Kuna jogoo kataga yai hapa ni dogo tofauti na ya majike.
- Tunachokijua
- Jogoo ni kuku wa kiume aliyekomaa
Je, jogoo anaweza kutaga?
JamiiCheck imepitia machapisho na tafiti kuhusu kuku kutaga mayai na kubaini kuwa Jogoo haliwezi kutaga mayai kama inavyoelezwa.
Tovuti ya BackYard Chickens inaeleza kuwa miongoni mwa maswali mengi yanayoulizwa kuhusu kuku ni iwapo Jogoo anaweza kutaga mayai? Ambapo tovuti hiyo inabainisha kuwa Jogoo hawezi kutaga mayai bali yupo kwa ajili ya kururtubisha mayai ya kuku jike.
Inaelezwa kuwa tukio la awali kabisa la Jogoo kutaga yai lilirekodiwa Basel, Uswisi mwaka 1474 ambapo Jogoo hilo lilihukumiwa kifo “Uhalifu usio wa kawaida wa kutaga yai.” Tukio kama hilo lilitokea tena nchini Uswisi mwaka 1730.
Nchini Marekani, mwaka 1922, “jogoo” wa aina ya brown Leghorn huko Madison, Wisconsin, alianza kutaga mayai.
Ili kuthibitisha hilo, Idara ya Ufugaji wa Kuku katika Kituo cha Majaribio cha Wisconsin ilimfungia ndege huyo kwenye zizi lililoundwa kwa namna ambayo watu wenye mizaha wasingeweza kuingiza mayai kwa siri. “Jogoo” huyo alitaga yai moja kila siku.
Je, ni kwanini inaonekana ama kuaminika kuwa Jogoo anataga?
Tovuti ya Cackle Hatchery inabainisha kuwa Jogoo linaloonekana kutaga mayai inaweza kuwa imesababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo
Mabadiliko ya ghafla ya Jinsia
Kuku jike ana ovari mbili ambapo inayofanya kazi ni moja ya upande wa kushoto na iwapo ovari hiyo itaathirika na kushinda kufanya kazi zake ndipo Ovari ya kulia inaweza kukua na kuwa na mchanganyiko wa ovari na korodani.
Na hapo ndipo kuku jike anapoanza kuwa na tabia za jogoo ikiwemo kukua kwa kishungi, anaweza kuwika, kupanda kuku jike wengine, kubadilisha manyoya na kufanana kama jogoo.
Mabadiliko ya Homoni