Jonas Mkude na mashabiki wa Simba wapata ajali, shabiki mmoja afariki

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Gari walilokuwa wakisafiria baadhi ya wachezaji na mashabiki wa klabu ya Simba akiwemo nahodha wa kalabu hiyo Jonas Mkude limepinduka maeneo ya Dumila mkoani Morogoro
baada ya tairi ya gari ya nyuma kupasuka.

walipokuwa njiani kutokea Dodoma

Shabiki mmoja mwanamke aliyejulikana kwa jina la Shose amefariki baada ya kupata majeraha makubwa. Jonas Mkude alipata majeraha madogo sana na yupo salama, majeruhi wengine wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo wamewahishwa kwenye hospital ya Morogoro.
Jonas mkude na wachezaji wengine waliokiwa kwenye gari lingine walikuwa wanaiwahi kambi ya timu ya Taifa.

Klabu ya Simba inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki no wapenzi wote wa klabu ya Simba.

Klabu ya Simba inaendelea kuwasiliana na ndugu wa marehemu kwa ajili ya kushirikiana katika msiba mzito kwa klabu nzima ya Simba kwa kumpoteza Shabiki wake mkubwa ambaye alikuja Dodoma kuisapoti timu yake pendwa ya Simba katika kuchukua ubingwa.


c39c21efec69080c0630533b2b24bf79.jpg
0b2efb4387d2d6194cd2bc649a466823.jpg
f0b7e51cdffb333a1792ed593e1ab494.jpg
7d494d475bddc1ac8e982fe3ff4e9940.jpg
 
Pole mtani wa jadi,japo jana mlichakachua ushindi dhidi ya Mbao...ili mpunguze kulia lia..na kulilia point za bure kule Fifa...
Mola awafanyie wepesi...
 

Nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba Mkude hakugambeka jana na kwamba hata leo hakuamka na Gambe kama kawaida yake. Haya Masela wa Gambe wa Mango Garden akina Dula na Side Kiumbe Dogo yenu Mkude mliyomfundisha Kugambeka yamemkuta.

Nawaombea tu wote waliopata Ajali wapate nafuu haraka na lolote baya zaidi lisitokee ila binafsi sikuona kabisa sababu ya wao kuwa na mwendo kasi eti kwa Kisingizio cha kuwahi Kambi ya National Team halafu badala yake unaishia tu kuwa Majeruhi au Kilema hivi.
 
Dah nakumbuka zamani mechi ya Simba na Yanga lazima mchezaji au kiongozi wa zamani afe.
 
Back
Top Bottom