Johnny Mad Dog movie

Genecandy

JF-Expert Member
Dec 13, 2017
277
500
Heshima yenu wakuu

Niende moja kwa moja kwenye mada wapenda movie nawaomba hapa; nilikuwa ndani ya gari naenda mkoani ndo nikakutana na hii movie ya JOHNNY MAD DOG

Sijawahi kuiona ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza ila nilipoaingalia ikanisisimua sana jinsi vijana wa Kiafrika walivyouvaa uhusika sio siri ni movie ilonisikitisha sana.

Swali langu ni hili naomba kujua kama story ya hii movie ni kweli? Na kama ni kweli ilikuwaje mpka vijana wakaingia mtaani? Na je, nchi haikuwa na jeshi mana ni vijana wadogo na wachache tu lkn walifanya mambo ya kutisha; mana naona mpka jeshi la UN wamo ndani na hawafanyi chochote.

Na vipi kuhusu casting wa hii movie nikiangalia wanaonekana bado vijana wadogo sana mana kama 2008 wako hivyo inamaana kwa sasa hawazidi Miaka 30 kwa jinsi walivyouvaa uhusika naiman huko kwao liberia ni vijana maarufu sana!!kwa anayefahamu japo kdgo kuwahusu anijuze.

Mwisho scene ilonisikitisha ni ile ya kale kajamaa cjui ndo ka Johnny kenyewe kalokuwa ka dereva kalivyosababisha kifo cha yule binti kilimla afu baade kikawa na demu mwingine cjui kale kabinti kakajipiga shaba .

Ila hii movie imenikumbusha matukio ya msumbiji kabla Alshababy hawajafikia hatua walofikia kwa sasa ilianza hvyo hvyo vijana wadogo wanaingia kijijini wanachoma nyumba na kuanza kuchinja watu mpka wakaja kujizatiti wakawa kikundi kukibwa chenye masilaha ya kutosha dah MUNGU IBARIKI AFRICA.

Samahanini kwa gazeti ila naomba wajuvi mje jmn wengine Google sio yetu ki malkia hakipandi jmn tusaidiane wandugu!
 

Genecandy

JF-Expert Member
Dec 13, 2017
277
500
ooh xo hawatakiwi kujibizana nao?sasa jeshi la serikali lilikuwa wapi mana naona kama walisambaratisha mitaa watu wakawa wakimbizi !!
Wanajeshi wale hawako kivita bali Ni walinda àmani.ndio maana wale machalii walivyofika pale wale wanajeshi walifanya tu kuwatuliza huku wakijihami.
 

Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
3,926
2,000
Ni film Bora kwa kweli kwa kipindi hiko, ingawa matukio mengine yametengenezwa ili kunogesha lakini Ni kisa Cha kweli kabisa kilicho wahi kutokea huko Liberia miaka 2002 katika Vita ya wenyewe kwa wenywe.
Ilio zaa vikundi vya wapiganaji vilivyoshindwa kudhibitiwa na serikali baada ya serikali kuwa corrupt.
 

Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
3,926
2,000
Mwisho scene ilonisikitisha ni ile ya kale kajamaa cjui ndo ka Johnny kenyewe kalokuwa ka dereva kalivyosababisha kifo cha yule binti kilimla afu baade kikawa na demu mwingine cjui kale kabinti kakajipiga shaba .

Vikukundi vyote vya kijeshi haswa vya uasi hufanya Sana mambo ya ubakaji.
Lakini Kama ilivyo kwa mwanadamu kuwa na moyo wake mapenzi ndivyo ivyo kua kwa huyu kijana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom