kamanda kubenea hawezi kuchafuliwa na mtu dhaifu kama huyu anayetegemea 7000 ili aishi .Wivu Kubenea pita huku uone huyu bwana anavyokuchafua
Ni kweli kwamba Mnyika ameongoza hilo jimbo kwa awamu mbili?
Badala ya kulia na serikali ya ccm unalia na mnyika??
Hii tabia ya kuwatetea upinzani kutofanya vizuri majimboni vyao kwa kisingizio kuwa wao sio serikali siyo njema kabisa. Hawa akina Mnyika wanasubiri wapewe habari za ufisadi kisha hao mjengoni kwenda kuripoti mjengoni. Hilo ni jambo jema lakini sio kusudi kuu la sisi kuwachagua.
Wabunge vijana wanabidi wabadilishe jinsi ya kuwajibika kama wabunge. Mimi nilitegemea mtu kama Mnyika ambaye anauwezo mzuri kielimu akamate wasomi wachache waandike miradi tofauti tofauti na kufanisha kutatua matatizo ya watu jimbo lake hata kwa uchache tu.Sio kuitegemea serikali katika kila jambo. Mitaa ya kimara kuna barabara nyingi ni mbovu kabisa lakini kuna watu wenye uwezo wa kipesa na kujitolea kujenga au kuchangia barabara kama hizo pindi kama atatokea mbunge mwenye kuonyesha jitihada na nia ya dhati kutatua tatizo la barabara kwa kukutana na wananchi na kuwapa motisha.
Kwa kweli wabunge vijana wameniangusha sana....tunataka mabadiliko lakini mabadilko halisi yataletwa na wabunge vijana wanoweza kufikiri nje ya box na sio kukaa kwenye viti virefu wasubiri kuongwa habari nyeti za kwenda kupinga ufisadi tu. Bull shiiiiiit
Duu Babeli kumbe mnyika alikuwa anakusanya kodi usituambie bwana. Rais hakuahidi maji,umeme vitakuwa historia miaka kumi iliyopita leo hii vp na kodi kakusanya. Tunapomlaumu mbunge tena wa upinzani kidogo tutumie akili ya kuzaliwa. Angekuwa waziri je si ungemmeza mbunge wa watu. Mnyika hata akigombea Arusha anashinda asubuhi kabla hujaamka kama humtaki wapo milioni 6 wanamhitaji.
Katika wabunge ambao wanajigamba wana solution ya matatizo ya wananchi wao majimboni ni huyu kamanda.
Kamanda umetuangusha sana nadhani ndio maana umekimbia jimbo kwa madai eti unamwachia Kubenea.
Wananchi wako uliwaahidi ndani ya siku 100 utakuwa umetatua tatizo hilo. Hivi katika kipindi chako cha miaka 05 umefanya nini hasa cha maana.
Yaani mnakera sana kwa kuahidi mambo hewa kwa sababu yanarudisha nyuma imani kwa wananchi. Wananchi wapo kwenye vyombo vya habari saa hizi wanalalamika nyinyi mnatesa tu mitaani.
Bwana Kubenea ameamua kubeba mfupa uliomshinda Mnyika ndie atatutia aibu mara mia. Ni kheri hata asingegombea kwa sababu kama Mnyika na ujanja wote kasepa kiaina huyu Kubenea atawezaje.
Ujinga mtupu mnaudhi
Hao ndio wanataka kuongoza nchi wakati majimbo yanawashinda. Ni wapumbavu tu ndio watawapigia kura CHADEMA. Sisi wenye akili zetu, #HapaKaziTu
Hata kibamba hajafanya kitu amwache Dr Mukangara afanye mambo
Kama hata hujui kipindi alichokaa Mnyika bungeni, hauwezi kujua mambo aliyoyafanya !
Wananchi wa ubungo (nikiwemo na mimi) ndio tuliompeleka Mnyika bungeni, ninaamini kwa wale wa kibamba watamrudisha tena bungeni.... Na sisi wengine tuliobaki Ubunge tutampeleka Kubenea bungeni.....
October 25 sio mbali, tuvute subira !
Katika wabunge ambao wanajigamba wana solution ya matatizo ya wananchi wao majimboni ni huyu kamanda.
Kamanda umetuangusha sana nadhani ndio maana umekimbia jimbo kwa madai eti unamwachia Kubenea.
Wananchi wako uliwaahidi ndani ya siku 100 utakuwa umetatua tatizo hilo. Hivi katika kipindi chako cha miaka 05 umefanya nini hasa cha maana.
Yaani mnakera sana kwa kuahidi mambo hewa kwa sababu yanarudisha nyuma imani kwa wananchi. Wananchi wapo kwenye vyombo vya habari saa hizi wanalalamika nyinyi mnatesa tu mitaani.
Bwana Kubenea ameamua kubeba mfupa uliomshinda Mnyika ndie atatutia aibu mara mia. Ni kheri hata asingegombea kwa sababu kama Mnyika na ujanja wote kasepa kiaina huyu Kubenea atawezaje.
Ujinga mtupu mnaudhi
Umezungumza kweli kabisa. Kama makamanda tunaahidi kwa kuitegemea mgongo wa ccm basi tuwe na uhakika na tunachoahidi sio kutapeli wananchi. Tusitumie kutokuelewa kwa wananchi kuwa ni faida na fursa kwetu. Tuwe wakweli na basi tuahidi yale tutakayoyamudu basi. Na kamwe tusiitupie ccm lawama kwa lolote kwa sababu nafasi za ubunge wananchi wananchi wametupa sisi na sio wa ccmKwanini aliahidi? au hawa wanaoahidi sasa kuna haja gani ya kuwachagua ikiwa wanaitupia lawama ccm!? bora kumpa mgombea wa ccm atatupa majawabu. Masaburi oyeeeee!