Jongoo ana nini mpaka wanawake mumuogope?

Jongoo ana nini mpaka wanawake mumuogope?

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,077
Reaction score
17,260
Jongoo ni mdudu mdogo sana ambaye anaogopwa na jopo kubwa kabisa la wanawake,
Hii inafika mbali zaidi mpaka unakuta wanawake wanatoka nduki huku wakisasambua nguo zao, wengine hujikuta wanaruka Kung-Fu Panda bila kutegemea huku wakituachia TV ya bureee eti kisa wamekaona kajijongoo kanapita karibu yao!

Kitu kilichonifanya mpaka nishangae unakuta wengi ukiwauliza wanadai eti huwa wanamuogopa jongoo sana tena kuliko nyoka,
Umeona balaa hilo? Yani eti nyoka mwenye sumu kwao ni bwege tu, lakini akiona jongoo atapiga yowe utadhani U.S.A ameona mabomu ya Korea Kaskazini.!

Sasa wanawake inabidi mje mtuambie kipi kinachofanya mpaka mumuogope kiasi hiko?
 
Bora wao jongoo haonekani mara nyingi, wengine tunataman paka wapotee duniani maana tunaogopa kupita kiasi
sasa kwanini mnawaogopa kupita kiasi? Kwanini?
 
Yaani umenikumbusha mbali....kuna mama mmoja anaogopa jongoo siwezi hata kuelezea........
Yeye hata ukitamka tu jongoo anapiga kelele mpaka majirani wanajaa
 
Simpendiiiiii..mtu akinitishia ilo dudu sisemezan nae maana huwa naweweseka had usiku. Yaan likijikunjaa mara litembee mwili wangu unasisimka woga. Naandika huku nimekunja midomo umemtajia ninnn
 
Sijawahi kumuogopa jongoo kwakweli.
Ila kitu nyoka na ile mijusi wakati fulani unaezaikuta ndani (kwa baadhi ya nyumba zetu flan)
Doohntaenda lala kwa jirani
 
Yaani sijui kwanini akikugusa unaweza hata zimia, nina rafiki yangu ukimuekea jongoo mbele yake chochote utachomuambia anakubali...sijui kwann tunaogopa kiasi hiki
Nipe namba ya rafiki yako na mimi ninafuga majongoo mengi sana. Ili nione kama kweli nitakachomwambia atakubali.
 
Back
Top Bottom