundi wa kompyuta. Dunia hiyo ingekuwa kimya, ukimya wake ungetisha ajabu yaani bila maendeleo, bila mawasiliano, na bila mwelekeo. Hisabati ni dira. Ndugu huyu “Hisabati” Yeye ndiye anayeelekeza dira ya ukuaji wa taifa lolote.

Ndiyo maana mataifa kama:
1. China,
Imewekeza mabilioni katika elimu ya STEM (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati), na matokeo yake ni mabadiliko ya kiuchumi yaliyotegemea sana nguvu ya maarifa.

2. India,
inayotoa mamilioni ya wataalamu wa teknolojia duniani, imekuwa na historia ndefu ya heshima kwa wanafalsafa wa hisabati kama Ramanujan.

3. Israeli,
taifa lenye idadi ndogo ya watu lakini ubunifu mkubwa, linaongoza katika usalama wa kidijiti na teknolojia, kutokana na msingi wa elimu ya kisayansi na hisabati.

4. Marekani,
Nchi ya MIT, Caltech, na NASA ambapo uvumbuzi wa anga na teknolojia unategemea hisabati kwa asilimia kubwa.

Hitimisho

Leo hii, tunapozungumza juu ya safari za kwenda Mars au akili unde (AI), tunazungumza juu ya ushindi wa akili za wanahisabati. Ulimwengu mpya hautaongozwa na nguvu za kijeshi, bali na nguvu ya akili, akili iliyoimarishwa kwa namba, mantiki, na maono yaani Hisabati.

Hisabati ni mlinzi wa ustaarabu. Ni mwanga wa kutufikisha kwenye sayari za mbali, na daraja la kuunganisha watu wa tamaduni tofauti kwa lugha moja: lugha ya mantiki. Kama tunataka Afrika iinuke, basi tutangulize Hisabati mbele kama dira ya maendeleo.

Joramu Nkumbi
Mwanahisabati

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Sisi wazee wa hkl ni kilio tu
1749972465534.jpg


Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
the problem of many Tanzanians is that many of them dislike mathematics and the fewest who like it and perform well in this subject they dont know where to apply the knowledge of mathematics in different carreers. Tanzanian student should be taught that each topic they are studing is very useful in some careers ,this will boost their moral of studying this subject. for enxample student should be aware where they will apply the knowledge of algebra in their future academic careers.
 
Kwa kweli Hisabati ni muhimu katika nyanja mbalimbali za maisha, siyo tu katika sayansi na uhandisi bali pia katika biashara, kilimo, afya na hata kwenye maisha ya kawaida ya kila siku.
 
Back
Top Bottom