John Heche: Lissu ana siku 350 Gerezani

John Heche: Lissu ana siku 350 Gerezani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,472
Reaction score
14,786
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, ameiomba Mahakama iitishe na kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu ili kesi iishe na Lissu akafanyiwe matibabu ambapo amesema kama Lissu atapatwa na lolote akiwa gerezani kuna Watu watalazimika kujibu ni nini kimempata.

Akiongea Jijini Dodoma leo Machi 24, 2026, Heche amesema “Juzi Mwenyekiti wetu (Lissu) akiwa gerezani ameandikia Mahakama wa Rufani kwa hati ya dharura kusikiliza kesi dhidi yake ya Uhaini na kuifanyia maamuzi, sote tunajua Lissu alishambuliwa kwa risasi hapa Dodoma kwahiyo kila baada ya muda amekuwa akienda kwenye matibabu na check up”

“Suala la afya yake ni concern ya Chama na Watanzania leo ni siku 350 bado siku 15 Mwenyekiti wetu atakuwa ametimiza mwaka mzima gerezani kwa kesi ya uongo na ya kutunga, Watu wanataka wamtishe apige magoti, tunalizungumza kwasababu ya afya yake angekuwa mzima hata wakiendelea na kesi miaka mitatu tusingepiga magoti”

“Hii naileta kwenu Watanzania, lolote litakalompata Tundu Lissu akiwa chini ya hawa Watu watakuwa na sababu ya kueleza Watanzania nini kimetokea, haitakubalika, Chama chetu hakitokubali, Duniani haitokubali, hii kesi isikilizwe haraka iishe Mwenyekiti wetu akapate matibabu, kitendo cha kuendelea kumshikilia kama madhara yatatokea kuna Watu watalazimika kujibu”

 
Back
Top Bottom