Zito na wapambe wake wanapaswa kulielewa hili kuhusu uendeshaji wa chama cha siasa.
Uendeshaji wa chama cha siasa una changamoto nyingi. Kikubwa ni uongozi bora na fedha. Vyote viwili vinachangia kukuza na kuimarisha chama.
Uongozi uko namna mbili kuna wale wnaokiuza chama kutokana na mvuto wao kwa umma (wafuasi) kama vile kuwa wazungumzaji wazuri majukwaani (yaani fiery/eloquent speakers), haiba zao (charisma) nk. Katika CDM watu hawa ni kama Zitto, Dr Slaa, Lema, Tundu Lissu, Wenje nk.
Aina nyingine ya viongozi ni wale wenye kuchangia akili (brain power) katika CDM kama vile Tundu Lissu, Prof Safariegu - nk. Ingawa Lissu yuko pande zote mbili.
Lakini hata kama chama kina viongozi lukuki wa namna hii ni bure bila kuwapo pesa kuendesha chama (logistics).
NCCR-Mageuzi ilipoteza umaarufu wake kutokana na kutokuwa na pesa kuendesha ingawa chama kilikuwa na watu wenye mvuto na haiba (charisma) kama vile Mrema, Lamwai etc. Serikali ya chama tawala iligundua hilo kwani NCCR ilikuwa inategemea ruzuku tu kutoka serikalini na serikali ikaona hapo ndipo pa kukinyongea chama maana bila fedha chama hakiwezi kwenda mbele.
Serikali ikachochea vikundi viwili kuibuka ndani ya chama hicho (Cha Mrema na cha Marando) na kuvipambanisha kwamab kipi kina haki ya kupokea ruzuku kwa kuwa na Trustees wanakubalika. Serikali ikaamuwa kukiona kikundi cha Marando ndiyo halali kupata ruzuku.
Katika Chadema serikali ya CCM imeshindwa kuisambaratisha Chadema kwa njia ya fedha, kwani imegundua CDM ina vyanzo vingine vya kupata fedha kuendesha chama.
Na hili wengi katika Chadema hawalijui -- yaani fedha tena kwa mabilioni. Angalia kampeni za chaguzi ndogo zilizofanyika mahelikopta nk -- vitu ambavyo kimekiwezesha chama hicho kuchuana vikali na CCM yenye pesa zilizo katika ncha za vidole wakati wowote (ni ku-snap fingers only!). Swali nani anagharamia fedha hizi katika CDM? Ni ile ruzuku pekee kutoka serikalini? Kweli wengi wanashindwa kujiuliza hili.
Hata Zito mwenyewe bila shaka analifahamu hili kama yuko honest with himself.
Tuangalie viongozi wakuu wa CDM na waasisi. CDM ina bahati (kuliko ilivyokuwa NCCR au hata CUF) kuwa na viongozi wakuu ambao ni mabilionea -- naweza kusema hawa ni Mzee Mtei, Ndesamburo, na Mbowe mwenyewe.
Na katika hao Mbowe (mwenyekiti) ndiyo kiungo muhimu (vital coordinator) anayeaminika na hao wengine wawili katika ku-channel funds za kuendesha chama. Kwanza nasikia kuna uhusiano wa kifamilia baina ya Mbowe na Ndesamburo (au Mbowe na Mtei? Sifahamu vizuri).
Sasa basi wafuasi wa Chadema wenye kuchambua mambo wataona kwamba Mbowe kuwa mwenyekiti wa CDM ni kitu muafaka haswa, hasa wakati huu ambapo chama kinajijenga.
Ninavyosikia ni kwamba kama kunatokea haja ya fedha kwea ajili ya shughuli fulani ya haraka ya chama, kama vile helikopta nk katika kukamilisha mkutano fulani wa hadhara au wa kampeni Mbowe ndiyo hutoa hayo maombi kwa akina Mtei na Ndesamburo) na hapo mara moja vitu hivyo vinapatikana.
Hivyo basi hebu fikiria iwapo Mwenyekiti wa CDM ni mtu mwingine, kwa mfano Zito Kabwe, jee channel hizi za kupata pesa zinaweza kweli kuendelea kuwepo? Swali gumu!
Zito mwenyewe kasema kwenye mkutano Serena kwamba yeye hana pesa hajajilimbikizia fedha. Kama kweli, basi uwenyekiti wake wa CDM ambao watu fulani wanadai ndiyo lengo lake utakuwa ni uwenyekiti wa matatizo makubwa! Akina Mtei hawatamuamini kuchannel fedha zao. Chama kitayumba.
Itakuwa kama vile ilivyoandikwa katika kitabu cha Joan DArc msichana Mfaransa katika Karne ya 15 aliyekuwa maarufu katika kuongoza majeshi na kuweza kuwashinda adui.
Lakini hakuwa anajua fedha za kugharamia majeshi (logistics) zilikuwa zinatoka wapi, na siku moja wakuu wa nchi walimfanyizia jambo ili aelewe hilo. Kwa maana nyingine alitakiwa kujua kuwa umaarafu wake vitani ni sawa, lakini alikuwa anakijua kile kilichokuwa kinamsukuma kupata umaarufu huo?
Mimi binafsi ninapenda kuamini kwamba bomu la Soweto ilikuwa ni kutaka kumuuwa Mbowe (assassination attempt) kwa lengo la kuikatia CDM chanzo kikubwa cha fedha. Napenda kuamini hivyo.
Aidha wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 CDM ilikuwa haina fedha nyingi za ruzuku ya serikali kama wakati huu. Chama kilishindwa kuweka wagombea ubunge katika majimbo mengi tu. Inasemekana fedha nyingi za kampeni katika majimbo hayo na katika kampeni za urais zilitoka kwa akina Mtei.
Matokeo yake ni kwamba katika majimbo ya ubunge hayo waliyoshinda na ukichanganya na viti maalum, CDM imeweza kuwa inajipatia ruzuku ya zaidi ya sh milioni 200 kwa mwezi, (CCM ni zaidi ya sh bilioni moja kwa mwezi).
Kama kweli Zito ananyemelea uwenyekiti kama vile wapambe wake wanavyodai na kwamba mgogoro wote baina yake na uongozi wa juu wa CDM ni huo uwenyekiti basi anakosea saana! Namsihi atambue kwamba yeye bado young sana, achangie umaarufu wake kukisaidia chama kushika dola na iwapo kitashika dola, basi hayo masuala ya fedha ya kuendesha chama yatakuwa yametatuliwa. Na hapo ndipo anaweza kuomba kugombea Uwenyekiti.
Kwa sasa hivi CDM inahitaji fedha, tena fedha nyingi kukiendesha chama, na kama hizo zinapatikana kuotka kwa uongozi wa juu uliopo, wana-Chadema laizime washukuru hilo na tusiharibu mambo.
Nawasilisha. Ni mawazo yangu.