John Mrema hufai kuwa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Mrema hufai kuwa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gwota, Jul 2, 2011.

 1. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Imekuwa ni kawaida kwa wabunge na viongozi wengine wa chadema kuwa karibu sana na wananchi na kuwatetea mahala husika, Hali hii ni tofauti kabisha kwa huyu mkurugenzi wa halmashauri ya bunge John Mrema, Kwa zaidi ya mara tatu nimekuwa nikimpigia simu na kumuandikia sms ashiriki katika ufunguzi wa tawi la chadema mahala ninapoishi ila kila anavyopokea simu na kusikiliza ninachomwambia juu ya mm kumtaka awe miongoni mwa watakaokuja kuzindua anasema yupo busy nimpigie badae na sms hajibu, Nashangaa anavyojifanya busy kumshinda hata Mbowe au slaa ambao ukiwapigia simu ukawaelezea shida yako ya kukiendeleza chama wanakusikiliza na kukusaidia na km kwa muda huo wapo busy wanakipigia badae,

  Ombi langu kwa uongozi wa juu wa chama:
  • Watu kama hawa muwachukulie hatua mathubuti kwani wanazuia maendeleo ya chama kwa makusudi na wanatukera sana sisi wanachama tuliopo ngazi za chini tunaojaribu kufanya utekelezaji wa kukiimarisha chama kutoka ngazi ya msingi na tawi sehemu sehemu zilizo muhimu zaidi.
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Chasema?
   
 3. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,609
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Naona ni spelling mistake,lakini kaeleweka....
   
 4. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,609
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkuu kama ni hivyo basi waambie hao wakubwa wake wakina mbowe na slaa ndio waje kwanza wanaweza kukataa???
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,345
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  eee! lakini jamani na wewe utakuta pengine kulikuwa na watu wengine ungeweza kuwaomba kushriki shughuli hiyo.........angechangia lema mwenyewe tungepata picha kamili haya mambo mengine ya mtu kuamka na kumwandika mtu direct bila kujua kuwa wewe ni nani na unawakilisha nani na upo kitongoji au kata gani yanaweza kutuvuruga sana.....unaweza ukawa unasema ukweli ila pia walio makini hawawezi kuchangia na kujadili mtu binafsi kirahisi hivyo vinginevyo naamnini falsafa ya chadema ni zaidi ya magamba yaani ungewasilisha sehemu husika ili lifanyiwe kazi badala ya kusema tu viongozi wa juu wamchukulie hatua..............
  "TO ME THE POST IS TOO BLIND TO BE DISCUSSED"
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe mwenyewe huwezi kulizindua au ujiamini.

  Tengaza Posho hapo kwa ajili yake kuja na kuzindua kama ujasikia anakuja siku ya pili tu
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Kwani wewe unamtaka John Mrema au unataka tawi la CDM? Wewe watafute CDM wenzako mfungue ili tawi lenu
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  umeuambia uongozi kabla huja leta hapa, maana kama viongozi mtakuwa mna kimbilia JF kushitaki au kulalamika sijui kama tutafika.. viongozi type ya John Mrema hawafai kwani wao hufikilia kuwa uongozi ni mapozi...
   
 9. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Gwota, Got it wrong because he aired his complaints on this forum instead of channelling his views directly through party machinery.Let me hope kwamba amepeleka malalamishi kule,kama hajafanya hivyo next time inabidi afanye hivyo ili kuimarisha flow of information,kuwajibishana na nidhamu ya kweli katika chama ambacho kina jukumu la kutoa taswira ya wajibu na nidhamu katika kuiwajibisha serikali iliyopo madarakani.Kama chadema ingekuwa MNC ( Mult-national Company) basi Gwota ungekuwa umevunja mojawapo ya Corporate values! you could be in trouble.

  However,We should employ political tolerance in this era of multi-political democratic landscape.Mleta hoja Hajafanya kosa kubwa sana,kwa hiyo tusimlaumu mleta hoja badala yake tuonyeshe tolerance kwa kujadili hoja aliyoileta.Kama muhusika anapita huku naye kwa umakini wake wa kisiasa,kwa utashi na unyofu wa moyo wake na kwa nidhamu ya kutumikia jukumu alilo nalo basi atalifanyia kazi hili kwa uaminifu na au hata kujirekebisha

  Tuwe tayari kupokea changamoto na kuzifanyia uatuzi kwa kiwango husika na kinachostahili,ni wakati wa kuonyesha kwamba tuko tayari kujisahihisha.Sidhani kama wapenzi na wafuasi wa chama chochote cha siasa kinachojua kwamba CCM imefika hapa ilipo kutokana na kuwa kiziwi au kiburi cha kutowasikiliza wananchi,wanachama na wafuasi wake kitasita kuyafanyaia kazi malalamishi,mawazo,maoni na au hata kuchukua hatua za kinidhamu katika kuwajibishana ili tutoe taswira tofauti na ile iliyozoeleka.

  Kwa hiyo ni bora kujadili hoja za mleta hoja,ingawa siungi mkono mantiki ya kukimbilia JF au kwenye media kabla ya kupeleka hoja zako kwenye vyombo husika,na vilevile hatuwezi kuwa vipofu au kufumbia hoja ati kwa sababu imetolewa in a wrong platform.Hii ni social-political forum,Motto wa JF pengine umemsukuma kuinbgia hapa na kusema aliyosema ila asiutumie uhuru huo vibaya pia.Afikirie maslahi ya wengi zaidi(kupitia chama kwa maslahi mapana)

  So,It is my humble request that,People have the right to free speech, and yes, even the right to be offensive. I don't condone filthy talk but at least let's not turn here into a freaking circus. It'll just be like turning yourself into a laughing stock
   
 10. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ben,

  Una lako, ndio nimesema unalako unaki-nyongo. Muda uliotumia kuandika hio makala yako na hoja hii hapa havilingani. Kwanini wewe kwa akili ndogo hujui hiki ni kipindi cha bunge na yeye ndo muda wake wa kuperform? kumbe ndo maana ulijitoa kuunganisha nguvu?

  Samahani lakini kama nakubore. Uzuri huku kwetu Kahama tunasomea humu-humu ila nyie waDar mnajuana vizuri, so nimeelewa hivo na ku-hukumu hivo.
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Selous,
  Asante uko sahihi/pengine hauko sahihi.Hujani-bore kabisa.you are free to express whatever you feel......Na hilio ndilo ninalopigania always hakli yako ya kusema,haki ya kutoa maoni ,haki ya kunikosoa ili nijisahihishe niweze ku-fit katika society na Tanzania ijayo(Kanaan)

  Muda wa kuandika makala ndefu?duh...muda wa bunge? si umuulize mleta hoja ni lini alimpigia,au kumwita?hata mimi sijamuuliza..so ndiyo maana nikamuelekeza kwamba alistahili kufuata proper channels za chama,pengine angeeleweshwa na asingekuja huku JF.Kuhusu makala ndefu hailingani na hoja,what do you mean?ukubwa wa hoja aliyeleta mhusika inategemeana na jinsi msomaji alivyoona,wewe utaona ni ndogo hoja yake but mimi naweza kuiona kubwa au ndogo lakini nikajibu katika picha pana ili kusaidiana na kujengana ...Rafiki wa kweli ni yule mwenye kukueleza ukweli bila hofu.Sisi ni tofauti na CCM kwenye mkusanyiko wa watu wenye hofu,na ukondoo.what makes a party revolutionary,change oriented is boldness,braveness and Tolerance.Kuhusu kujitoa hiyo ni ajenda nyingine,ila jinsi ulivyoileta hapa inafurahisha kwali.Again sitaki kucheka coz it might be offensive kwa mtu mwingine/wengine!loh

  But sijaona kibaya katika niliyosema,na labda ukirudia kusoma maelezo yangu utakuja na comment tofauti.Kwa akili Ndogo? anyaway,just exercise your freedom of speech....(just use your mighty brain to re-read and comprehend the contents of my post).the bottomline is,This is a forum and it may belong to an individual but its strength lies in the collectivity of its users.Thank you
   
 12. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nadhani hapa kuna hoja nzito, ingawa Gwota kaileta jamvini hivyo kuonekana hajafuata utaratibu.
  Kwa upande mwingine namuunga mkono sana Gwota kwamba wapo viongozi ndani ya CDM wana mapungufu makubwa sana, hasa kwa mfano uliotolewa na Gwota. sina uhakika na tuhuma zinazoelekezwa kwa John Mrema kwa sababu binafsi sijawahi kuwasiliana naye.
  Viongozi wa CDM lazima watambue sasa kwamba priority ya chama ni kuwa na wanachama wengi na matawi mengi kwa kadri inavyowezekana, wapo watu wengi wa aina ya Gwota ambao wanajitahidi kufikia malengo hayo na ni jukumu la CDM makao makuu kuwapa support.
  Pale makao makuu kuna watu wengi ambao ni well known kwenye jamii, ilikuwa ni jukumu la John Mrema kama aliona hana nafasi angetafuta mtu wa kumwakilisha ili lengo la kufungua tawi likamilike.
   
 13. Miss Parliament

  Miss Parliament Senior Member

  #13
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 27, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ben,
  Umeandika maelezo mazuri na msimamo wako umeweka wazi.hoja ulizoandika zinashawishi kwa kiasi kikubwa na zinaonekana ila inaonekana unatumia spinning na propaganda tamu sana unapokabilaina na adui zako.hofu yangu usijekuta ile kauli iliyokuwa inasemwa hapa JF kwamba wewe ni mtaalamu wa kulipa visasi kama Jk ina ukweli.Najua John Mrema aliungana katika kuwaengua kwenye uchaguzi.tafadhali usikubali kuwa kambi zao wanaotaka kuwania uenyekiti na urais 2015.mtaumiza wengi
   
 14. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ben,

  Asante kwa para ya kwanza na majibu kwa ujumla. ila nimependa hayo maneno ya para ya kwanza.

  Usicheke wala usishangae hapo kwenye nguvu ila niliumizwa sana cos sikutegemea na najaribu kukusoma positively mpaka leo sielewi but time will tell. You don have to defend your action but just leave it. One day will prove something but i was disappointed. thanks and off.

  Umeandika mengine ambayo kwa kujua unachoandika ni rahisi na pia bora ungejikita kumdadisi huyu bwana ili picha iwe clear. Kwa mtazamo wangu nasikia huyu bwana ni director wa halmashauri na bunge. Na kwa jinsi niavyoona the man is now very busy unless otherwise. Leo unamuita akafungue tawi. does it make sense wewe Ben??? kama sio uchuro na wewe unaruhusu huu ujinga bala hata ya kujiuliza huyu jamaa anamtafutia nini Mream? please Ben, saa nyingine watu wajue hata kufikiri ili jamaa asaidie kule bungeni. i supported you kwenye kugombea uenyekiti simply najua you have been exposed na niliamini kukaa hapa jamvini unajua nini kinatakiwa.

  Inawezekana Mrema hayupo Dodoma lakini but huu ndo mtazamo wangu kuwa ajikite dom kwani kuna hotuba nyingine zinatakiwa na haziwezi kundikwa na mtu mmoja hata kama ni kipanga namna gani.

  Hayo tu kaka.
   
 15. Miss Parliament

  Miss Parliament Senior Member

  #15
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 27, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ben,

  jiandae na jimbo lako,nimepata fununu unataka kugombea jimbo moja hapa dar es Salaam na kuna mbunge mmoja(CCM) jana kwenye vinywaji tu kasema anakuwekea mikakati.waache wanaoutaka urais au uenyekiti taifa waendeleee wewe jipange na jimbo lako.Achani uhuni,ushenzi wenu mnaofanya!Mwenzenu jeuri ya hela za madini ndizo anazotumia kukataa posho na kufadhili kwa hali na mali makundi ndani ya chama.Najua mmedhamiria kuwashughulikia wote waliowawekea mizengwe kwa njia zote,uhuni wenu wa kisiasa hautafanikiwa.itafikia mahala mtaungana mkagombee urais huko NCCR si mlishamtanguliza kafulila?jeuri yenu ya Elimu isitumike vibaya kulipa kisasi kwa wabaya wenu
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nilishawahi kukuambia hapa JF mara nyingi,sina kundi sijui kundi lolote.Labda wewe una taarifa zaidi.Kuuhusu Ubunge sijui nini,hiyo ni ajenda nyingine.Mwambie huyo mbunge wa CCM namtakia kila la kheri...ni haki yake kuweka mikakati ya kisiasa,sasa unataka asiweke? Hayo mengine unayosema sijui kambi,kafulila mara NCCR naona ni muendelezo wa matusi tu.Ukisoma ila hadithi ya visingizio vya mbwa Mwitu kujenga hoja ya kuahalalalisha yeye kumla mwanakondoo utaelewa ninachosema

  Halafu hayo maneno uliyotumia hapo kwenye Red,too low noow!

  I have noticed a very disturbing pattern. Why is it when a an argument is being lost we result to abusive words or when someone has any opinion different from ours we insult them or shout them down. What happened to freedom of expression. It is this attitude of wanting to hear what suits us that breeds sycophants and makes our leaders lie to us. How exactly are we going to grow as a nation if the enlighten ones do not have basic respect other peoples opinion. This basic respect is the hallmark of civilised society

  Let us decided on this forum not to dignify insults with any response no matter how tempting it might be
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hebu tupe maelezo kidogo ya huyo anaeongelewa kwenye Blue

  Hapo kwenye red hapana bishosti. Matusi ya nini?
   
 18. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jaribu kupeleka malalamiko sehemu nyingine na kuona jinsi gani kuna mkakati muhimu wa CHADEMA
   
 19. Miss Parliament

  Miss Parliament Senior Member

  #19
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 27, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nani asiyejua ni Zitto?
  watu wanatumia taaluma zao na ushawishi kujenga makundi na kujiimarisha zaidi.sijamtukana,Ben kama nimekukosea nisamehe lakini ushawishi na taaluma yako usiitumie.inaonekana wewe ni kundi la akina zitto,kitila na akina ndesamburo.wewe ni kijana mdogo acha kiu ya kulipa visasai hata kama unaona umeonewa.
   
 20. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Got lost!!!! What is the discussion about?
   
Loading...