Jokate Kidoti amwaga misaada kwa watoto yatima

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
JOKATE.jpg

Dar es Salaam. Mwanamitindo Jokate Mwegelo leo Ijumaa ametoa zawadi za Eid katika kituo cha yatima na wajane cha Ahbaabul Khairiya kilichopo Mwananyamala B, jijini Dar es Salaam.

Katika zawadi hizo Jokate alitoa mchele kilo 250, unga kilo 250, mafuta ya kupikia, mbuzi wawili na nguzo za watoto na wanawake.

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo, Jokate ambaye mwaka 2006 alishika nafasi ya pili katika Shindano la Miss Tanzania, amesema ameguswa kuwasaidia watu wenye uhitaji ili nao washerehekee Sikukuu ya Eid kwa furaha.

"Nikiwa kama mwanajamii nimeguswa na watoto hawa na akina mama nikaona si vibaya nikajikusanya na kutoa kidogo nilichonacho ili nao wafurahie sikukuu."

Mkuu wa kituo hicho, Ahmed Shebe ameshukuru kwa msaada huo na kuwataka wasanii wengine kuiga mfano huo.

"Ukiwasaidia wasiokuwa na uwezo Mungu anakuongezea maradufu, niwasihi wasanii kujitoa kwa ajili ya wanajamii na si kufanya matendo na matumizi ya anasa,"amesema Shebe.

Chanzo: Mwananchi
 

middle east

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
1,205
2,000
Huyu Dada atafute mume wa ndoa ...alidharauliwa sana na yake matamshi ya mama kariakoo na mwanae ....
 

Didas Nbc

JF-Expert Member
Sep 21, 2014
470
500
Kampeni zimekatazwa hadi 2020 ...yeye kaamua kutoka kivinge.....aya bhana "hurusiwi kuongea ukiwa unakula"
 

TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
1,275
2,000
Angalia vizuri sura yake mkuu. Si wa kukaa na mme huyo.

Chunguza kwa kina sana sura yake itakupa tafsili halisi ya tabia yake.
Much know;,,mwanamke akiwa na tabia iyo ni mtihani kukaa nae,, ila wanakuwaga mafaita kwenye kusaka pesa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom