Jogoo akiwikia kulia kuna madhara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jogoo akiwikia kulia kuna madhara?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Oct 4, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,219
  Likes Received: 5,617
  Trophy Points: 280
  Jogoo akiwikia kulia kuna madhara?
  Written by Administrator
  Sunday, 04 October 2009 07:24

  pole na majukumu ya kila siku, mimi naitwa Docras naishi Mbeya, nimeolewa miaka saba iliyopita na kwa muda wote huo sikuweza kupata mimba.

  Kwa bahati nzuri hivi sasa nina ujauzito wa miezi miwili, nilisikia kuwa jogoo la mwanaume likiwa tayari kufanya kazi likiwa limelalia kulia hizo ni dalili kuwa bunduki zake haziwezi kumpa mwanamke ujauzito, naomba unieleze usahihi wa madai hayo.

  Kwanza nakupa hongera kwa kuweza kupata ujauzito maana kipindi cha miaka saba uliokaa si haba. Pia nampongeza mume wako kwa uvumilivu maana wengi wanakata tamaa na kuanza kurukaruka.

  Kuhusu swali la msingi, kusema ukweli mtu aliyekupa mchapo huo alikuwa anakudanganya. Jogoo kama anawika, basi atawika tu na bunduki zake zitafanyakazi kama kawaida bila kujali umelalia upande gani.

  Suala la jogoo kulalia upande gani, inategemea na uamuzi wa mtu mwenyewe atakavyotaka kumhifadhi katika kabati yake. Akiamua alalie kulia, sawa, kushoto poa tu hata katikati hiyo hawezi kumfanya ashindwe kutimiza wajibu wake. Kwa hiyo dada yangu hilo lisikupe hofu, ni uzushi tu ambao watu wameuanzisha na kuueneza.

  Ananizengea kimabavu

  KWAKO Anti Lisa, mimi ni msichana kwa bahati nzuri au mbaya ametokea mwanaume mmoja ambaye ameoa ana familia ametokea kunipenda lakini nimemkatalia, sasa amehamia kwa rafiki yangu. Kinachonipa wasiwasi ni vitisho vyake anavyonitolea hadi nakosa amani,je huyu baba ana nia gani na mimi? Naomba ushauri wako. Wako Dada S. wa Tabora.

  Pole sana dada yangu na vitisho unavyopata kutoka kwa huyo mwanaume. Pia nakupongeza kwa msimamo wako na ninakusihi uendelee hivyo hivyo.

  Kuhusu vitisho anavyotoa dhidi yako, nakushauri uchukue hatua za kisheria kwa kuripoti suala hilo kituo chochote cha polisi kilichopo karibu na wewe.

  Nakusihi usipuuze vitisho hivyo kwani inawezakana akakudhuru. Ikibidi pia mwambie hata mke wake jinsi mume wake anavyokufuatafuata naamini atamkanya. Mwanaume huyo siyo wa kuchekea kwani inaonekana siyo mwaminifu ndiyo maana ameshindwa kutulia na familia yake. Vitisho vyake visikufanya ukamkubalia matakwa yake ambayo naamini matokeo yake yatakuwa siyo mazuri.

  Nikiachana na mwanamke anaugua

  ANTI Lisa habari za leo, naitwa Ibra, nipo Kilwa Masoko, swali langu ni kuwa ninapoishi na msichana na baadaye nikaamua kuachana naye basi nikimwambia anakuwa mgonjwa na wakati mwingine kulazwa hospitali. Hiyo imetokea kwa wasichana wengi ambao nimekuwa nao na uhusiano wa kimapenzi. Naomba ushauri nifanyeje?

  Kaka yangu inavyoonekana wewe ni mwanaume wa ajabu. Inashangaza kuona katika kipindi hiki cha UKIMWI bado unaendelea kurukaruka kwa kubadilisha wanawake **** nguo.

  Inabidi ufahamu kuwa mapenzi ya dhati yanatoka moyoni, wale wasichana wamekuwa wakikupenda kwa dhati na dhamira yao inakuwa na matumaini na wewe bila kujua kuwa wewe ni tapeli wa mapenzi.

  Wanapokuwa wamejipa matumaini kuwa wamepata mwanaume wewe unawakoroga. Tabia hiyo siyo nzuri, nakushauri utafute mpenzi mmoja ambaye utadumu naye.

  Kadiri unavyobadilisha wapenzi unakuwa unajitengenezea mapito ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

  Naogopa kumweleza bosi

  Shikamoo Anti Lisa, mimi nifanyakazi kwa mtu sasa nimepata rariki tuna zaidi ya miaka miwili, bosi wangu hafahamu na ninaogopa kumwambia kwani nahisi atachukia. Kijana huyo anataka awe mchumba wangu na ana mipango ya kuja kujitambulisha kwake na baadaye aende kwa wazazi wangu kulipa mahari. Je,nifanyeje? Wako Upendo wa Dar es Salaam.

  Mdogo wangu hiyo bahati siyo ya kuchezea, nakushauri utafute mtu yeyote ambaye yupo karibu na bosi wako, umueleze hali halisi ili aweze kumfikishia ujumbe.

  Iwapo utaona njia hiyo ni ngumu kwako, basi nakushauri umwambia mchumba wako huyo atume washenga kwa bosi wako wako waende kujitambulisha. Mshenga akifika kwa bosi wako na kueleza kilichompeleka, utaitwa na kuulizwa kama ni kwali na ukikubali naamini mambo yataenda vizuri.

  Usiogope hilo ni jambo la kheri nina imani kuwa bosi wako hawezi kuchukia. Hata hivyo nakusihi uwe makini maana siku hizi kuna wanaume wengi wanaowaingia wasichana kwa gia ya kuoa, wakishapata wanachokihitaji wanaingia mitini.

  Hataki tutumie kondomu, nimkubalie?

  Habari yako Anti Lisa, mimi nina rafiki yangu wa kiume ambaye ni Polisi, nimekuwa nikifanya naye mapenzi kwa kutumia kondomu lakini anadai hasikii raha anataka tuache kuzitumia, mimi naogopa, naomba ushauri, ni mimi Vicky.

  Mdogo wangu Vicky nakushauri usimkubalie mwanaume huyo, hana nia nzuri na wewe.

  Kama atakupenda ni lazima akulinde kwa kufanya mapenzi na wewe kwa kutumia kondomu. Usikubali kufanya naye mapenzi bila kondomu kabla hamjapima afya zenu ili kujua kama mna maambukizi ya VVU au la.

  Mwambia kama hataki, basi atafute mwanamke mwingine ambaye atakuwa tayari kwa hilo. Ukiona mwanaume ana tabia hiyo, basi ujue anafanya hivyo hata kwa wanawake wengine. Chonde chonde usimkubalie kama asikii raha atafute kwingine.
   
Loading...