John Tendwa kwenye dk45 ITV

Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema haoni sababu zozote za msingi za maandamano ya CHADEMA.

"unaposema utaandamana kutoka Arusha hadi Mtwara, unamkomna nani? Ni vema ukatafuta utaratibu mwingine wa kutatua matatizo badala ya kuandamana"

Tendwa alitoa kauli hiyo alipokuwa akifanya interview ktkt kipindi cha DAKIKA 45 cha ITV saa tatu leo usiku.

Tendwa ametishia pia kukifuta chama chochote cha siasa kinachoendeleza kampeni wakati uchaguzi umekwisha.

Akitoa maelezo alisema
"ukishindwa uchaguzi unajipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao. Taratibu zinasema unajipanga na sio unafanya kampeni."

Akaongeza,
"sio unatoka bungeni unaenda kuwaambia wananchi, sisi ni wachache kuliko CCM kakini hawatushindi hoja. Sisi tunatoa hoja za kuomba mwongozo kuliko CCM, kwa hiyo uchaguzi ujao mtuchague sisi" aliongeza Tendwa bila kusema wazi anakilenga chama gani.

Ktk kuonesha mamlaka aliyonayo amesema hatasita kukifuta chama chochote kitakachokiuka taratibu.

Alipoulizwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Selemani Semunyu kuwa jeuri hiyo ameitoa wapi alijibu,
"mamlaka ninayo, sio jeuri ni mamlaka."

SOURCE:ITV

Tendwa ama anaugua amnesia au ni msanii wa viwango vya kipekee. Mara kadhaa amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa maandamano ni haki ya msingi wa vyama vya siasa. Sasa anatishia nini hapa? Nani kamtuma Tendwa kutishia watu? Na ubavu gani huyu babu kama si kujependekeza?
Na kama kweli ni mwanaume afute 'hicho' chama, afute tuone!

Hamna jipya.yupo kimagamba zaidi nimemfuatilia mpaka mwisho mambo machache sn kayaweka sawa lakini maandamano ya chadema kachemka.anaonyesha kabisg anavutia upande fulani.nahic atakua analinda kibarua chake

Muandaji au uulizaji maswali wa huyu ndugu wa ITV bado unahitaji maberosho. Kuna namna unaweza kuweka swali na mtu akakupa jibu la ndani kabisa bila kujijua. Lakini kwa mtindo huu wa sasa ni vigumu mtu kama Tendwa kusema kile kilochoko moyoni kwake kwa sababu nyingi tu ikiwemo ajira yake. Tukumbuke gabbage in gabbage out! Usitegee jibu la maana kama swali lenyewe ni legelege.
Hiki kipindi hakina msisimko kwa sababu ya maswali anayouliza muongozaji, hawezi kuuliza maswali chokonozi,abadilishwe!

Tendwa ama anaugua amnesia au ni msanii wa viwango vya kipekee. Mara kadhaa amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa maandamano ni haki ya msingi wa vyama vya siasa. Sasa anatishia nini hapa? Nani kamtuma Tendwa kutishia watu? Na ubavu gani huyu babu kama si kujependekeza?

Na kama kweli ni mwanaume afute 'hicho' chama, afute tuone!

Mkuu,
huyu mzee ni msanii sana, tena muhuni na ni sharobaro wa kufa mtu.

Binafsi nimeshindwa kuelewa ameenda studio kama msajili wa vyama vya siasa, au kama msajili wa wanachama wa ccm?

Nani asiyemjua tendwa, huyo ni mteule wa ccm lazima alinde maslahi ya chama na kwa kuwa maandamano ya chadema yanatishia uhai wa chama chake lazima ayaponde.

Wakuu huku kwetu umeme imekua bidhaa adimu tangia tumng'oe mramba kwahiyo mtujuze anachosungumzia

tena selasini aliongelea hiyo ishu kwa machungu sana. Vuteni subira

Kaulizwa swali kwanini vyama vya upinzani vikiandamana ndio waopigwa na kuonekana wabaya lakini ccm wanapata baraka zote eti anajibu ccm wanafuata utaratibu nimemshangaa sana nikaamini magamba wameiteka nchii

nlizan ni mi2 kumbe nawe umemuona furuu kiCCM mpk nachefuka roho

Maneno ambayo amezungumza sikumshangaa.huyo ni mwana CCM. Usishangae ukisikia 2015 anachukua fomu kugombea ubunge kupitia CCM hata kama umri umemtupa mkono. Huyo mtangazaji hana uwezo wa kuendesha hicho kipindi ama atakua anayo maelekezo maalumu toka kwa mwenye tv stesheni asiulize maswali magumu,si unajua naye ni mwana magamba!

Jamani yale ya nape sio kampeni za uchaguzi? Huyu tendwa katendwa na ccm "robotized" change will come. Mzee anaongea yale aliotumwa na mwanasheria wao. Hivi inakuaje wewe uliyetedwa unavutia upande wa uongozi wa mafisadi wananchi tunakuelewaje? Mtendwa umeteleza.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom