Kabla sijaenda mbali, je unaweza kuaccess kwa kutumia username hiyohiyo na password tokea front end? Je unatumia joomla version ipi??
Kama unaweza kuacess, basi inawezekana kuna extension (imeharibu permission) hivyo umepoteza uhalisia wako kama admin, hivyo nenda kwenye database na uhakikishe user ID ipo kwenye admin group.
Kama hauwezi kuacces hata kwa front end, basi inawezekana user table imecorrupt au kufutwa, inaweza kusababishwa na kivamiwa au extensions zisizotengenezwa vyema. Hivyo unatakiwa kuirecover tokea kwenye backup kama table nzima imefutwa au kama sio basi nenda hatua ya chini.
Kama umesahau password ya admin au admin akaunti imefutwa basi fanya hivi.
(Kwa joomla 2.5) nenda front end na usajili akaunti yoyote (kumbuka username na password), halafu nenda kwenye configuration.php na chini kabisa andika
public $root_user='myname'; ambapo myname ni jina la hiyo akaunti mpya.
Baada ya hapo, login na ukabadilishe password ya admin na kufuta huo mstari wa juu kwenye configuratio.php . Kumbuka kuangalia logs files kwa chanzo.
Nimeanza mafundisho ya joomla ambayo yatapatikana kwenye AfroIT.com na pia
https://www.youtube.com/watch?v=6tv8j6mX6vA nadhani itawasaida wengi.