Jongoo ana nini mpaka wanawake mumuogope?

jongoo akikupandia unawashwa kweli me siwapendi ila joka na panya nikikutana nao naweza zimia
 
Yaani umenikumbusha mbali....kuna mama mmoja anaogopa jongoo siwezi hata kuelezea........
Yeye hata ukitamka tu jongoo anapiga kelele mpaka majirani wanajaa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119]
 
huwa wanatisha hivi hasa wawe wale wanene. kuna siku nilipita chini ya muembe akanidondokea mmoja begani uuuwi siwez kusahau, mpaka kesho sipiti wala kusimama chini ya muembe
 
Had ww unaogopa panya na ujanja wote huo[emoji23]
kuna siku namkimbia panya jikoni nikakimbilia kwenye kona na kuna meza si akapanda na meza then mwili wangu nilijikojolea kwa woga kitu cha sekunde moja haloo sina hamu na huyu mdudu... akiingia ndani naweza mpisha kwa kweli
 
Jongoo ana chemical anayo itoa inaitwa hydrogen cynide.... Utafit wang utaanzia kam hii chemical ipo kweny manii. Hapa c kuna watu wanasem jongoo =dushe. Ndiomana nimejarib ingia ndan kidogo
 
Jongoo ana sumu inayoitwa cyanide ni hatari kama ukiila(ingest)... Anatumia kemikali hio kujilinda na wanaomla (predators kama ndege na baadhi ya wanyama)
Jongoo wengi wana rangi za onyo (aposematic colouration) mara nyingi ni nyeusi na rangi zingine mng'ao kama nyekundu na njano(hapo kwenye picha tunaona ni nyeusi na miguu mekundu) .... Rangi hizo huonya adui wa jongoo kama ndege na wengineo (ni kama kusema nione na kaa mbali na mimi, mi sifai kuliwa nina sumu kali)... Jongoo wengi wakiguswa hujifanya umbo la mviringo (kujilinda) au kujitupa(kwa kuzunguka kwa kasi kama nyoka) hapo uiga nyoka (mimicry) yote ni kujilinda na anayeweza kua adui... Kuna mnyama mmoja anapenda sana kula jongoo... Tunamuita fungo (civet),huyu mwili wake unaweza kuchakata sumu ya jongoo isimdhuru.
NB:kama sio mtaalam wadudu epuka kugusa wadudu wenye rangi za mng'ao...hasa mchanganyiko wa nyeusi, nyeupe, nyekundu au njano Wengi wao wanasumu(chemicals za majimaji) inayoweza kutoa malengelenge au kuunguza ngozi. Japo kuna wadudu wanatumia hizo rangi kudanganya wana sumu (mimicry)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…