John Mnyika awajibu kisheria wanaohoji kuhusu CHADEMA kutokusaini kanuni za maadili ya uchaguzi 2025

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,210
Reaction score
4,631
Anaandika JJ Mnyika Katibu Mkuu.

Kujibu andiko la Wakili Msomi Jonathan Mndeme
———————

Kabla ya vifungu vya 162(2) na (3) vya Sheria ulipaswa kuanza na 162 (1).

Kifungu cha 162(1) kinaeleza Tume baada ya kushauriana na vyama vyote vya siasa na Serikali itandaa na kuchapisha katika Gazeti la Serikali Kanuni za Maadili ya Uchaguzi.

Kwa kifungu hiki anayendaa Kanuni za Maadili ya Vyama Vya Siasa ni Tume sio kikao kikao kati ya Tume na Vyama na Serikali. Kikao ni sehemu tu ya Tume kutekeleza jukumu la kushirikisha. Baada ya kushirikisha huko Kanuni za Maadili hazipati nguvu ya kisheria mpaka kwanza chapishwe katika Gazeti la Serikali.

Strictly speaking Vyama vilipaswa kutakiwa kusaini Kanuni za Maadili baada ya kuwa kwanza Tume imekaa kikao cha Tume, imezipitisha na zimechapishwa kwenye Gazeti la Serikali.

Soma Pia: Mnyika: Sitakuwepo kuwakilisha Chama kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi 2025 kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi

Hivyo, Serikali na Vyama kusaini kwenye mchakato wa kushirikishwa kama ilivyokuwa tarehe 12 Aprili 2025 hakuzuii Chama ambacho haikusaini wakati huo kusaini baada ya kuwa Maadili ya Vyama vya Siasa kuwa yameshachapishwa kwenye Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Kifungu cha 162(2) cha Sheria.

Ili mradi kusaini huko kufanyike kabla ya kushiriki uchaguzi kwa mujibu wa masharti mabaya(yaliyo kinyume cha katiba na sheria) yaliyoko kwenye Kanuni za Maadili kipengele cha 1.5 (a). Ndio maana hata Kanuni za Maadili zenyewe kuanza kutumika kwake kwa mujibu wa kipengele cha 1.3 kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 ni kuanzia siku moja baada ya tarehe ya uteuzi wa wagombea. Hivyo, Chadema ikiamua kusaini kabla ya uchaguzi inayo nafasi kisheria na haki kufanya hivyo. Nafasi kama hiyo imewahi kutolewa kwenye Uchaguzi Mkuu mmoja wapo wa miaka ya nyuma sikumbuki vizuri mwaka hapa nilipo.

Kwa upande mwingine, kwa taathira ya No Reforms No Election Reforms zikitokea za kikatiba au za kisheria zitasababisha pia reforms za Kikanuni ikiwemo Kanuni ya Maadili ya Uchaguzi na kupelekea mchakato kusaini kufanyika tena.
 
Atakula majibu yake dadeki CCM tumeamua hatucheki na kima

USSR
 
Mnyika umekuwa kipofu kama mwenyekiti wako.Mnaongoza chama kwa kubahatisha
 
Binafsi naona CHADEMA ni kama wamebetia hela ya ada. Waki pata watapata mamilioni. Wakikosa kimewaramba.
 
Afu utamsikia DIBLO DIBADALA anahangaika na wahitimu kwenda veta wakati kuna matahira mengi huko ccm kama haya kina Kailima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…