John J. Mnyika - 2025 And Beyond

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,299
3,055
Ndugu John John Mnyika ni aina ya watu na kiongozi ambaye kama Taifa tunamhitaji sana (itikadi, mambo binafsi pembeni).

Kijana huyu ni mtu wa kuandaliwa, kufundishwa, kuelekezwa, kutiwa moyo, kutunzwa vema, ndio na kuombewa; ili siku moja alitumikie Taifa letu Tanzania katika nafasi ile, kwa kadiri ya kipawa, tabia, moyo na uwezo mkubwa wa uongozi Mwenyezi Mungu aliomkirimia. Huyo atalitoa Taifa hili hapa tulipokwama na kutupeleka mahali pa juu na bora kuliko wote waliomtangulia. Sio ndoto, ni maono halisi.

John Mnyika ni hazina na tunu ya kiongozi. Tumuombee afya njema na maandalizi mema ya kuja kulitumikia Taifa letu kwenye ngazi stahiki ya juu.
 
Ninaweza kukuunga mkono kwa hili, lakini hujaeleza chochote cha maana sana.

Ni nini hasa kimekusukuma ukalaka mjadala juu yake wakati huu?

Mpe nafasi aonyeshe uwezo wake zaidi katika miaka hii inayofuata kabla ya huo muda, aendelee kujenga matumaini ya watu kwa uwezo wake, na hapo ndipo utakuwa na nafasi nzuri ya kumpigia debe.

Sasa hivi unammulikia mwanga hafifu, pengine mwanga utakaozima matumaini yake kabisa.
 
Mnyika ndio anatakiwa kuwa Makamu wa Rais, nawashangaa watu wanapiga kelele tu sijui Makamba na nani, hao hawana utendaji wowote wamezoea kupachikwa tu madarakani.

Mama Samia afanye kama Magufuli alivyofanya kwa Mama Mghwira kule Moshi, chukua kijana bright huyo mchape kazi ule wakati wa kuishi kwa mazoea umepita.
 
Kama unayosema kweli kuhusu mnyika, atoke hadharani ahoji ukomo wa mwenyekiti chadema
Hapo ndio utaelewa HAKUNA kitu
Ili mbowe aondoke madarakani ccm ibadilishe utaratibu wao kikatiba mwenyekiti wa ccm taifa lazima awe rais, hivo ili ujadili ukomo wamwenyekiti mbowe basi angalia pia ukomo wamwenyekiti wa ccm.tafakari hilo
 
Itakuaje tukimuona Babaeni Lissu ikiwa na matamanio ya madaraka 2025. Mnyika atatumbia nn? Au ndo atatengeneze chama chake...
Mnaitaji muda kujinadi tena katika masoko makubwa ya siasa Kama haya..

mnavoongoa na kutembea kwenu mnaonekana ni wana wa Yuda....😂😂😂
 
Ili mbowe aondoke madarakani ccm ibadilishe utaratibu wao kikatiba mwenyekiti wa ccm taifa lazima awe rais, hivo ili ujadili ukomo wamwenyekiti mbowe basi angalia pia ukomo wamwenyekiti wa ccm.tafakari hilo
Ccm mbona ipp wazi? HAKUNA mwenyekiti aliyezidi miaka 10
 
Back
Top Bottom