Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,607
Kwa umahiri wake katika siasa Mheshimiwa John Magale Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanasiasa wenzake walimpatia jina la DROGBA (Mshambuliaji hatari wa timu ya Chelsea wakati huo)
Mnamo Mwaka 2009 - 10, wakati wa kupanda kwa "joto la kisiasa" ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Shibuda akiwa ni mwanachama wa chama hicho na Mbunge pia, alipatwa na joto hilo, pale ambapo alipishana lugha na wenzie ndani ya Chama na baadae kufanya maamuzi ya hasira na kuhamia CHADEMA ambako alipokelewa kama LULU na kutangazwa nchi nzima na viongozi waandamizi wa Chama hicho.
Kwa namna ya mapokezi yake yalivyokuwa hakuna aliyeweza kuamini wala kutegemea kuwa huo ulikuwa ndio mwanzo wa kifo cha kisiasa cha mkongwe, nguli na mbabe huyo wa kisiasa hapa nchini.
Hakuna kilichomponza zaidi ya rekodi ya mafanikio yake, uwezo wake na utashi mkubwa alionao katika siasa za ndani na nje ya nchi, MAARIFA ya JOHN MAGALE SHIBUDA yaliwatia hofu Viongozi wa CHADEMA juu ya nafasi zao, vyeo vyao na hatma yao ndani ya Chama hicho.
Zengwe likaundwa, watu wakaandaliwa na vihunzi vikatengwa kuhakikisha kuwa SHIBUDA ananasa, anadhibitiwa na anapotezwa, ndivyo ilivyokuwa kwani muda mfupi tu, tuhuma zikaanza, malalamiko yakasikika na mishale ikarushwa kwa Shibuda, alikwepa mingi lakini hakuweza kukwepa yote, alitandikwa, akapewa jina MSALITI, akachafuka hatimae kupotezwa..
Kwangu mimi huyu bwana ni Mwalimu wa siasa, ni hazina na njia ya kuifuata katika mapito ya kisiasa. Namtafuta- DROGBA, nataka kuona umahiri wake, ufundi wake na maarifa yake hivi sasa akiwa na wakati mgumu kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.